Watumishi wa TRA Wanaoomba Rushwa—Uzoefu Wako Ukoje? Tuwafichue hapa

Safi sana
Kila mtu ajue haki zake
 
TRA leo mmepanic.
 
Hakuna Afisa yoyote anayeomba Rushwa wanaotoa Rushwa ni Walipakodi wenyewe tena baada ya ku default pale ndipo wanamuomba ofisa awapunguzie na kama wakikataa wakasimamia mambo jinsi yalivyo basi kungekua na Vilio vingi narudia walipakodi ndiyo huanza ku approach maafisa ili wapate taafifu kwenye mambo ya Kodi.
 
Haujakutana na kadhia hiyo. Wapi Wanakuomba wao wenyewe. Tena ndo wenyewe.
 
Sheria haina huruma kikubwa awee na ushahidi, hauwezi fumbia macho uhalifu, rushwa ni adui wa haki
 
Hii Nchi suala la Rushwa lilipigwa marufuku na kutoa au kupokea Rushwa liliogopwa kipindi cha Karume, Nyerere mpaka kwa Sokoine...ila sshv usishangae hata wafanyakazi wa TAKUKURU wakikuomba RUSHWA na huna cha kuwafanya
 
Sera ya CCM kwasasa ni marufuku kufichua ufisadi au rushwa.
 
Watanzania wana roho mbaya sana chuki hapo sio rushwa ni kuona huyo jamaa anafanya kazi TRA au ana visa nae..
 
Unaombwa rushwa kama hauna changamoto hizo rushwa mnazitengenezea mazingira wenyewe..
 
Unamharibia mtu kazi ni vyema kwenda kumripoti ofisi husika ukiambatanisha na ushahidi.
Kama unakula Rushwa ukitajwa hatukuharibii Bali ni kuliokoa taifa dhidi ya watu wabadhirifu
Watanzania wana roho mbaya sana chuki hapo sio rushwa ni kuona huyo jamaa anafanya kazi TRA au ana visa nae..
Chuki ili iweje. Yaani hicho kimshahara chake Cha kusuburi siku 30 ndo kisababishe niwe na chuki nae.. Mimi ni miongoni mwa wale wanaochukia Rushwa tu basi.
 
Waliniambia wananidai mapato ya wapangaji wa nyumba yangu wakasema ni milioni moja.nikamuita mmoja wao akadai laki mbili ila nilipe laki moja yaishe nikampq.Tatizo nilipo jumlisha break down yao haikuwa milioni bali laki moja
Ni Arusha
 
Kama unakula Rushwa ukitajwa hatukuharibii Bali ni kuliokoa taifa dhidi ya watu wabadhirifu

Chuki ili iweje. Yaani hicho kimshahara chake Cha kusuburi siku 30 ndo kisababishe niwe na chuki nae.. Mimi ni miongoni mwa wale wanaochukia Rushwa tu basi.
Sio kweli bhana ukweli unaujua mwenyewe hapo ni chuki tu bhana...
 
Waliniambia wananidai mapato ya wapangaji wa nyumba yangu wakasema ni milioni moja.nikamuita mmoja wao akadai laki mbili ila nilipe laki moja yaishe nikampq.Tatizo nilipo jumlisha break down yao haikuwa milioni bali laki moja
Ni Arusha
Duuuuh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…