Wako mjini sema watoto tulkubaliana tuwe tunatumia laki Moja kila mwezi japo Mimi nilioona Bora nifanye ushauri kama wako wa biashara na hapo yenyewe natumaga 50K Tena wanalalamika haiwatoshi
Ninyi ni waninga sana yaani mnakubaliana tuu kuwa mtakuwa mnatuma laki nyumbani bila sababu!? Vipato vyenu Vinafana, tuma endapo kuna dharura au ugonjwa tuu mwisho sio kila mwezi. Gombana na hao ndugu zako ndipo utaendelea. Watu ni wakongwe kazini lakini hatuna huo utaratibu wa kutuma kila mwezi bali ni penye uhitaji, dharura na wakati ambao mwenyewe nafsi yangu imeamua tuu niwakumbuke wazazi.
Kipato changu siwezi kukubaliana na mtu yeyote zaidi ya mke namna ya kutumia.
Nunua friji, weka nyama kwenye friji, chemsha maharage ya kutosha wela kwenye friji, nyanya unaweza kuziweka pia kwenye friji tena ukazigandisha, mimi kwangu nyanya zinakaa zaidi ya mwezi, kila kitu unaweza kukifanyia package ukaweka kwenye friji.
Ukinunua nyama wapime kwenye ujazo wa nusu kilo ili utumie ile inayohitajika tuu.
Ukiweza ichemshe yote gawa kwenye vi kontena weka kwenye friji.
Wekeni ratiba ya chakula na mboga na muifuate hakuna kuishi maisha ya kiswahili swahili na ya kishamba yasiyo na mpangilio.
Kisha weka malengo ya wazi ukimshirikisha mkeo kuwa, mwezi huu laki moja tutanunua vyombo, mwezi unao kiti, mwezi ujao nguo, mwezi ujao tutaanza kulipia kidogokidogo tv mwezi next and next mtakuta ndani ya mwaka mmoja mmepiga hatua.
Mimi leo naweza kuisaidia familia na wategemezi kwenye masuala muhimu tuu kwa sababu nilikataa kata kata kuishi maisha ya kimaskini ya eti kuchangia sijui sh ngapi kila mwezi no no no. Hata misaada ya kijinga jinga kutoka kwa ndugu acha kabisa huo ujinga mtabaki wote maskini.
Jitafute wewe kwanza na mkeo, jengeni familia yenu kwanza baadaye automatically mtakuwa na uwezo wa kusaidia wengine tena sio kwa laki bali kwa milioni. Otherwise utaishia jela nakuambia wewe mtumishi wa umma.