Bonde la Baraka
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 4,580
- 7,943
Kwema wakuu?
Miaka iliyopita mshahara ukitoka tu Maza alikuwa ananiambia nikamtolee fedha yote nitakayoikuta kwenye akaunti yake pindi tu mshahara unapoingia.
Nikifika tu NMB nakutana na foleni kubwa sana. Nikienda tarehe za kawaida kwa issue zingine pale Benki nikichungulia ATM sioni foleni kubwa.
Hii nimeishuhudia pia nilipoingia kwenye Utumishi wa Umma. Watumishi wa Umma na Wafanyakazi wa kampuni binafsi Tanzania hali zao ni ngumu, Waajiri wanakiuka haki za waajiriwa wao.
Waajiri (mabosi) wanawatesa watumishi wao kwa kuwapatia maslahi kiduchu huku wao wakipata viyoyozi nyumbani, kazini na barabarani. Watumishi wengine wana madeni mengi, furaha yao ni siku 5-10 tu ndani ya mwezi.
Mwingine anaweza kusema kama maslahi madogo acha kazi, na mwingine anaweza kusema shukuru maana wengine hata hicho kidogo hatuna, hizi ni hoja dhaifu na hazipaswi kutolewa na mtu mwenye akili timamu.
Viongozi Waandamizi muzipitie Sera za Utumushi.