Watumishi 15,578 waliobainika kughushi vyeti na kupata ajira hawastahili kurudishwa kazini wala kulipwa malipo yoyote!

Inaumiza, inauma sana, imetugharimu sana tuliokutwa au ndugu zetu kukutwa na janga hili lakini ni muhimu kufanya mambo sahihi kadri inavyotakiwa

Mimi binafsi watu wangu wa karibu sana wamepigwa na hili janga na familia zimeyumba na imetugharimu lakini kamwe siwezi kuilaumu serikali na kumtetea mtu aliyenunua au kughushi vyeti. Kamwe!!!!

Kosa ni kosa tuu haijalishi linakufaidisha au kukubeba kwa kiasi gani

Usiangalie kosa katika kughushi tu, angalia kosa katika kumwajiri, kosa katika kukubali utumishi wake kwa miaka mingi, kosa katika kuikubali kodi yake kwa miaka mingi.

Pamoja na kosa walilofanya, zile 10% zao za mafao walizokatwa wakipewa huo ni ubinadamu lakini wengi wao wameshakubali adhabu na pengine wana maisha yenye mwanga kuliko waliochukua hayo maamuzi. Siwatetei, mm ni muumini wa utu.
 
Kosa la kumwajiri lingetokea wapi kama asingefanya kosa la kughushi na kumuongopea mwajiri?
Kuhalalisha haramu nalo ni kosa lingine. Haramu haijawahi kuwa halali hata ukaitetea vipi

Kuumizwa tumeumizwa, kuumia tumeumia lakini tusijibebmbeleze ati tumeonewa. Kukubali kosa ni jambo jema
 
Umesoma ukaelewa?
Sijasema kaonewa mtu. Wanastahili yaliyowapata ila kama watapewa zile 10% walizokatwa kwenye miahahara still bado huo utakuwa ni utu tu.

Ni Sawa na kumtupa mhalifu jangwani na ukampa chupa ya maji ya kunywa.

Halafu wewe hujaumizwa ila ni tetea tetea wa serikali, usitumie nguvu sana kutetea maana hata hao yaliowakuta wamekubali makosa na wanaendelea na maisha.
 
Mwizi ni mwizi haijalishi hata, umeghushi vyeti then unataka ulipwe?
 
Bajeti ya 21\22 ni kama 33t, ya mwaka 22/23 ni kama 39t. Kutakuwa na bonge la ongezeko la mshara. Hakuna atapungukiwa take home ya 50,000 kwa kima cha chini. Mama oyee
Lini bajeti yetu ilianyiwa kazi 100%?
 
Roho mbaya inakutesa ka jiwe kukomoa komoa
Yani kulipa watu walioiba na kughushi vyeti ni sawa? Hii nchi haitakaa ifike mahali kwa mentality hizi wallah! Kama mnawekwa kwenye decision making na mentality hizi unadhani tutafika kweli?
 
Ilibidi wote wafukuzwe akiwemo yule kijana pendwa aliyekuwa RC jiji la maraha.
Kama wengine walipendelewa wakaachwa na wengine wakafukuzwa huo ulikuwa ni uonevu wa kiwango cha 5G.
Mungu atusaidie
 
Umesoma ukaelewa?
Sijasema kaonewa mtu. Wanastahili yaliyowapata ila kama watapewa zile 10% walizokatwa kwenye miahahara still bado huo utakuwa ni utu tu.

Ni Sawa na kumtupa mhalifu jangwani na ukampa chupa ya maji ya kunywa.

Halafu wewe hujaumizwa ila ni tetea tetea wa serikali, usitumie nguvu sana kutetea maana hata hao yaliowakuta wamekubali makosa na wanaendelea na maisha.

Hilo la mimi kuumizwa au kutoumizwa sijakulazimisha kuniamini. Nikiamini mimi mwenyewe inatosha

Kikubwa Tujifunze kuacha udanganyifu, tujifunze kukubali makosa yetu na kuyabeba! Udanganyifu wa vyeti ni wizi kama wizi mwingine
 
Hii nchi imejaa siasa nyingi za hovyoo...mtaani kuna vijana wengi tu wamemaliza vyuo na hawana ajira..ila serikali inakomaa na wazee walioghushi vyeti pamoja na umri.....ila pia kitu nilichojifunza katika suala la utafutaji adui yetu mkubwa sisi vijana wa leo ni hawa wazee........wazee wanatupiga vita za chinichini.....
 
Zamani ulikuwa ukifaulu na wazazi wako hawaeleweki jina anapewa mtu mwingine imagine ni wewe umefaulu afu jina lako liuzwe?
 
Hilo la mimi kuumizwa au kutoumizwa sijakulazimisha kuniamini. Nikiamini mimi mwenyewe inatosha

Kikubwa Tujifunze kuacha udanganyifu, tujifunze kukubali makosa yetu na kuyabeba! Udanganyifu wa vyeti ni wizi kama wizi mwingine
Hatuelewani. Haya mafunzo unayotoa unajiweka kwenye utakatifu fulani. Mm sijaongelea utakatifu. Nimeongelea kuwa hakuna ubaya wakipewa ile michango na sijasema wizi ni jambo sahihi. Wasipopewa pia hawatakuwa wameonewa. Usihubiri.
 
Mimi sijasema kuwa ni mtakatifu, wala kujiweka kwenye utakatifu, wewe ndio umeniwazia hayo.
Nilichokisema ni kwamba kughushi au kuiba vyeti ni kosa. Na siwezi kusema ni sawa ili kukuridhisha wewe

Kuhusu kupewa hiyo michango sijasema kwamba kuna ubaya. Ila kabla hatujadai hiyo michango kwa kulalamika na kulazimisha wataalamu wa sheria watuambie pia kuna adhabu au gharama gani kwenye kosa la kughushi kwa kukusudia

Narudia kusema tusiangalie tulipoumizwa au kuumia, tujiulize nani amepelekea sisi kuumizwa. Na nani aliyeghushi?
 
Usiangalie kosa katika kughushi tu, angalia kosa katika kumwajiri, kosa katika kukubali utumishi wake kwa miaka mingi, kosa katika kuikubali kodi yake kwa miaka mingi.

Pamoja na kosa walilofanya, zile 10% zao za mafao walizokatwa wakipewa huo ni ubinadamu lakini wengi wao wameshakubali adhabu na pengine wana maisha yenye mwanga kuliko waliochukua hayo maamuzi. Siwatetei, mm ni muumini wa utu.
Kuiba na kutokujulikana hakuhalalishi wizi......
 
Mimi sijasema kuwa ni mtakatifu, wala kujiweka kwenye utakatifu, wewe ndio umeniwazia hayo.
Nilichokisema ni kwamba kughushi au kuiba vyeti ni kosa. Na siwezi kusema ni sawa ili kukuridhisha wewe

Kuhusu kupewa hiyo michango sijasema kwamba kuna ubaya. Ila kabla hatujadai hiyo michango kwa kulalamika na kulazimisha wataalamu wa sheria watuambie pia kuna adhabu au gharama gani kwenye kosa la kughushi kwa kukusudia

Narudia kusema tusiangalie tulipoumizwa au kuumia, tujiulize nani amepelekea sisi kuumizwa. Na nani aliyeghushi?
Sawa. Ni kosa hilo linajulikana.
Hoja yangu ilikuwa kama wakipewa zile 10% walizokuwa wanakatwa hakuna ubaya na wasipopewa hawawezi kulalamika sasa wewe ukawa unaendelea na mahubiri ya wizi na unyang'anyi.
 
Yani kulipa watu walioiba na kughushi vyeti ni sawa? Hii nchi haitakaa ifike mahali kwa mentality hizi wallah! Kama mnawekwa kwenye decision making na mentality hizi unadhani tutafika kweli?
Ccm yenyewe huiba kura sembuse waliofoji vyeti?
 
Back
Top Bottom