Watumishi wa TRA Wanaoomba Rushwa—Uzoefu Wako Ukoje? Tuwafichue hapa

Wadau, naomba uzoefu wenu kuhusu TRA.
Nimeona niwashirikishe jambo ambalo nimekuwa nikikutana nalo katika shughuli zangu za biashara. Kuna baadhi ya watumishi wa TRA ambao, wakati wa kushughulikia masuala ya kikodi au ukaguzi, wamekuwa wakinipa hisia kwamba bila kutoa "Rushwa" au “kitu kidogo” mambo hayawezi kwenda kwa urahisi. Hili limenifanya nijiulize kama ni mimi tu ninayekutana na hali hii au kuna wengine wana uzoefu kama huo.

Bila kuwa mnafiki Kuna Kuna jamaa Afisa Mmoja anaitwa Juma Mapocho Mwakipasile wa ofisi ya Ilala aise huyu jamaa ni kirusi, anaomba Rushwa waziwazi mpaka najiuliza huyu haogopi kufukuzwa?

Kwa wale ambao mmewahi kukutana na hali kama hii, mliombwa nini, katika mazingira gani, na ofisi/tawi gani?

Lengo ni kupata picha ya uzoefu halisi wa wafanyabiashara kuhusu suala hili, si kumshutumu mtu bila ushahidi.

Karibuni kwenye mjadala hasa wale wenye uzoefu wa moja kwa moja.
Hivi wewe unajua madhara ya hiki kitu ulichokiweka hapa? Hivi hata nafsi haikusuti kumtaja mtu kwa majina kutoa shutuma serious kama hizi? Unajua watu wangapi wanamtegemea huyo mtumishi? Akifukuzwa kazi unadhani watu wanaomtegemea wataishije? Machozi yao unadhani yatakuacha salama? Kuwa makini sana na hii dunia bro! Kila kitendo kibaya unachomfanyia mwenzako kitakurudia kwa kipimo kilekile na pengine hata zaidi.
 
Hapana sipo huko mkuu na Wala sikusiki kabisa na hao makaisali.
Nachojaribu kuweka sawa ni watu wasijue pata mwanya wa kuweka majina ya watu kwa kuchafuana kwa chuki zao binafsi
Ninachoamini hata ukimtaja, TRA na Serikali kwa ujumla vina mamlaka za kiuchunguzi ambapo tuhuma isipothibitika kwa ushahidi, baada uchunguzi mtuhimiwa anabaki kuwa huru na anaendeleaj na kazi
 
Wana tamaa za kijinga sana Wafanyakazi wa TRA , Kuna siku nilikuwa nahamisha TIN Kutoka mkoa wa Kodi Kinondoni kwenda Mkoa wa Kodi ILALA , Eti Afisa wa TRA akaniambia nimpooze 😬, nikamwambia Acha tamaa wewe nikupooze nini wakati umekaa kwenye kiyoyozi na mimi nimetoka kupigwa jua huko nje ???
 
Hivi wewe unajua madhara ya hiki kitu ulichokiweka hapa? Hivi hata nafsi haikusuti kumtaja mtu kwa majina kutoa shutuma serious kama hizi? Unajua watu wangapi wanamtegemea huyo mtumishi? Akifukuzwa kazi unadhani watu wanaomtegemea wataishije? Machozi yao unadhani yatakuacha salama? Kuwa makini sana na hii dunia bro! Kila kitendo kibaya unachomfanyia mwenzako kitakurudia kwa kipimo kilekile na pengine hata zaidi.
Unadhani anaponikandamiza kwenye biashara yangu na kuididimiza kupitia Rushwa za kijinga, umefikiria kwamba wanaonitegemea wataishije biashara yangu ikifa? All in All anapaswa kuzingatia maadili katika utendaji wake wa kazi hakuna atakayemuonea
 
Ni mfumo ambao mmekataa kuuacha
Kila mmoja katika nafasi yake anatoa na kupokea Rushwa.

Kila mmoja anajua hapati kitu bila kutoa hongo au Rushwa

Unaenda ofisi imeandikwa ukiombwa rushwa toa taarifa hizo ila ni maandishi tu
Kwanini hawakamatwi Kama traffic police wa Kenya?
Mifumo mibovu sana mpaka kero
Sio kuwa mishahara haiwatosha, hasha Bali ni hulka tu na uroho
 
Hivi wewe unajua madhara ya hiki kitu ulichokiweka hapa? Hivi hata nafsi haikusuti kumtaja mtu kwa majina kutoa shutuma serious kama hizi? Unajua watu wangapi wanamtegemea huyo mtumishi? Akifukuzwa kazi unadhani watu wanaomtegemea wataishije? Machozi yao unadhani yatakuacha salama? Kuwa makini sana na hii dunia bro! Kila kitendo kibaya unachomfanyia mwenzako kitakurudia kwa kipimo kilekile na pengine hata zaidi.
Kwanini aombe rushwa huyo Afisa kwani halipwi mshahara? Maadili ya kazi yake yanamwelekeza kuomba rushwa?

Mimi huwa nawalipua tu huwa nawalipoti kwa kupiga ile namba 0800750075 na nilikuwa nipo recorded kabisa.
 
Hawa maafisa wa kuzuia magendo ndo kirusi kingine. Badala ya kuzuia wanasaidia kuwezesha magendo kusafirishwa au kuingizwa nchini wakishavuta mpunga

Hao Rushwa zao zinaanzia Milioni 30 kwenda Juu. Jamaa wanavuta hadi Milioni 100 tena By Cash...wale waliopo TUNDUMA na Mbeya ni Mashahidi.

Wapo vizuri sana Hawa Jamaa
 
Kwanini aombe rushwa huyo Afisa kwani halipwi mshahara? Maadili ya kazi yake yanamwelekeza kuomba rushwa?

Mimi huwa nawalipua tu huwa nawalipoti kwa kupiga ile namba 0800750075 na nilikuwa nipo recorded kabisa.
Je mrejesho huwa upoje?
Wanafukuzwa au wanahamishwa?
 
Je mrejesho huwa upoje?
Wanafukuzwa au wanahamishwa?
Siwezi kujua maana sijafuatilia , maana nimeshawahi kufanya mara mbili

Kwanza yule aliyetaka hela ili athibitishe TIN No yangu imehamia Mkoa wa Ilala nili shout mbele ya Wenzake yawezekana aliitwa na kuonywa ofisi ni pale jengo la Johari Rotana Hotel halafu yule dogo ni Mzanzibari.

Baada ya kuhamisha TIN no ikawa kituo cha Kodi ni TRA Vingunguti, siku naenda kuchukua control number mida ya saa 8 mchana, eti Mlinzi akawa anaongea kwa nyodo na maringo , Meneja kasema hakuna kazi sasa hivi na haruhusiwi mtu kuingia sasa hivi.

Nikawapigia ile number 0800750075 nikaunganishwa mpaka na Meneja wa TRA Vingunguti akawa anasema kazi ziIlizidi kwahiyo njoo tu ndugu Mteja.

Nikamwambia siku nyingine mimi nishaondoka halafu punguzeni madharau yaani mtu nakuja kulipia nyinyi hamtaki kutoa huduma mnasema mna kazi nyingi.

Sijui nini kilimkuta yule Meneja.
 
Hivi wewe unajua madhara ya hiki kitu ulichokiweka hapa? Hivi hata nafsi haikusuti kumtaja mtu kwa majina kutoa shutuma serious kama hizi? Unajua watu wangapi wanamtegemea huyo mtumishi? Akifukuzwa kazi unadhani watu wanaomtegemea wataishije? Machozi yao unadhani yatakuacha salama? Kuwa makini sana na hii dunia bro! Kila kitendo kibaya unachomfanyia mwenzako kitakurudia kwa kipimo kilekile na pengine hata zaidi.
Mkuu,Akikaa kimya pia kuna madhara,Name and Shame nayo ni Mbaya ila sasa tujiulize Je ni Tuhuma hizi ni za Kweli?Akitakiwa kutoa ushahidi anao?Ameripoti TAKUKURU na Katika Dawati la Malalamiko TRA?

Kwa ninavyofahamu Tatizo la Rushwa TRA msingi wake ni Desturi za Watanzania na Mazoea tuliyawawekea.Nafikiri TRA Tanzania Wanapaswa wafike hapa,wasome hili kisha wafanye Tafakari ya kitaasisi.

Ni Vibaya sana kama Taasisi inafikia hatua kwamba inaaminika kwamba bila Rushwa Hupati huduma bora na ya haki.Kwa sasa Suala hili la Rushwa sio la kulitazama katika mtazamo wa Madhara ya mtu mmoja bali tulitazame katika jicho la Madhara kwa taswira ya Taasisi na Madhara katika Taifa kwa Ujumla.

Maadam Jina lake limetajwa ana options ya ama kujitazama na kujitafakari au achukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu za kitaasisi
 
Siwezi kujua maana sijafuatilia , maana nimeshawahi kufanya mara mbili

Kwanza yule aliyetaka hela ili athibitishe TIN No yangu imehamia Mkoa wa Ilala nili shout mbele ya Wenzake yawezekana aliitwa na kuonywa ofisi ni pale jengo la Johari Rotana Hotel halafu yule dogo ni Mzanzibari.

Baada ya kuhamisha TIN no ikawa kituo cha Kodi ni TRA Vingunguti, siku naenda kuchukua control number mida ya saa 8 mchana, eti Mlinzi akawa anaongea kwa nyodo na maringo , Meneja kasema hakuna kazi sasa hivi na haruhusiwi mtu kuingia sasa hivi.

Nikawapigia ile number 0800750075 nikaunganishwa mpaka na Meneja wa TRA Vingunguti akawa anasema kazi ziIlizidi kwahiyo njoo tu ndugu Mteja.

Nikamwambia siku nyingine mimi nishaondoka halafu punguzeni madharau yaani mtu nakuja kulipia nyinyi hamtaki kutoa huduma mnasema mna kazi nyingi.

Sijui nini kilimkuta yule Meneja.
Na huu Ndio URAIA.Ukiona Jambo linaenda ndivyo sivyo chukua hatua,
 
Wadau, naomba uzoefu wenu kuhusu TRA.
Nimeona niwashirikishe jambo ambalo nimekuwa nikikutana nalo katika shughuli zangu za biashara. Kuna baadhi ya watumishi wa TRA ambao, wakati wa kushughulikia masuala ya kikodi au ukaguzi, wamekuwa wakinipa hisia kwamba bila kutoa "Rushwa" au “kitu kidogo” mambo hayawezi kwenda kwa urahisi. Hili limenifanya nijiulize kama ni mimi tu ninayekutana na hali hii au kuna wengine wana uzoefu kama huo.

Bila kuwa mnafiki Kuna Kuna jamaa Afisa Mmoja anaitwa Juma Mapocho Mwakipasile wa ofisi ya Ilala aise huyu jamaa ni kirusi, anaomba Rushwa waziwazi mpaka najiuliza huyu haogopi kufukuzwa?

Kwa wale ambao mmewahi kukutana na hali kama hii, mliombwa nini, katika mazingira gani, na ofisi/tawi gani?

Lengo ni kupata picha ya uzoefu halisi wa wafanyabiashara kuhusu suala hili, si kumshutumu mtu bila ushahidi.

Karibuni kwenye mjadala hasa wale wenye uzoefu wa moja kwa moja.
Usipowapa rushwa , watatumia sheria zetu hizi za kipumbavu kukunyorosha. Kuna Dada mmoja pale TRA mwenge ambao sasa wamehamia pale mbele, aliwahi kunipa mzigo(deni) la milioni 270......tukakaa mezani, sikubishana nae ila tukaongea tukayajenga yakajengeka pande zote mbili.
 
Hivi wewe unajua madhara ya hiki kitu ulichokiweka hapa? Hivi hata nafsi haikusuti kumtaja mtu kwa majina kutoa shutuma serious kama hizi? Unajua watu wangapi wanamtegemea huyo mtumishi? Akifukuzwa kazi unadhani watu wanaomtegemea wataishije? Machozi yao unadhani yatakuacha salama? Kuwa makini sana na hii dunia bro! Kila kitendo kibaya unachomfanyia mwenzako kitakurudia kwa kipimo kilekile na pengine hata zaidi.
Hapa umeandika utumbo.
Yaani mtu anafanya uhalifu halafu unaleta habari za watu kumtegemea kwani yeye alivyokuwa anaomba rushwa alikuwa hajui kuwa ana wategemezi?au unadhani watu walioko jela hawana wategemezi?sheria huwa haiangalii hivyo,kutegemewa haiwezi kuwa excuse
 
Wadau, naomba uzoefu wenu kuhusu TRA.
Nimeona niwashirikishe jambo ambalo nimekuwa nikikutana nalo katika shughuli zangu za biashara. Kuna baadhi ya watumishi wa TRA ambao, wakati wa kushughulikia masuala ya kikodi au ukaguzi, wamekuwa wakinipa hisia kwamba bila kutoa "Rushwa" au “kitu kidogo” mambo hayawezi kwenda kwa urahisi. Hili limenifanya nijiulize kama ni mimi tu ninayekutana na hali hii au kuna wengine wana uzoefu kama huo.

Bila kuwa mnafiki Kuna Kuna jamaa Afisa Mmoja anaitwa Juma Mapocho Mwakipasile wa ofisi ya Ilala aise huyu jamaa ni kirusi, anaomba Rushwa waziwazi mpaka najiuliza huyu haogopi kufukuzwa?

Kwa wale ambao mmewahi kukutana na hali kama hii, mliombwa nini, katika mazingira gani, na ofisi/tawi gani?

Lengo ni kupata picha ya uzoefu halisi wa wafanyabiashara kuhusu suala hili, si kumshutumu mtu bila ushahidi.

Karibuni kwenye mjadala hasa wale wenye uzoefu wa moja kwa moja.
Manispaa ndio wenye tabu hiyo
 
Usipowapa rushwa , watatumia sheria zetu hizi za kipumbavu kukunyorosha. Kuna Dada mmoja pale TRA mwenge ambao sasa wamehamia pale mbele, aliwahi kunipa mzigo(deni) la milioni 270......tukakaa mezani, sikubishana nae ila tukaongea tukayajenga yakajengeka pande zote mbili.
Duh deni la milioni 270?wakati huo deni halisi lilikuwa ngapi?Yaani hii wanakufosi utake usitake utatoa tu
 
Hivi wewe unajua madhara ya hiki kitu ulichokiweka hapa? Hivi hata nafsi haikusuti kumtaja mtu kwa majina kutoa shutuma serious kama hizi? Unajua watu wangapi wanamtegemea huyo mtumishi? Akifukuzwa kazi unadhani watu wanaomtegemea wataishije? Machozi yao unadhani yatakuacha salama? Kuwa makini sana na hii dunia bro! Kila kitendo kibaya unachomfanyia mwenzako kitakurudia kwa kipimo kilekile na pengine hata zaidi.
Hawawezi kumfukuza mtu kazi kisa jina lake limetajwa mtandaoni. Kama wakiamua kutafuta ukweli wakajiridhisha kuwa kilichosemwa hapa ni kweli akachukuliwa hatua ndio hasa lengo la uzi.
 
Unadhani anaponikandamiza kwenye biashara yangu na kuididimiza kupitia Rushwa za kijinga, umefikiria kwamba wanaonitegemea wataishije biashara yangu ikifa? All in All anapaswa kuzingatia maadili katika utendaji wake wa kazi hakuna atakayemuonea
Kabisa mkuu, watu wanajifikiria wao tu utadhani wafanyabiashara wao hawana familia
 
Back
Top Bottom