Watumishi wa Mungu wamekuwa wakame rohoni sasa makanisani wanafundisha falsafa za kidunia, Falsafa ambazo unaweza kuzipata popote

Injili ya kale ya akina Petro ilikuwa Rhema.
Rhema ni neno la Mungu kwa wakati husika. Yaani Mungu anasema kwa kinywa cha mtu. Anaweza kutumia neno hili la kila siku (logos) ila anaposema Mungu mwenyewe hulitia uzima na kutimiza kusudi lake kwa haraka kama umeme.
Ndio maana ukisoma kitabu cha Matendo ya mitume kimejaa matendo makuu mpaka kitabu kikaitwa MATENDO YA MITUME na si mausia au maneno ya mitume.
Anania na safira walipofanya udanganyifu Petro alitamka neno Rhema na ikawa vivyohivyo.
Sasa hivi wewe hata ukipeleka sadaka pesa uliyofanya ujambazi sawa, ulifanya ukahaba sawa.
Neno kutoka kwa BWANA (RHEMA) halipo.
Sasa hivi mtu akiuza mafuta ya upako hata kahaba anamuuzia tu hakuna shida maana ni biashara kama biashara zingine.
Mafundisho yanayofundishwa makanisani sasa ni mepesi na ya kawaida. Mtu yeyote anayeweza kuongea anaweza kuhubiri bila wasiwasi.
Unaangalia tu nini kinatrendi kwasasa unalinganisha na maandiko ya kwenye Biblia unashangiliwa mchezo umeisha.
Wale wahubiri ambao hawasimami madhabahuni kuhubiri mpaka wasikie sauti ya Mungu ikiwaambia waseme nini sasa hawapo.
Ni mazoea tu. Mtu akikumbuka niliwahi kufundisha somo fulani nilipata credit basi atalibeba akafundishe mahali pengine.
Kanisa limegeuka mahali pa kuanzisha vikundi vya kusaidiana na vya kikabila.
Mungu aliponye kanisa.
Muhubiri anapitia YouTube mahubiri ya wahubiri wengine naye huyabeba kanisani kwake.
Iko wapi kazi ya Roho wa Mungu?
Watu wametengana kwa dhambi ya uzinzi mpaka sasa wameona hakuna namna uzinzi usiwe dhambi ya kutengana maana kanisa Zima limejaa uzinzi.
Kanisa ambalo halina NENO HAI (RHEMA) ni kichaka cha uzinzi, uchawi, majungu na kila aina ya dhambi.
Ukiona umeshaanza kuwaponda na kuwadharau wachungaji ujue kiburi tayari kimeshakuvaa!! Hata kama hayo uliyoandika ni kweli lakini hukupaswa kufanya hivyo!! Ulipaswa kuwaombea na kuongea nao kwa upendo!! Uko hatarini sana kama haujui!!
 
Kuna huyu anaitwa Tony Kapola ndiyo yupoyupo tu. Yaani hamna neno ila ujanjaujanja tu.
Kapola ukitaka kujifurahisha na kuwa motivated ndo anafaa umsikilize ila kama ni mambo ya kiroho na ukiristo wa matendo huyo wala hashughuliki nao yeye ni maisha ya mwili tu!
 
Kanisa limejengwa juu ya mitume na manabii

Kama tunataka kurudisha kanisa (mwili wa kisiri wa Yesu Kristo) kama vile lilivyotenda kazi katika kitabu cha Matendo ya Mitume Basi turudi kwenye basics zile zile walizokuwa nazo mitume kwa sababu yeye Mungu hana kigeugeu (Malaki 3) Yesu Kristo ni yeye yule Jana Leo na hata milele (Ebr 13:8)

Mungu akija Leo hatauhukumu ulimwengu kwa taratibu/mapokeo/kanuni za Imani za kikatoliki,kilutheri,kipentekoste, Methodist, Anglican, Baptist,Kisabato,mashahidi wa Yehova etc

Ulimwengu ukihukumiwa kwa mapokeo ya kilutheri basi Wote tumeangamia, ukihukumiwa kwa mapokeo na kanuni za Kisabato basi wengine wote tumekwisha.

Mungu atauhukumu ulimwengu kwa Neno lake (Mbingu na Nchi zitapita ila hilo Neno halitopita)

Turudi basi kwenye basics za Matendo ya Mitume (sio kwa mihemuko) namna walivyobatiza, namna walivyomhubiri Kristo.

Kwa sababu Mkuu wa wajenzi Paulo aliuweka msingi na akasema kwenye Wagalatia 1:8 (ikiwa malaika kutoka Mbinguni au mtu mwingine yeyote atawahubiri injili nyingine tofauti na hii niliyohubiri na alaaniwe)

Bible mwishoni imetoa onyo ukiongeza au ukipunguza jina lako linaondolewa kwenye kitabu cha uzima,na mapigo utapata.

Turudi kwenye basics za kanisa la kwanza la kibibilia sio tasfiri za watu walizojiwekea creeds (kanuni za imani) and Dogmas (mafundisho ya sharti)

Asanteni.
 
Ile misingi migumu sana ila ndio ukristo.
Kanisani kuna watu wana magari mpaka mengine yamepitwa na fashion kwao hawawezi tena kuyatumia wameyajaza tu uani, the same church binti anapita mbele kuombewa na hao mabwana na mabibi wenye mabilioni ili binti apate hitaji lake ambalo ni mtaji wa karanga na maji katoni 5 (sh. 50 elfu tu).
Hapa ndipo lilipoanza tatizo
 
Injili ya kale ya akina Petro ilikuwa rhema.

Rhema ni neno la Mungu kwa wakati husika. Yaani Mungu anasema kwa kinywa cha mtu. Anaweza kutumia neno hili la kila siku (logos) ila anaposema Mungu mwenyewe hulitia uzima na kutimiza kusudi lake kwa haraka kama umeme.

Ndio maana ukisoma kitabu cha Matendo ya mitume kimejaa matendo makuu mpaka kitabu kikaitwa "Matendo ya Mitume" na si mausia au maneno ya mitume.

Anania na Safira walipofanya udanganyifu, Petro alitamka neno "rhema" na ikawa vivyohivyo.

Sasa hivi, wewe hata ukipeleka sadaka pesa uliyofanya ujambazi, sawa, ulifanya ukahaba, sawa.

Neno kutoka kwa BWANA (rhema) halipo.

Sasa hivi, mtu akiuza mafuta ya upako, hata kahaba anamuuzia tu, hakuna shida, maana ni biashara kama biashara zingine.

Mafundisho yanayofundishwa makanisani sasa ni mepesi na ya kawaida. Mtu yeyote anayeweza kuongea anaweza kuhubiri bila wasiwasi.

Unaangalia tu nini kinatrendi kwa sasa, unalinganisha na maandiko ya kwenye Biblia, unashangiliwa, mchezo umeisha.

Wale wahubiri ambao hawasimami madhabahuni kuhubiri mpaka wasikie sauti ya Mungu ikiwaambia waseme nini, sasa hawapo.

Ni mazoea tu. Mtu akikumbuka niliwahi kufundisha somo fulani, nilipata credit, basi atalibeba akafundishe mahali pengine.

Kanisa limegeuka mahali pa kuanzisha vikundi vya kusaidiana na vya kikabila.

Mungu aliponye kanisa.

Muhubiri anapitia YouTube mahubiri ya wahubiri wengine, naye huyabeba kanisani kwake.

Iko wapi kazi ya Roho wa Mungu?

Watu wametengana kwa dhambi ya uzinzi, mpaka sasa wameona hakuna namna uzinzi usiwe dhambi ya kutengana, maana kanisa zima limejaa uzinzi.

Kanisa ambalo halina "NENO HAI" (rhema) ni kichaka cha uzinzi, uchawi, majungu, na kila aina ya dhambi.

Note: Watumishi wa Mungu wenye kujitoa kwa kila hali wapo, wanaotembea na Mungu kila leo wapo, ingawa ni wachache na si maarufu, wengi wao.
Hakika
 
Nishangaa jamaa ombaomba mbezi anamafuta ya upako. Kila baada ya muda anajipaka ili kuvuta wateja.

Injili ya sasa hivi, soma vitabu vya Kiyosaki, Brian trecy, Robert Green, Robin Shama, new age motivational speakers and get rich quickly books. Changanya na tuvitabu vtwa Oyadepo, Keneth, Jakes, Ben hinn, na vifungu vya biblia. Kama kanisa liko mjini, changanya na kakiingerezaSwahili.
Utakula pesa.

Naunga mkono thread. Mimi napenda pure Gospel. Hata nikiwa church ukianza maujinga ya kuongea vitu vya kidunia na kujipendekeza nafungua biblia nasoma sikusikilizi, na sifuati chochote utakachoamuru, ikiwemo kurudiarudia maneno au kufanya vitendo. Ila simchukii mtoa masimulizi hayo.
 
Kuna huyu anaitwa Tony Kapola ndiyo yupoyupo tu. Yaani hamna neno ila ujanjaujanja tu.
Anawaiga wakina Apostle Joshua Selman. Wanasoma vitabu vya motivesheni na kutafuta vifungu vya kuunganishia. Injili hizo wasikilizaji kuacha dhambi ni mziki.
 
Injili ya kale ya akina Petro ilikuwa rhema.

Rhema ni neno la Mungu kwa wakati husika. Yaani Mungu anasema kwa kinywa cha mtu. Anaweza kutumia neno hili la kila siku (logos) ila anaposema Mungu mwenyewe hulitia uzima na kutimiza kusudi lake kwa haraka kama umeme.

Ndio maana ukisoma kitabu cha Matendo ya mitume kimejaa matendo makuu mpaka kitabu kikaitwa "Matendo ya Mitume" na si mausia au maneno ya mitume.

Anania na Safira walipofanya udanganyifu, Petro alitamka neno "rhema" na ikawa vivyohivyo.

Sasa hivi, wewe hata ukipeleka sadaka pesa uliyofanya ujambazi, sawa, ulifanya ukahaba, sawa.

Neno kutoka kwa BWANA (rhema) halipo.

Sasa hivi, mtu akiuza mafuta ya upako, hata kahaba anamuuzia tu, hakuna shida, maana ni biashara kama biashara zingine.

Mafundisho yanayofundishwa makanisani sasa ni mepesi na ya kawaida. Mtu yeyote anayeweza kuongea anaweza kuhubiri bila wasiwasi.

Unaangalia tu nini kinatrendi kwa sasa, unalinganisha na maandiko ya kwenye Biblia, unashangiliwa, mchezo umeisha.

Wale wahubiri ambao hawasimami madhabahuni kuhubiri mpaka wasikie sauti ya Mungu ikiwaambia waseme nini, sasa hawapo.

Ni mazoea tu. Mtu akikumbuka niliwahi kufundisha somo fulani, nilipata credit, basi atalibeba akafundishe mahali pengine.

Kanisa limegeuka mahali pa kuanzisha vikundi vya kusaidiana na vya kikabila.

Mungu aliponye kanisa.

Muhubiri anapitia YouTube mahubiri ya wahubiri wengine, naye huyabeba kanisani kwake.

Iko wapi kazi ya Roho wa Mungu?

Watu wametengana kwa dhambi ya uzinzi, mpaka sasa wameona hakuna namna uzinzi usiwe dhambi ya kutengana, maana kanisa zima limejaa uzinzi.

Kanisa ambalo halina "NENO HAI" (rhema) ni kichaka cha uzinzi, uchawi, majungu, na kila aina ya dhambi.

Note: Watumishi wa Mungu wenye kujitoa kwa kila hali wapo, wanaotembea na Mungu kila leo wapo, ingawa ni wachache na si maarufu, wengi wao.
Bila Shaka wewe ni mtumishi pia ndiyo maana umeweza kuyaona haya, tena siyo tu mtumishi jina ila ni mtu uliyebahatika kuijua kweli kwa sehemu yako na unajua utakatifu ni nini. Mungu atusaidie wanadamu tumetingwa na changamoto za dunia
 
Nishangaa jamaa ombaomba mbezi anamafuta ya upako. Kila baada ya muda anajipaka ili kuvuta wateja.

Injili ya sasa hivi, soma vitabu vya Kiyosaki, Brian trecy, Robert Green, Robin Shama, new age motivational speakers and get rich quickly books. Changanya na tuvitabu vtwa Oyadepo, Keneth, Jakes, Ben hinn, na vifungu vya biblia. Kama kanisa liko mjini, changanya na kakiingerezaSwahili.
Utakula pesa.

Naunga mkono thread. Mimi napenda pure Gospel. Hata nikiwa church ukianza maujinga ya kuongea vitu vya kidunia na kujipendekeza nafungua biblia nasoma sikusikilizi, na sifuati chochote utakachoamuru, ikiwemo kurudiarudia maneno au kufanya vitendo. Ila simchukii mtoa masimulizi hayo.
Huo ndiyo ukomavu na ufahamu wa kiroho, siyo kuburuzwa tu kama kondoo wanaopotea wanaoenda kuchinjwa
 
laiti mngejua ni nini maana ya kanisa.

huko mnakosema ni makusanyiko tu ya watu hayajafikia level za kuitwa "kanisa". kanisa ni kitu kitakatifu!

Yesu ni Kristo
 
Back
Top Bottom