KERO Watumishi wa Afya - Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, Mbeya, tunaomba timu ya DMO ivunjwe na uchunguzi ufanyike

KERO Watumishi wa Afya - Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, Mbeya, tunaomba timu ya DMO ivunjwe na uchunguzi ufanyike

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Watumishi wa afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, Mbeya, tulitoa malalamiko kuhusu DMO, In-charge wa Hospitali ya Wilaya, Katibu wa Afya wa Wilaya na timu yake ya CHMT, tukidai kuwepo kwa matumizi mabaya ya mapato ya hospitali kwa starehe, ikiwemo safari za Matema Beach, wakati watumishi hatulipwi stahiki zetu za uhamisho, likizo, extraduties na calls.

Mwezi Julai 2026, timu ya ukaguzi kutoka mkoa ilifika kuchunguza malalamiko yetu na tukahakikishiwa kuwa kungefanyika mabadiliko ya viongozi na kuhakikisha tunalipwa haki zetu. Hata hivyo, jana CHMT ilivunjwa, lakini DMO amewarudisha baadhi ya watu muhimu katika nafasi zao, akiwemo MOI na Katibu wa Wilaya. Pia, DNO amewekwa mtu ambaye tunadai ni mpenzi wake.

Tunaomba uongozi ubadilishwe kwa sababu tunaona maagizo yaliyotolewa na timu ya mkoa hayajafanyiwa kazi. Watumishi tumekata tamaa ya kazi, na tunapojaribu kuomba uhamisho kutokana na mazingira magumu ya kazi, tunanyimwa.

Tunaomba timu ya DMO ivunjwe upya na uchunguzi ufanyike, ikiwemo uwezekano wa DMO na Katibu wake kuhamishwa. Tunadai kuwa baadhi ya watumishi wenye weledi, wakiwemo wenye shahada, hawawekewi mazingira ya kutumia uwezo wao, huku wengine wakipewa nafasi kwa misingi isiyoeleweka. Tunaomba mamlaka husika zisikilize kilio chetu na kuhakikisha haki za watumishi zinalindwa.
 
Back
Top Bottom