Watumishi wa Mungu wamekuwa wakame rohoni sasa makanisani wanafundisha falsafa za kidunia, Falsafa ambazo unaweza kuzipata popote

Ukiona umeshaanza kuwaponda na kuwadharau wachungaji ujue kiburi tayari kimeshakuvaa!! Hata kama hayo uliyoandika ni kweli lakini hukupaswa kufanya hivyo!! Ulipaswa kuwaombea na kuongea nao kwa upendo!! Uko hatarini sana kama haujui!!
 
Kuna huyu anaitwa Tony Kapola ndiyo yupoyupo tu. Yaani hamna neno ila ujanjaujanja tu.
Kapola ukitaka kujifurahisha na kuwa motivated ndo anafaa umsikilize ila kama ni mambo ya kiroho na ukiristo wa matendo huyo wala hashughuliki nao yeye ni maisha ya mwili tu!
 
Kanisa limejengwa juu ya mitume na manabii

Kama tunataka kurudisha kanisa (mwili wa kisiri wa Yesu Kristo) kama vile lilivyotenda kazi katika kitabu cha Matendo ya Mitume Basi turudi kwenye basics zile zile walizokuwa nazo mitume kwa sababu yeye Mungu hana kigeugeu (Malaki 3) Yesu Kristo ni yeye yule Jana Leo na hata milele (Ebr 13:8)

Mungu akija Leo hatauhukumu ulimwengu kwa taratibu/mapokeo/kanuni za Imani za kikatoliki,kilutheri,kipentekoste, Methodist, Anglican, Baptist,Kisabato,mashahidi wa Yehova etc

Ulimwengu ukihukumiwa kwa mapokeo ya kilutheri basi Wote tumeangamia, ukihukumiwa kwa mapokeo na kanuni za Kisabato basi wengine wote tumekwisha.

Mungu atauhukumu ulimwengu kwa Neno lake (Mbingu na Nchi zitapita ila hilo Neno halitopita)

Turudi basi kwenye basics za Matendo ya Mitume (sio kwa mihemuko) namna walivyobatiza, namna walivyomhubiri Kristo.

Kwa sababu Mkuu wa wajenzi Paulo aliuweka msingi na akasema kwenye Wagalatia 1:8 (ikiwa malaika kutoka Mbinguni au mtu mwingine yeyote atawahubiri injili nyingine tofauti na hii niliyohubiri na alaaniwe)

Bible mwishoni imetoa onyo ukiongeza au ukipunguza jina lako linaondolewa kwenye kitabu cha uzima,na mapigo utapata.

Turudi kwenye basics za kanisa la kwanza la kibibilia sio tasfiri za watu walizojiwekea creeds (kanuni za imani) and Dogmas (mafundisho ya sharti)

Asanteni.
 
Ile misingi migumu sana ila ndio ukristo.
Kanisani kuna watu wana magari mpaka mengine yamepitwa na fashion kwao hawawezi tena kuyatumia wameyajaza tu uani, the same church binti anapita mbele kuombewa na hao mabwana na mabibi wenye mabilioni ili binti apate hitaji lake ambalo ni mtaji wa karanga na maji katoni 5 (sh. 50 elfu tu).
Hapa ndipo lilipoanza tatizo
 
Hakika
 
Nishangaa jamaa ombaomba mbezi anamafuta ya upako. Kila baada ya muda anajipaka ili kuvuta wateja.

Injili ya sasa hivi, soma vitabu vya Kiyosaki, Brian trecy, Robert Green, Robin Shama, new age motivational speakers and get rich quickly books. Changanya na tuvitabu vtwa Oyadepo, Keneth, Jakes, Ben hinn, na vifungu vya biblia. Kama kanisa liko mjini, changanya na kakiingerezaSwahili.
Utakula pesa.

Naunga mkono thread. Mimi napenda pure Gospel. Hata nikiwa church ukianza maujinga ya kuongea vitu vya kidunia na kujipendekeza nafungua biblia nasoma sikusikilizi, na sifuati chochote utakachoamuru, ikiwemo kurudiarudia maneno au kufanya vitendo. Ila simchukii mtoa masimulizi hayo.
 
Kuna huyu anaitwa Tony Kapola ndiyo yupoyupo tu. Yaani hamna neno ila ujanjaujanja tu.
Anawaiga wakina Apostle Joshua Selman. Wanasoma vitabu vya motivesheni na kutafuta vifungu vya kuunganishia. Injili hizo wasikilizaji kuacha dhambi ni mziki.
 
Bila Shaka wewe ni mtumishi pia ndiyo maana umeweza kuyaona haya, tena siyo tu mtumishi jina ila ni mtu uliyebahatika kuijua kweli kwa sehemu yako na unajua utakatifu ni nini. Mungu atusaidie wanadamu tumetingwa na changamoto za dunia
 
Huo ndiyo ukomavu na ufahamu wa kiroho, siyo kuburuzwa tu kama kondoo wanaopotea wanaoenda kuchinjwa
 
laiti mngejua ni nini maana ya kanisa.

huko mnakosema ni makusanyiko tu ya watu hayajafikia level za kuitwa "kanisa". kanisa ni kitu kitakatifu!


Yesu ni Kristo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…