gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,312
- 3,345
Waziri wa Fedha, usiwatoe kafara watendaji wako. Wewe ndiye chanzo cha mayowe ya kodi kandamizi kwa wafanyabiashara
Ndugu zangu wanabodi, huwa napenda sana kuishi kwa kujifunza kutoka kwenye hotuba za viongozi na kupitia hotuba hizo huwa nanyakuwa baadhi ya mambo ambayo kwangu ninayoyaona yanamantiki.Ipo hotuba moja iliwahi kutolewa na Rais wa sasa Mh. Magufuli na kwenye hotuba hio alikuwa akilalamika kwamba licha ya tanzania kuwa na idadi kubwa ya watu kuliko nchi zilizotuzunguka lakini ndio nchi ambayo idadi yake ya walipakodi (tax base) ni ndogo kuliko nchi ambazo zinawananchi(population) wachache. Ni dhihiri hapa ndipo kulitakiwa kuwekewe mkazo lakini badala yake kodi inakusanywa kwa faini na kubambikizia wafanyabiashara kodi kubwa.
Zipo taarifa zinazagaa kwamba TRA wapewa target yakukusanya trilioni mbili kwa mwezi. Mimi sina tatizo na hili lakini tatizo langu ni mkakati haramu uliolenga kuwaongezea na kuwabambikizia wafanyabiashara kodi ili ku meet target.
Mh. Mpango anapaswa kujua hawa watendaji 22 aliowasimamisha kazi wapo ambao wamelazimika kuwabambikizia kodi kubwa wafanyabiashara ili kulinda nafasi zao kwani wasipofikia lengo nafasi zao zipo mashakani.
Mh mpango anapaswa kujua hii target ya trillion mbili kwa mwezi imekua si mwiba tu kwa wafanyabiashara ila pia imekua ndio chanzo cha wafanyakazi wa TRA kukosa uadilifu.
Nasisitiza mtambue hali huku mtaani imekua mbaya sana, zamani watu walikua wakiogopa polisi lakini leo TRA wanahofiwa zaidi ya chochote.
Nimelizie kwakisema kama chanzo cha haya machungu tunayoyapitia wananchi kwa sasa ni umeme wa Stigglers basi ni heri tukarudi kwenye mgao wa umeme hii miradi ikasimama kuliko haya mateso ya TRA.
Mh Mpango nakusihi twendeni taratibu tutafika lakini huu mwendo wa sasa sio sawa na mayoe yataendelea kuwa mengi kila mahali.
====
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ameagiza watumishi 22 wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.
Amesema wameshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kujihusisha na ufisadi na kuikosesha Serikali mapato na kumtaka kamishna mkuu wa mamlaka hiyo, Dk Edwin Mhede kuwasimamisha kazi.
Amebainisha kuwa wanatuhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa, kutosimamia ipasavyo matumizi ya mashine za kutolea stakabadhi (EFD’s), kuwabambikia kodi kubwa wafanyabiashara na kuagiza apatiwe taarifa ya utekelezaji wa maelekezo yake ndani ya siku 90 kuanzia leo.
Dk Mpango ametoa maagizo hayo leo Jumatano Desemba 16, 2020 mjini Dodoma katika kikao kilichozihusisha bodi za wakurugenzi, menejimenti na mameneja wa mikoa wa mamlaka hiyo.
Lengo la kikao hicho ilikuwa kupanga mikakati namna ya kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini pamoja na kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato ya kodi na maduhuli ya Serikali.
“Nakuagiza kamishna mkuu uwapumzishe kazi kuanzia leo kwa mujibu wa kanuni ya 37 ya Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2003 na umwagize mkuu wa idara ya mambo ya ndani awachunguze wahusika wote ndani ya siku 90 na nipatiwe nakala ya taarifa hiyo ya uchunguzi na hatua zilizochukuliwa dhidi ya kila mmoja wao,” amesema Dk Mpango
Chanzo: Mwananchi