Watumishi wa TRA Wanaoomba Rushwa—Uzoefu Wako Ukoje? Tuwafichue hapa

Watumishi wa TRA Wanaoomba Rushwa—Uzoefu Wako Ukoje? Tuwafichue hapa

Ushahidi ninao na nilishaupeleka mamlaka husika na nilishaitwa kutoa udhshidi

Binafsi nikupongeze kwa kuanzisha huu mjadala 😊

Mimi namiliki duka la dawa. Nilipopata changamoto kama hii, nilituma taarifa moja kwa moja TRA kupitia:


Walijibu kwa wakati na walifanya uchunguzi.

Ni vizuri ku-post hapa, lakini kama unataka mtumishi ashughulikiwe rasmi, tuma pia taarifa kupitia mfumo wao.

Kwa uzoefu wangu, TRA ina watumishi wengi wazuri. Tatizo ni wachache wenye tamaa wanaochafua jina la taasisi nzima.
 
Maafisa kazeni wajinga wajinga wanataka kuwaaribia pigeni Offence za maana mtu mpaka apate homa😂😂
 
Vyombo vya kupambana na rushwa vipo,wakilisheni malalamiko yenu sehemu husika
 
Vyombo vya kupambana na rushwa vipo,wakilisheni malalamiko yenu sehemu husika
Washauri ujinga nao watatembeza offence mpaka watakuja tena majukwani kulalamika si unalazimisha wafuate Misahafu ya Kodi inavyotaka?😀😀😀😀
 
Hii ya kutajana majina humo bado sioni ni sawa japo kuwa kweli watajwa hapo juu wakawa na hizo ishara zote za kupenda rushwa ila wapo watakao wataja watu kwa maslahi yao binafsi hira zao binafsi wivu wao, kama mtu anahusika mambo kwa ushahidi wapelekeni kwenye vyombo vinavyopambana na rushwa,
 
Kuna kile kikosi kazi cha kuzuia magendo ndani ya TRA wapo TUNDUMA na Mbeya, aiseeee wale jamaa kuanzia Madereva hadi Maafisa ni Mabilionea wa kutupwa...wanapiga hela wale jamaa na zile Land Cruiser zao za Hardtop zenye namba plate za United Kingdom na zingine Zina namba A au B Hawa jamaa wanapiga hela bhana
Mbeya?
 
Washauri ujinga nao watatembeza offence mpaka watakuja tena majukwani kulalamika si unalazimisha wafuate Misahafu ya Kodi inavyotaka?😀😀😀😀
Kwamba jf ni sehemu ya kupata haki na kuwasilisha lalamiko hapo unatafuta nini labda
 
Hivi wewe unajua madhara ya hiki kitu ulichokiweka hapa? Hivi hata nafsi haikusuti kumtaja mtu kwa majina kutoa shutuma serious kama hizi? Unajua watu wangapi wanamtegemea huyo mtumishi? Akifukuzwa kazi unadhani watu wanaomtegemea wataishije? Machozi yao unadhani yatakuacha salama? Kuwa makini sana na hii dunia bro! Kila kitendo kibaya unachomfanyia mwenzako kitakurudia kwa kipimo kilekile na pengine hata zaidi.
Haaa, we jamaa udhulumu haki za weengine alafu uonewe huruma kwa kuwa tu kuna mandugu au matoto yako yanakutegemea?

Hao unaowafanyia huo ubaya hawana wategemezi?
 
“Mimi kama muhangaikaji siwezi kum-snitch muhangaikaji mwenzangu ikiwa kumpa kitu kidogo kutayafanya yangu yaende”..Huu ni ukweli na utabaki kuwa hivyo.

Hata wewe unayelalamika siyo msafi kiasi hiko kwamba ukikaguliwa leo hautakutwa na dosari,ila inakera kama afisa akaweka limit ya kiasi but kama mnakaa mezani kuzungumza akakusikiliza unamtoaje huyo ni mwana sana usiache kumuweka kwenye circle ya watu wako wa muhimu.
 
Hivi wewe unajua madhara ya hiki kitu ulichokiweka hapa? Hivi hata nafsi haikusuti kumtaja mtu kwa majina kutoa shutuma serious kama hizi? Unajua watu wangapi wanamtegemea huyo mtumishi? Akifukuzwa kazi unadhani watu wanaomtegemea wataishije? Machozi yao unadhani yatakuacha salama? Kuwa makini sana na hii dunia bro! Kila kitendo kibaya unachomfanyia mwenzako kitakurudia kwa kipimo kilekile na pengine hata zaidi.
Mkuu kuna jambo hujaliweka sawa, kama huyo jamaa mambo haya anayafanya kweli na anaumiza watu, Usitegemee waliomtaja hadharani kama watadhurika kwa lolote kamwe hakuna kitu kama hicho, lakini kama wanamsingizia basi yatawarudia
 
Mtarban

Ndugu yangu kwa ushauri tu unaweza Kumrepoti wanayo utaratibu mzuri tu wa kuwashughulikia watumishi wao wachafu na watakupa taarifa/Mrejesho mzuri tu

Wala hakuna haja ya kusnichiana wabongo tunajuana huyo anayelalamika nae akifuatiliwa kesho humkuti sokoni hiyo biashara anafunga.

Halafu anataja kabisa majina ya mtu,kwa faida gani?
 
Hivi wewe unajua madhara ya hiki kitu ulichokiweka hapa? Hivi hata nafsi haikusuti kumtaja mtu kwa majina kutoa shutuma serious kama hizi? Unajua watu wangapi wanamtegemea huyo mtumishi? Akifukuzwa kazi unadhani watu wanaomtegemea wataishije? Machozi yao unadhani yatakuacha salama? Kuwa makini sana na hii dunia bro! Kila kitendo kibaya unachomfanyia mwenzako kitakurudia kwa kipimo kilekile na pengine hata zaidi.
Mwizi mkubwa wewe
 
Unamharibia mtu kazi ni vyema kwenda kumripoti ofisi husika ukiambatanisha na ushahidi.
Wao wanavyochelewesha upatikanaji wa huduma bila ruswha kwani hawafelishi maisha ya wat, hizi huruma zenu za kipuuzi na kihuni ndizo zimetufikisha hapa, yaani washenzi wanaoumiza wengine bila huruma, mnataka nawao huruma itumike kuwahukumu?.

Hii nchi bila maamuzi magumu kwa wavunjaji wa haki haitoendelea
 
Binafsi nikupongeze kwa kuanzisha huu mjadala 😊

Mimi namiliki duka la dawa. Nilipopata changamoto kama hii, nilituma taarifa moja kwa moja TRA kupitia:


Walijibu kwa wakati na walifanya uchunguzi.

Ni vizuri ku-post hapa, lakini kama unataka mtumishi ashughulikiwe rasmi, tuma pia taarifa kupitia mfumo wao.

Kwa uzoefu wangu, TRA ina watumishi wengi wazuri. Tatizo ni wachache wenye tamaa wanaochafua jina la taasisi nzima.
Wengi ni wahovyo kuliko wema
 
Mfumo wa rushwa ni wa nchi nzima,kama wanasiasa na vyama vya siasa hasa ccm kinafanyika hivyo kuna haja ya kumlaumu huyo sisimizi? Kama ICD zinajengwa kambi za kijeshi na Kila kitu kimya huyo ni wa kumlaumu?
Kifupi ni kwamba mifumo imekufa na usimlaumu huyo ndugu
Hili la icd kupewa kambi ya jeshi linatisha sana..
 
Maafisa kazeni wajinga wajinga wanataka kuwaaribia pigeni Offence za maana mtu mpaka apate homa😂😂
Wewe unazani zile offence zinaukweli basi....

Sasa mtu anamtaji wa biashara 10m afu kwenye ukaguzi deni linakuja 100m how!! ni kutengenezeana hofu tu ili uingie king.

Na wanajua kabsa wafanyabiashara wengi hawajui sheria za kodi....+ Ile lugha iliyotumika.
 
Back
Top Bottom