Watumishi wa serikali mliwezaje kutoboa, mbona mimi naenda kushindwa

Hongera sana mkuu
 
Msamehe bure
 
Tuko watoto watatu watumishi so tulkubaliana tuwe tunawatumia wazazi Hela wawe wananunua chakula.

Wazazi ni wazima na hawana changamoto yoyote
Kwahiyo mnawapa laki 3 Kwa mwezi
Sasa kaeni nyie watatu ongeeni muulíze mzee anaweza kufanya nn Cha mtaji mdogo Mpe idea hata genge na matunda hapo hapo nyumbni Kisha mpeni mtaji then tulieni muangalie mwambieni halinhalis ya maisha muwe mnamsapot pocket money za kawaida km mzazi Kwa muda huu mkiwa matajiri mtaendelea na utaratibu wenu km mzazi muelewa ataelewa
 
Hongera sana mkuu
Asante Mimi bi Mkubwa nampanga na anapangika na anajua navohangaika kutafuta Hela Nampa akili Hela atafute mwenyew😀

Kias imenisaidia na nikimpa Nampa na njia afanyaje asianguke sabbu mtu mzima hawez survive kibiashara km vijana
yani sahizi yeye ndo ananiletea vitenge nivae mara nakutumia vocha vip huko ngoja nikusave naenjoy mm tu no stress
 
Hizo ndio baraka za wazazi na utazidi kufanikiwa mpaka ushangae.
 
Lakin 6 ni ndogo mtu ukiwa na familia. Yaani mm nachukua hiyo hiyo lakini maisha yanakimbiza mpaka sasa sina hata saving shilingi 10.
Utamlaumu tu wife anamatumizi mabaya ila hiyo pesa ni ndogo. Kikubwa tafuta njia mbadala ya kuongeza kipato
Ni ngumu kushindwa kumaintain kidogo ukatarajia kikubwa ndio kikuendeshee maisha muhimu weka tu vipaumbele ni ngumu lakin unaweza kujaribu hata 50 Kwa mwez matumizi yasiyo ya lazima unaepuka tumia exprience hata za wanaoish Kwa mishahara ya laki 3 wanasurvivr vipi hata Kwa muda Ili upate mtaji uanze njia mpya
 
Mboga gani hiyo unayokula ya sh 5,000 kwa siku? Hapo ndipo unapokosea. Ukinunua mchele nunua na maharage na dagaa. Kwa kuwa upo mkoani mboga za majani fungu la sh 500 linatosha kula mara mbili mchana na usiku. Hapo kwenu unapeleka 100,000 na ukweni kwako unapeleka 100,000 kupitia mkeo bila wewe kujua.
 
Naona umeandika sehemu upo kada ya Afya.
Fanya yafuatayo
Fungua duka la dawa muhimu na hii ni kwa sababu duka hilo faida yake ni kubwa huwa sawa na mtaji.




Pia kwa kijijini hata laki tano unaweza kufungua baada ya kuwa umekwisha andaa fremu.

Mtengenezee mazingira mkewe apate short courses ya uuzaji wa madawa,hapo hizo stress za kujitakia zitaisha na utaanza kuwazia tofari ni bei gani.




Mtengenezee mzazi shughuli itayomuingizia pesa halafu jukumu lako wewe muwezeshe mtaji




Usichukue mkopo wa kwanza ukaenda kuwekeza kwenye vitu ambavyo sio vya kukuingizia pesa kama kujenga nyumba ya kuishi, mkopo huo utakutesa.

Wekeza sana kwenye biashara, acha kuishi maisha ya wengine jaribu kuishi maisha ya uhalisia wako kwa kupunguza gharama zisizo na ulazima kama kodi ya nyumba na pesa ya matumizi ya nyumbani.
 
Acha kazi endesha boda boda kwa siku utapiga 70000 kwa mwezi 2100000 milion
 
Pesa unayo muachia nyumbani mkeo ni kubwa kwa kipato chako duni punguza. Anza kumpa 60% ya hiyo mwambie kazini kuna shida imejitokeza unakatwa mshahara kiasi fulani.
Unapotafuta mtaji au uweze kutunza akiba zingatia yafuatayo:-
  1. Siyo lazima kila siku kula wali.
  2. Siyo lazima kula kitoweo kizuri kila siku.
  3. Usipange nyumba nzima kama familia yako ndogo.
  4. Panga sehemu yenye gharama ndogo ili mradi iwe na usalama. Hama hapo unapoishi sasa.
  5. Ukiweza lima bustani ya mboga mboga hata kwenye makopo.
  6. Zingatia matumizi ya gesi na mkaa visitumike ovyo. Tumia mtungi mdogo wa gesi na usinunue mara mbili ndani ya mwezi mmoja kwa familia ya mke na mtoto mmoja kama unanunua na mkaa. Usipike vitu vigumu kwenye gesi mfano maharagwe.
  7. Mkeo asijifanye ana roho nzuri na kugawa vitu kwa jirani.
  8. Mkeo aweke kibubu (pig bank) cha familia siyo Cha fedha ya kutuma kwao au kujenga kwao.
  9. Wewe na mkeo msishindane na mtu kwenye mavazi, manukato na urembo.
  10. Punguzeni matumizi ya gharama za simu au internet bundles.
  11. Zingatieni matumizi mazuri ya umeme na maji ya kulipia. Vitu vikishika baridi Zima jokofu(refrigerator), asikeshe anaangalia TV, usitumie jiko la umeme kwa sasa au tumia la umeme usitumie mkaa wala gesi.
  12. Mtoto mdogo asishinde amevalishwa diapers (Pampers) kutwa nzima ni gharama na mbaya kwa afya.
  13. Usitumie sigara
  14. Usinywe pombe au ukishindwa kujizuia kunywa mara chache kwa mwezi. Pia usijigeuze tajiri kununulia wengine Pombe.
  15. Usipeleke pesa nyingi kanisani au msikitini.
  16. Usicheze kamari au michezo ya kubahatisha Kamwe.
Don't spend above your average means.
--------------------------
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…