Watumishi wa Umma ambao hatujapanda daraja tukutane hapa

Watumishi wa Umma ambao hatujapanda daraja tukutane hapa

Madeni yapo na yataendelea kuwepo, hata Marekani inadaiwa. Kaa kwa kutulia shukuru umepanda daraja enzi ya dikteta hata kupanda usingepanda
Una uhakika nimepanda? Au umebuni tu?

Kama hizo hela zipo kwanini wasilipwe kwa pamoja wote? Utashangaa wengine wataona mabadiliko baada ya mwezi mmoja au miezi kadhaa na kusababisha ujazaji wa fomu za Arreas, yanini yote hayo?
 
Una uhakika nimepanda? Au umebuni tu?

Kama hizo hela zipo kwanini wasilipwe kwa pamoja wote? Utashangaa wengine wataona mabadiliko baada ya mwezi mmoja au miezi kadhaa na kusababisha ujazaji wa fomu za Arreas, yanini yote hayo?
Wewe hudaiwi hata kiberiti?
 
Yaan Ofisi ishughulikie Mapunjo
Mtu unalipa mapunjo halafu unapunjwa tena
Maana kodi wamekata kila kitu lakini bado wamekata na nyingine
Sasa sijajua shida ni nini
 
Mlikuwa mmepata barua za kupanda daraja?

Kuna kitu kilinichanganya. Waziri wa utumishi siku za nyuma alisema wamepanga kupandisha madaraja watumishi elfu 90. Lakini juzi kati taarifa ikatoka sijui wamepandisha watumishi elfu 70 hivi. Sasa wale elfu 20 wameenda wapi? au wanapandisha taratibu. Tuweni na subira!
 
Baada ya mbwembwe nyingi na mshahara kuchelewa tukiamini kuwa tutapanda madaraja, hatimaye salary imetoka bila mabadiliko yoyote! Vipi huko uliko mtumishi upi katika hali gani?
nimeumia sana,hawa viongozi wetu wanaumiza akili zetu yaani miaka 8 sijapanda daraja tangu niajiriwe naishije na huu mshahara wa ualimu na hapo bado nmb mkopo nakatwa
 
Mi hapa Manispaa ya Morogoro idara ya afya sijapanda daraja, ila kuna baadhi ya watumishi wenzetu wamepanda, tulipouliza tumeambiwa tutapandishwa mwezi ujao, tunavuta Subira.
 
Back
Top Bottom