SI KWELI Watumishi wa Umma waliofukuzwa kazi kimakosa 2018-2023 kurudishwa

SI KWELI Watumishi wa Umma waliofukuzwa kazi kimakosa 2018-2023 kurudishwa

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Hapo sijui wanataka kufanya nini. Kuna ukweli wowote hapa?

1736312050458.png
 
Tunachokijua
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (OR-MUUUB) imekuwa na jukumu la kuimarisha Utawala Bora katika uendeshaji wa shughuli za Serikali kwa kubuni Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu za uendeshaji na usimamizi wa shughuli za utumishi wa umma na kujenga uwezo wa watumishi wa Umma ili watoe huduma bora kwa wananchi.

Aidha Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) ni idara inayojitegemea iliyoanzishwa na Kifungu cha 29 (1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma SURA 298 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya 2007. PSRS ilianzishwa ili kuwezesha mchakato wa kuajiri kwa niaba ya Serikali.

Kumekuwapo na taarifa kuwa watumishi wa umma waliofukuzwa kazini kimakosa mwaka 2018 mpaka 2023 watarudishwa kazini,


Je ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck ulibaini kuwa Barua iliyo na taarifa hiyo si ya kweli kwani haikutolewa na Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Aidha tovuti na kurasa za mitandao ya kijamii za sekretarieti ya ajira ndizo huchapicha matangazo yenye taarifa zihusuzo ajira katika utumishi wa umma.

Aidha barua hiyo imebainika kuwa na mapungufu kadhaa yanayoitofautisha na barua rasmi ambazo huchapishwa katika kurasa za mitandao ya kijamii, za Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wala, mapungufu hayo ni pamoja na uwepo wa namba ya mtandao wa Whatsapp kwa ajili ya kuwasilishia nyaraka tofauti na utaratibu rasmi.

Pia kutofautiana kwa namba ya simu ya ofisi iliyopo kwenye anwani, ambapo Ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora hutumia Simu Na: +255 (026) 2963630 Nukushi: +255 (026) 2963629 tofauti na iliyohaririwa katika barua iliyopotoshwa ikionekana Simu Na: +255 615 976 097 Nukushi: +255 (026) 2963629

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeikanusha barua hiyo kwani si ya kweli huku ikiwataka wananchi kuipuuza.


Aidha upotoshaji wa aina hii si mara ya kwanza kufanyika rejea hapa na hapa kuona barua isiyokuwa ya kweli inayofanana maudhui yake na barua hii ya sasa.​
Nimejaribu kuhakiki jina la Mary naona ni la kweli na hata namba za ofisi tajwa ni sahihi pia.
Kwa akili hizi ,CCM itatawala sana

Kama member wa Jf unaingia mkenge kirahisi hivi,habari gani kwa member wa Facebook,insta na TikTok?

Ngoja na Mimi niwe tapeli tu kama watu wenyewe ndio hawa
 
Sio sawa kuwaita walimu zero brain kwanza Hilo tangazo lenyewe la kitapeli
Kaka kwa vile ume acha matusi, acha niku eleweshe nime sema zero brain Kama kina mpwayungu.

rejea kauli ya kuwa daka "maboya", huwa huoni baadhi ya waalimu wenye akili chache wanao vaaga mi kofia na kubeba mabango ya kijani siku za kampeni??

Kisa tu wame pewa vitenge na elfu kadhaa??, nina wakubwa zangu ni waalimu, hivyo situkani hovyo.
 
Kaka kwa vile ume acha matusi, acha niku eleweshe nime sema zero brain Kama kina mpwayungu.

rejea kauli ya kuwa daka "maboya", huwa huoni baadhi ya waalimu wenye akili chache wanao vaaga mi kofia na kubeba mabango ya kijani siku za kampeni??

Kisa tu wame pewa vitenge na elfu kadhaa??, nina wakubwa zangu ni waalimu, hivyo situkani hovyo.
Mkuu sometimes mamlaka zinawashindikiza na muda mwingine wanapewa posho kidogo watafanya Nini?
 
Serikali ya Mama haitaki mtu aonewe ila ndani ya utumishi wa umma kuna baadhi ya viongozi wenye dhamana wanawaonea sana walio chini hadi kufikia kufukuzwa kazi au kusimamishwa au hata kushushwa kwasababu tu ya MAJUNGU, FITINA NA UNAFIKI. Mambo hayo ndio yametqmalaki huko.
Menejimenti inapaswa iwalinde watumishi wote bila ubaguzi haswa walio chini.
Pongezi kwao.
 
Mkuu sometimes mamlaka zinawashindikiza na muda mwingine wanapewa posho kidogo watafanya Nini?
yaani mamlaka ambayo haya oni sababu ya kuku boreshea maslahi, halafu siku ya kampeni uka pigwe jua kisa laki au hata 1m ya kila Baada ya miaka 5 we una oa ni sawa??.

mki sema hatu endi mpaka uboreshe hapa na hapaz wata wafuta kazi wote??
 
Kwa akili hizi ,CCM itatawala sana

Kama member wa Jf unaingia mkenge kirahisi hivi,habari gani kwa member wa Facebook,insta na TikTok?

Ngoja na Mimi niwe tapeli tu kama watu wenyewe ndio hawa
Juha kweli wewe.
Sasa na wewe ndio unajiona mjanja kweli?

Muwe mnaelewa kile kilichoandikwa basi.
 
"Kwa wale watakao ona kimya. "

Mbona tangazo ni kama limeandaliwa na wahuni? Serikali huwa inatoa mrejesho na sio kukaa kimya. Na wana njia zao za kurudisha mrejesho
Wametoa na WhatsApp number haaa haaa
 
Back
Top Bottom