Watumishi wa Mungu wamekuwa wakame rohoni sasa makanisani wanafundisha falsafa za kidunia, Falsafa ambazo unaweza kuzipata popote

Watumishi wa Mungu wamekuwa wakame rohoni sasa makanisani wanafundisha falsafa za kidunia, Falsafa ambazo unaweza kuzipata popote

Nishangaa jamaa ombaomba mbezi anamafuta ya upako. Kila baada ya muda anajipaka ili kuvuta wateja.

Injili ya sasa hivi, soma vitabu vya Kiyosaki, Brian trecy, Robert Green, Robin Shama, new age motivational speakers and get rich quickly books. Changanya na tuvitabu vtwa Oyadepo, Keneth, Jakes, Ben hinn, na vifungu vya biblia. Kama kanisa liko mjini, changanya na kakiingerezaSwahili.
Utakula pesa.

Naunga mkono thread. Mimi napenda pure Gospel. Hata nikiwa church ukianza maujinga ya kuongea vitu vya kidunia na kujipendekeza nafungua biblia nasoma sikusikilizi, na sifuati chochote utakachoamuru, ikiwemo kurudiarudia maneno au kufanya vitendo. Ila simchukii mtoa masimulizi hayo.
Akili za watu zimechoka sana aisee, yaani mtu anapaka mafuta ya upako ili apate mvuto kwa watoa msaada!!
 
GMO food zimefanikiwa kuua nguvu ya kiroho kwa watu wengi siku hizi,shetani kaingia kanisani.
Kuna mtu wangu yeye ni muislam lakini kila j.pili huenda kanisani kwa ajili ya kufanyq uvuvi! Eti kanisani ndo kuna mademu wakali!

Nakubaliana na wewe, shetani sio kaingia tu bali kakaribishwa kanisani kama mgeni wathamani sana!
 
Wakihubiri habari za wokovu na uzima wa milele mnawasema wachungaji wamepitwa na wakati na hata kanisani hamuendi, wakihubiri mambo mnayopenda kusikia mnasema wachungaji wamekengeuka kwani binadamu mnatakaje ninyi? mihemko na unafiki tu.
Kimsingi mtumishi wa Mungu hapaswi kwenda kwa kuangalia upepo, anapaswa kuongozwa na Roho wa Mungu, nje ya hapo hamna kitu inabakia kuwa ni falsafa tu
 
Ukiona umeshaanza kuwaponda na kuwadharau wachungaji ujue kiburi tayari kimeshakuvaa!! Hata kama hayo uliyoandika ni kweli lakini hukupaswa kufanya hivyo!! Ulipaswa kuwaombea na kuongea nao kwa upendo!! Uko hatarini sana kama haujui!!
Hapana yupo sahihi kwa sababu wapo wachungaji wanaopita humu na kukutana na yanayo wahusu, kuwaombea ni sawa lakini ni lazima pia wafikishiwe ujumbe, hii ipo kimaandiko kabisa. Huwezi kumuacha mtu aendelee na njia mbaya wakati unaweza kumuonya. Ila hawa wachungaji walioamua kuwa hivi ni watu walioamua wengi wao wanajua kama wanakosea. Kwa mfano uzinzi na uasherati, huwezi kusema hakuna mchungaji asiyejua hii ni dhambi
 
Kanisa la sasa limejaa motivational speakers na social commentators dizaini ya akina Tonny Kapola na Daniel Mugogo; na mrundikano wa manabii na mitume wenye tamaa ya pesa. Ugalatia unapitia kipindi kigumu sana!

[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]

MWENYE SIKIO LA KUSIKIA ALIYE KANISANI ASIKIE LEO

Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.

Karibu nikujuze ufunuo huu nilioambiwa kwa ajili ya watu wa Kanisa.

■Nianze kwa kusema hivi Usipobadilika utaende jehanamu huku unaimba pambio, wewe mwimbaji ila mwasherati na mzinzi.

■Usipobadilika utaenda jehanamu na sauti yako yenye upako, wewe mhubiri ila mzinzi na mwasherati.

■Usipobadilika utaenda jehanamu huku nyimbo zako mwenyewe zikikusindikiza, kwa sababu tu wewe ni mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili ila mwasherati na mzinzi.

1 Wakorintho 6:9 " Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa MUNGU, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,"

■Uaskofu huku unaendelea na uzinzi wewe ni wa jehanamu, hata kama unaheshimika vipi hapa duniani.

■Uchungaji wa viwango lakini ni mzinzi, wewe ni wa jehanamu na sio mbinguni.

■Kuitwa Mtume au Nabii au Mwinjilisti au Mwalimu lakini huku wewe ukiendelea na uzinzi na uasherati wewe hakika ni wa jehanamu.

■Ukiwa mtoaji safi, mshirika sana na bado wewe ni mzinzi na mwasherati tambua kwamba YESU anasema

Mathayo 7:21-23 "Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu."

●Ndugu Mtumishi si unaendelea na uzinzi au usherati?

Ni rahisi sana kwamba YESU KRISTO atakuambia siku ukifa kwamba "Sikukujua wewe kamwe; ondoka kwangu, wewe mtendao maovu"

●Wewe uliyetumwa na shetani ili utembee na watu wa Kanisa wenzako ili wewe na wao mkose uzima wa milele.

●Wewe Mchungaji wa kondoo ambaye badala ya kuchunga kondoo wewe unatafuna kondoo mmoja mmoja wasio na akili.

■Usipobadilika utaenda jehanamu hata kama kwa sasa unaitwa mzee wa Kanisa au shemasi au kiongozi wa vijana au kiongozi wa wamama au Mwalimu wa kwaya au mwanakwaya au Mwalimu wa watoto.

■Usipotubu na kuacha uchafu wako ujue siku ile YESU Mwokozi atakuambia kwamba hakukujua kamwe.

●Wewe Mchungaji unayetangaza Kanisani kwamba unaenda mbali kufanya huduma kumbe unaenda kwa hawara yako.

●Enyi wanakwaya ambao mmegeuzana chakula kila mwanakwaya.

MUNGU amenituma nisema na inawezekana hii ndio nafasi yako ya mwisho umepewa.

Kuna makanisa ni zaidi ya danguro.

Kuna makanisa ni zaidi ya chuo cha kujifunza ukahaba.

Kuna makanisa uzinzi na uasherati uko kiwango sawa na kwa wapagani.

1 Wakorintho 5:1 " Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye."

●Kuna wamama wachungaji ni wazinzi na huwasaidia mabinti wa Kanisa kutoa mimba.

Kuna mabinti walishawahi kutoa hadi mimba za watumishi.

Ndugu, ni wakati wa kujikana na kujipambanua hata kama wanakwaya wenzako wote wameoza kwa uasherati na uzinzi.

Wewe usifanye dhambi hizo.

Ni wakati wa kujipambanua hata kama wabinti wenzako Kanisani ni waasherati.

Ndugu, kumbuka Neno la MUNGU linasema Wagalatia 6:5 " Maana kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe."

Wengine watabeba mafurushi yao kwenda jehanamu na sio mbinguni.

Wewe mtoto wa Mchungaji wala hutaenda mbinguni kwa sababu baba yako au babu yako ni Mchungaji au Askofu.

Ndugu, umepewa nafasi ya kutubu wewe binafsi, ukiichezea nafasi yako ujue watu wa aina yako wataenda jehanamu.

Kuna watu wako Kanisani hata miaka zaidi ya 10 lakini watu hao hawajawahi kuwa kondoo bali wao ni mbuzi tu siku zote, ndugu kuna jehanamu ya moto kwa waovu.

Nilipewa maandiko manne kwa ufunuo huu ili mwenye sikio la kusikia asikie Leo na kuacha dhambi zote hasa uzinzi na uasherati.

Neno la MUNGU mwenyezi linasema

Ufunuo 2:11 "Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo ROHO ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili."

Ufunuo 2:29 "Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo ROHO ayaambia makanisa."

Ufunuo 3:22 "Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo ROHO ayaambia makanisa."

Ufunuo 3:6 "Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo ROHO ayaambia makanisa."

Mimi nimekuambia Leo.

■Yule aliye na sikio la kusikia asikie Leo na kuacha uzinzi na uasherati.

●Kuna watu wengi sana wakiwa jehanamu wataaanza kuwalalamikia wachungaji wao kwamba kwanini hawakuwaonya wala kuwakemea, watawalaumu wachungaji wao kwa nini walihubiri mafanikio tu na sio toba.

Ndugu uliye wa Kanisa Mimi najua ni neema ya MUNGU mwenyewe ili ujifunze ujumbe huu kisha uache uzinzi na uasherati.

Mimi Peter Mabula ninamshukuru Bwana YESU maana alichoniambia kusema nimesema.

"Asante Eee Mwokozi wangu YESU KRISTO.

Mwenye sikio la kusikia atatubu na kuacha uzinzi na uasherati kuanzia Leo."

Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kuelewa ameelewa.

MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu.

Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?

Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu. Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.

Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.

Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.

By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292 (Sadaka na WhatsApp)
Ubarikiwe
Nitakutumia sadaka pastor
 
Ni kweli kabisa hata suala la bandari lingepewa kipaumbele sana kwenye Kanisa lililo hai ila,ndo bas tena.
 
Injili ya kale ya akina Petro ilikuwa rhema.

Rhema ni neno la Mungu kwa wakati husika. Yaani Mungu anasema kwa kinywa cha mtu. Anaweza kutumia neno hili la kila siku (logos) ila anaposema Mungu mwenyewe hulitia uzima na kutimiza kusudi lake kwa haraka kama umeme.

Ndio maana ukisoma kitabu cha Matendo ya mitume kimejaa matendo makuu mpaka kitabu kikaitwa "Matendo ya Mitume" na si mausia au maneno ya mitume.

Anania na Safira walipofanya udanganyifu, Petro alitamka neno "rhema" na ikawa vivyohivyo.

Sasa hivi, wewe hata ukipeleka sadaka pesa uliyofanya ujambazi, sawa, ulifanya ukahaba, sawa.

Neno kutoka kwa BWANA (rhema) halipo.

Sasa hivi, mtu akiuza mafuta ya upako, hata kahaba anamuuzia tu, hakuna shida, maana ni biashara kama biashara zingine.

Mafundisho yanayofundishwa makanisani sasa ni mepesi na ya kawaida. Mtu yeyote anayeweza kuongea anaweza kuhubiri bila wasiwasi.

Unaangalia tu nini kinatrendi kwa sasa, unalinganisha na maandiko ya kwenye Biblia, unashangiliwa, mchezo umeisha.

Wale wahubiri ambao hawasimami madhabahuni kuhubiri mpaka wasikie sauti ya Mungu ikiwaambia waseme nini, sasa hawapo.

Ni mazoea tu. Mtu akikumbuka niliwahi kufundisha somo fulani, nilipata credit, basi atalibeba akafundishe mahali pengine.

Kanisa limegeuka mahali pa kuanzisha vikundi vya kusaidiana na vya kikabila.

Mungu aliponye kanisa.

Muhubiri anapitia YouTube mahubiri ya wahubiri wengine, naye huyabeba kanisani kwake.

Iko wapi kazi ya Roho wa Mungu?

Watu wametengana kwa dhambi ya uzinzi, mpaka sasa wameona hakuna namna uzinzi usiwe dhambi ya kutengana, maana kanisa zima limejaa uzinzi.

Kanisa ambalo halina "NENO HAI" (rhema) ni kichaka cha uzinzi, uchawi, majungu, na kila aina ya dhambi.

Note: Watumishi wa Mungu wenye kujitoa kwa kila hali wapo, wanaotembea na Mungu kila leo wapo, ingawa ni wachache na si maarufu, wengi wao.
Yesu alifundisha Kwa Migano then akaleta katika maana ya Kimbingu. Mpanzi, Mwana mpotevu, walioalikwa Harusini
 
Kuna wengine waume kwa wake wanafundisha wanandoa kunyanduana. Mbona kunyanduana ni asili inayofuata mkondo wake haihitaji kufundishwa? Mbaya zaidi kuna watoto wanasikia. Mambo ya kunyanduana kuna semina za wamama na wababa/wanandoa wakafundishane huko kwa uhuru. Tena wamama peke yao na wababa peke yao wasioneane aibu.
 
Kuna mmoja anasema yeye hafundishi habari za mbinguni kwa kuwa hajawahi kufika huko. Anasema yaye atafundisha vitu halisi, duh! Siku hizi kuna watumishi wa Mungu wenye mafundisho ya ajabuajabu yasiyoendana na mukhtadha wa biblia
 
Hamna hata mmoja humo ni ujanjaujanja
Kama unawafahamu akina Moses Kulola, Mwamposa na Mwakasege... Hakika neno la Mungu limekufikiā na umetambua Yesu ni Bwana na Mwokozi wako...
Ungeniambia huwafahamu ningejua hawafanyi kazi ya Mungu
 
Mwamposa???. Wewe kweli mnafiki.
Kama unamfahamu MWAMPOSA... Hakika neno la Mungu limekufikiā na umetambua Yesu ni Bwana na Mwokozi wako...
Ungeniambia humfahamu ningejua hafanyi kazi ya Mungu
 
Mahubiri au wahubiri wengi kwa sasa hayana tofauti na maelezo ya mganga wa kienyeji, kuambiwa umeibiwa nyota, jirani yako sio mtu mzuri na mengine mengi ya kufarakanisha kwa sasa ndo yametalamaki.

Ni ngumu kwa sasa kukuta mhubiri akihubiri kuhusu
Watu waache dhambi, watu wamrudie Mungu na habari za wokovu kwa ujumla mahubiri yamejaa faraja za kijinga na baraka za uongo za utajiri cha ajabu wahubiri ndo wanazidi kuneemeka (kutajirika)

Kubwa kabisa waumini wengi hawasomi biblia wanasubiri mhubiri (prophet) ndie aisome awaeleze alichokielewa na madhehebu mengi hayaruhusu waumini kuhoji maswali pale ambapo hawaelewi.

La mwisho nnaloliona waumini wengi wamekuwa waoga kwa viongozi wao wa kiroho (kiongozi) amegeuzwa mungu mtu naogopwa kama vile ye sio mtu wa kawaida hakosei akitamka jambo kwa muumini basi muumini ye ni kutekeleza!
 
Mahubiri au wahubiri wengi kwa sasa hayana tofauti na maelezo ya mganga wa kienyeji, kuambiwa umeibiwa nyota, jirani yako sio mtu mzuri na mengine mengi ya kufarakanisha kwa sasa ndo yametalamaki.

Ni ngumu kwa sasa kukuta mhubiri akihubiri kuhusu
Watu waache dhambi, watu wamrudie Mungu na habari za wokovu kwa ujumla mahubiri yamejaa faraja za kijinga na baraka za uongo za utajiri cha ajabu wahubiri ndo wanazidi kuneemeka (kutajirika)

Kubwa kabisa waumini wengi hawasomi biblia wanasubiri mhubiri (prophet) ndie aisome awaeleze alichokielewa na madhehebu mengi hayaruhusu waumini kuhoji maswali pale ambapo hawaelewi.

La mwisho nnaloliona waumini wengi wamekuwa waoga kwa viongozi wao wa kiroho (kiongozi) amegeuzwa mungu mtu naogopwa kama vile ye sio mtu wa kawaida hakosei akitamka jambo kwa muumini basi muumini ye ni kutekeleza!
 
Back
Top Bottom