Watumishi wa Mungu wamekuwa wakame rohoni sasa makanisani wanafundisha falsafa za kidunia, Falsafa ambazo unaweza kuzipata popote

Akili za watu zimechoka sana aisee, yaani mtu anapaka mafuta ya upako ili apate mvuto kwa watoa msaada!!
 
GMO food zimefanikiwa kuua nguvu ya kiroho kwa watu wengi siku hizi,shetani kaingia kanisani.
Kuna mtu wangu yeye ni muislam lakini kila j.pili huenda kanisani kwa ajili ya kufanyq uvuvi! Eti kanisani ndo kuna mademu wakali!

Nakubaliana na wewe, shetani sio kaingia tu bali kakaribishwa kanisani kama mgeni wathamani sana!
 
Wakihubiri habari za wokovu na uzima wa milele mnawasema wachungaji wamepitwa na wakati na hata kanisani hamuendi, wakihubiri mambo mnayopenda kusikia mnasema wachungaji wamekengeuka kwani binadamu mnatakaje ninyi? mihemko na unafiki tu.
Kimsingi mtumishi wa Mungu hapaswi kwenda kwa kuangalia upepo, anapaswa kuongozwa na Roho wa Mungu, nje ya hapo hamna kitu inabakia kuwa ni falsafa tu
 
Ukiona umeshaanza kuwaponda na kuwadharau wachungaji ujue kiburi tayari kimeshakuvaa!! Hata kama hayo uliyoandika ni kweli lakini hukupaswa kufanya hivyo!! Ulipaswa kuwaombea na kuongea nao kwa upendo!! Uko hatarini sana kama haujui!!
Hapana yupo sahihi kwa sababu wapo wachungaji wanaopita humu na kukutana na yanayo wahusu, kuwaombea ni sawa lakini ni lazima pia wafikishiwe ujumbe, hii ipo kimaandiko kabisa. Huwezi kumuacha mtu aendelee na njia mbaya wakati unaweza kumuonya. Ila hawa wachungaji walioamua kuwa hivi ni watu walioamua wengi wao wanajua kama wanakosea. Kwa mfano uzinzi na uasherati, huwezi kusema hakuna mchungaji asiyejua hii ni dhambi
 
Nitakutumia sadaka pastor
 
Ni kweli kabisa hata suala la bandari lingepewa kipaumbele sana kwenye Kanisa lililo hai ila,ndo bas tena.
 
Yesu alifundisha Kwa Migano then akaleta katika maana ya Kimbingu. Mpanzi, Mwana mpotevu, walioalikwa Harusini
 
Kuna wengine waume kwa wake wanafundisha wanandoa kunyanduana. Mbona kunyanduana ni asili inayofuata mkondo wake haihitaji kufundishwa? Mbaya zaidi kuna watoto wanasikia. Mambo ya kunyanduana kuna semina za wamama na wababa/wanandoa wakafundishane huko kwa uhuru. Tena wamama peke yao na wababa peke yao wasioneane aibu.
 
Kuna mmoja anasema yeye hafundishi habari za mbinguni kwa kuwa hajawahi kufika huko. Anasema yaye atafundisha vitu halisi, duh! Siku hizi kuna watumishi wa Mungu wenye mafundisho ya ajabuajabu yasiyoendana na mukhtadha wa biblia
 
Hamna hata mmoja humo ni ujanjaujanja
Kama unawafahamu akina Moses Kulola, Mwamposa na Mwakasege... Hakika neno la Mungu limekufikiā na umetambua Yesu ni Bwana na Mwokozi wako...
Ungeniambia huwafahamu ningejua hawafanyi kazi ya Mungu
 
Mwamposa???. Wewe kweli mnafiki.
Kama unamfahamu MWAMPOSA... Hakika neno la Mungu limekufikiā na umetambua Yesu ni Bwana na Mwokozi wako...
Ungeniambia humfahamu ningejua hafanyi kazi ya Mungu
 
Mahubiri au wahubiri wengi kwa sasa hayana tofauti na maelezo ya mganga wa kienyeji, kuambiwa umeibiwa nyota, jirani yako sio mtu mzuri na mengine mengi ya kufarakanisha kwa sasa ndo yametalamaki.

Ni ngumu kwa sasa kukuta mhubiri akihubiri kuhusu
Watu waache dhambi, watu wamrudie Mungu na habari za wokovu kwa ujumla mahubiri yamejaa faraja za kijinga na baraka za uongo za utajiri cha ajabu wahubiri ndo wanazidi kuneemeka (kutajirika)

Kubwa kabisa waumini wengi hawasomi biblia wanasubiri mhubiri (prophet) ndie aisome awaeleze alichokielewa na madhehebu mengi hayaruhusu waumini kuhoji maswali pale ambapo hawaelewi.

La mwisho nnaloliona waumini wengi wamekuwa waoga kwa viongozi wao wa kiroho (kiongozi) amegeuzwa mungu mtu naogopwa kama vile ye sio mtu wa kawaida hakosei akitamka jambo kwa muumini basi muumini ye ni kutekeleza!
 
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…