Watumishi wa TRA Waliochaji Rushwa ya Tsh 30 Billion, Kisha Kumfungulia Huyu Mama Kesi ya Uhujumu Uchumi, Washughulikiwe

Watumishi wa TRA Waliochaji Rushwa ya Tsh 30 Billion, Kisha Kumfungulia Huyu Mama Kesi ya Uhujumu Uchumi, Washughulikiwe

Wawekezaji kama hawa wangepewa ushirikiano vizuri, tutaweza kufanana kama Dubai.
Kitakachobadilisha hii hali, ni kuwepo na sera nzuri (hasa ya kikodi) na sheria ya kumlinda muwekezaji kwa angalau miaka 100. Ndani ya muda mfupi, viwanda vitazidi idadi ya watu; na serikali itapata mapato ya kutosha, kwa sababu bidhaa nyingi zitakuwa zinapelekwa nje.​
Kwa utaratibu huu wa kumbakia kodi ni ngumu kuzalisha mabilionea wazawa, ile sera ya uzawa ya kina marehemu Idd Simba iliishia wapi? nafikiri ilikuwa inalenga mambo kama haya.
 
Bilioni kumi wanaichukuliaje yani
Na container 20 unazichukuliaje yani ?

Hakuna mali inayojaza container 20 yenye thamani ya bilioni 20 za kodi ?

Mfanyabiashara mwenyewe kasema alipotajiwa hiyo kodi akasema hana hela, hakusema kodi imekosewa, kasema sikuwa na hela. What does that mean? Anajua kilichomo. Na si ajabu kodi hiyo ni cummulative assesment ya biashara ya miaka 10 bila kulipa kodi. Hii ni hadithi ya majukwaani ya upande mmoja. Huwezi kufanya conclusion yeyote kwa kihadithi cha dakika mbili cha upande mmoja.
 
Sidhani kama walitaka pesa per ser, japo angetoa pesa wangechukua, mimi nadhani kuna competitor alitaka amtoe Mama Bonge kwenye reli kwa kuwatumia maafisa TRA. Haiingii akilini 30B kodi anatengeneza nuclear kwani?
Sahihi kabisa...

Au kuna uwezekana yupo mwenzake walipakia wote kontena zenye bidhaa za kufanana....

Sasa ili sokoni uuzike kwa haraka, Ikabidi afanye dili na hao vijana wa TRA.. Wamzungungushe kwanza Mama Bonge kama hivyo... Wakija kumalizana naye mzigo wake Umeisha Mama Bonge ndiyo aanze kuuza wake sasa...
 
Kwa utaratibu huu wa kumbakia kodi ni ngumu kuzalisha mabilionea wazawa, ile sera ya uzawa ya kina marehemu Idd Simba iliishia wapi? nafikiri ilikuwa inalenga mambo kama haya.
Tatizo tulilonalo sisi waafrika, ni kumdidimiza mzawa mwenzetu aliyeona fursa ya uwekezaji kwa kuweka mazingira ya kumkwamisha, kuanzia kwenye vibali mpaka kodi; ndio maana matatizo mengi ya Afrika yana fanana fanana.​
 
Kwa hao viumbe wanaokufa baada ya kuchakata mbona wamezaliana sana zaidi hata ya binadamu, akichakata anazalisha kama elfu moja, akifa mmoja siyo mbaya.
Lakini hao viumbe mara moja anazalisha hata mia hivi tofauti na binadamu inakuwa mtoto mmoja
 
Usitoe hukumu kwa usicho kijua fatilia vizuri ujue huyo mama je ni kweli anaingiza contener hizo kumi je kampuni yake inaitwaje hutakiwi kusikiliza upande mmoja huenda state imempanga kutangeneza headlines kuficha mengi mabaya.
 
Sahihi kabisa...

Au kuna uwezekana yupo mwenzake walipakia wote kontena zenye bidhaa za kufanana....

Sasa ili sokoni uuzike kwa haraka, Ikabidi afanye dili na hao vijana wa TRA.. Wamzungungushe kwanza Mama Bonge kama hivyo... Wakija kumalizana naye mzigo wake Umeisha Mama Bonge ndiyo aanze kuuza wake sasa...
It is a very good observation sweet sis. And well said.
 
Lakini hao viumbe mara moja anazalisha hata mia hivi tofauti na binadamu inakuwa mtoto mmoja
Hapo ndo penye shida, hii inachangiwa na nyie kutoa moja pekee wakati mwanaume anatoa zaidi ya milioni.......jitahidini hata mfike mayai kumi.
 
Wanastahili adhabu ila wasinyongwe, ukianza kunyonga basi utanyonga waishe maana wasafi wanaweza kuwa wachache sana. Ukumbuke kuna Polisi, Halmashauri, wizarani na hata sekta binafsi. Kote huko kuna watu wa aina hii. Hapo hujagusa wanasiasa.

Wapunguziwe majaribu, mfumo wa kodi uwe digital kupunguza uhusiano wa moja kwa moja wa mlipa kodi na afisa. Tuwekeze kwenye technology.

Mfano magari zamani makadirio walikuwa wanapiga sana, sasa hivi hilo jaribu wameepushwa nalo.

Tusiwekeze kwenye uzalendo kwa mtindo wa kuacha mianya ya mtu kushawishiwa au kushawishi kupata kitu.
Huko huko kwenye digital, si ndo kuna mfumo sasa hivi? Watakuwekea viwango vya juu ili ushindwe, mwisho wake utawafuata tu muyamalize, utaambiwa lipa mil 200, mia tunakula sisi, 100 nyengine inaandikiwa receipt
 
Ngoja mkomeshwe mataahira nyie!

Hivi mlifikiri Magufuli anafanya vile kwa faida zake?

Alikuwa anajaribu kuwatetea nyie mbugilambugila ila makaishia kumtukana,,

Na bado, mbona mtaimba tu haleluya
Bora waingie wezi milioni Moja.Ubaya wao haufikii hata robo ya mabaya ya magufuli.Madhaifu yapo Kwa Kila nchi.Wape watu nafsi wayaanike ili ujue namna ya kuyashughulikua.Lkn yule mungu wako magu aliwafunfa watu midomo.Sasa utajuaje madudu ya TRA?Muulize Mo kilichomfanya atekwe
 
Na container 20 unazichukuliaje yani ?

Hakuna mali inayoweza kuwekwa kwenye container 20 yenye thamani ya bilioni 20 za kodi ?
Mama mwenyewe kasema alipotajiwa hiyo kodi akasema hana hela, hakusema kodi imekosewa, kasema sikuwa na hela. What does that mean? Anajua kilichomo. Na si ajabu kodi hiyo ni cummulative assesment ya biashara ya miaka 10 bila kulipa kodi. Hii ni hadithi ya majukwaani ya upande mmoja. Huwezi kufanya conclusion yeyote kwa kihadithi cha dakika mbili cha upande mmoja.
Rais Samia alikwisha piga marufuku kudai hizo kodi accumulated zaidi ya miaka 2
 
Huyu Mama ni mmoja kati ya walioongea jana mbele ya PM. Alidaiwa kodi ya Tsh 30 Billion kwa containers zake 10 alizo import. Baada ya kuonyesha kuwa hana hizo fedha akatengenezewa mashtaka ya uhujumu uchumi. Waliosokia kikao cha PM wakamfutia shtaka la uhujumu uchumi. Na kisha usiku wa kuamkia mkutano wa PM wakamuita akatoe mzigo.

Hivi ni vitendo vinavyorudisha nyuma maendeleo ya wafanyabiashara na nchi kwa ujumla. Nashauri vyombo vya dola vishughulike na Meneja TRA wa Mkoa wa Ilala pale Kipata na wengine wote waliohusika
View attachment 2626036
===Eti walianza na leta billion 30!

===Baadaye wakashuka hadi billion 15!

===Baadaye wakashuka hadi 10!

===Walipoona mama wa watu amekomaa kuikataa, wakamfungulia kesi ya uhujumu uchumi!

===Mwisho wakanyoosha maneno wenyewe kwa kumwitia mizigo yake bila kulipa chochote!!!!

Lakini swali kubwa la kujiuliza ni hili👇👇👇

Kwamba, hivi huyu mama anaweza kuwa na biashara kubwa kiasi gani ya kutoa rushwa ya TZS 30bn au 15bn au 10bn na bado akaendelea ku - survive katika game ya biashara?

===Hata kama ni Bakhresa umwambie atoe Kwa mkupuo mmoja TZS 30bn, lazima atafunga biashara zake tu..!!

Hawa watumishi wasakwe na wafunguliwe kesi ya uhujumu uchumi.!!

ADUI WA MAENDELEO YA NCHI YETU TANZANIA NI WAFANYAKAZI WA TRA na WIZARA YA FEDHA!!
 
Huyu Mama ni mmoja kati ya walioongea jana mbele ya PM. Alidaiwa kodi ya Tsh 30 Billion kwa containers zake 10 alizo import. Baada ya kuonyesha kuwa hana hizo fedha akatengenezewa mashtaka ya uhujumu uchumi. Waliosokia kikao cha PM wakamfutia shtaka la uhujumu uchumi. Na kisha usiku wa kuamkia mkutano wa PM wakamuita akatoe mzigo.

Hivi ni vitendo vinavyorudisha nyuma maendeleo ya wafanyabiashara na nchi kwa ujumla. Nashauri vyombo vya dola vishughulike na Meneja TRA wa Mkoa wa Ilala pale Kipata na wengine wote waliohusika
View attachment 2626036

TRA kuna baadhi ya watumishi wanaonra sana wivu wafanyabiashara.
TRA kuna wengine imekuwa kichaka cha wababaishaji na watu wanaodhulumu wengine kwa kujidai wanatimiza sheria.
Wengi ni wala rushwa wakubwa. Na cha kushangaza, they always seem to get away with it.

Haya bwana......
 
Huyu Mama ni mmoja kati ya walioongea jana mbele ya PM. Alidaiwa kodi ya Tsh 30 Billion kwa containers zake 10 alizo import. Baada ya kuonyesha kuwa hana hizo fedha akatengenezewa mashtaka ya uhujumu uchumi. Waliosokia kikao cha PM wakamfutia shtaka la uhujumu uchumi. Na kisha usiku wa kuamkia mkutano wa PM wakamuita akatoe mzigo.

Hivi ni vitendo vinavyorudisha nyuma maendeleo ya wafanyabiashara na nchi kwa ujumla. Nashauri vyombo vya dola vishughulike na Meneja TRA wa Mkoa wa Ilala pale Kipata na wengine wote waliohusika
View attachment 2626036
Kama mtu hafanyi biashara hawezi elewa haya.
 
asilimia kubwa wafanyakazi TRA wanaishi maisha ya juu kuliko hata mtu anayefanyabishara
Kuanzia majumba,magari,matumizi nk
Na fedha yao nyingi ni ya dhuluma

Ova
 
Mh Rais na viongozi wote kwa ujumla embu tungeni adhabu ya kuwanyonga maofisia wanao fanya mambo yakinyama kama haya kweli huyu mwanamke amefanyiwa haya yote kwa fitina hao walio mtengenezea fitina wanajulikana why kukaa kimya?
TRA huko wanalindana mauchafu yao

Ova
 
Watawanywe wote mikoani,waje wengine wapya.
Kibongo bongo utasikua huyu hagusiki.
 
Back
Top Bottom