Dr. Mahiga alikaimu Ukurugenzi wa Idara ya Usalama (enzi hizo kitengo cha Ikulu, kabla TISS haijaanzishwa rasmi kisheria).
Na alikuwa ni sehemu ya timu iliyopangua jaribio la kumpindua Nyerere miaka ya mwanzo ya 1980s.
Ukisoma kesi ya uhaini iliyotokana na jaribio hilo la Mapinduzi, Dr. Mahiga alikuwa shahidi aliyepewa jina la "Mr. X".
Baada ya hapo alipelekwa nje sana, Canada, Uswizi, Liberia, India, Italy, akifanyia kazi mashirika ya UN kama UNHCR na serikali ya Tanzania, kabla ya kupewa ubalozi kamili na rais Mkapa na kutumikia kama Muwakilishi wa Tanzania katika UBalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa, New York City, kuanzia mwaka 2003, kisha akarudi kufanya kazi Umoja wa Mataifa kama Muwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa Somalia, kisha akaja kugombea urais Tanzania, na baadaye akateuliwa na Magufuli kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, kisha Waziri wa Sheria, mpaka mauti yalipomkuta.
Alivyokuwa Usalama, tukiwa wadogo, tulikuwa tunajua Mzee Mahiga anafanya kazi muhimu Ikulu, lakini hatukuwahi kujua kama alikuwa bosi wa Usalama wa Taifa.
Alijiweka kuwa kama mtu wa kawaida sana.
Mpaka alivyokuja kuw balozi alikuwa anajichanganya sana na Watanzania kwa unyenyekevu mzuri tu kama mtumishi wa serikali.