SI KWELI Watumishi wa Umma waliofukuzwa kazi kimakosa 2018-2023 kurudishwa

SI KWELI Watumishi wa Umma waliofukuzwa kazi kimakosa 2018-2023 kurudishwa

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Hapo sijui wanataka kufanya nini. Kuna ukweli wowote hapa?

1736312050458.png
 
Tunachokijua
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (OR-MUUUB) imekuwa na jukumu la kuimarisha Utawala Bora katika uendeshaji wa shughuli za Serikali kwa kubuni Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu za uendeshaji na usimamizi wa shughuli za utumishi wa umma na kujenga uwezo wa watumishi wa Umma ili watoe huduma bora kwa wananchi.

Aidha Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) ni idara inayojitegemea iliyoanzishwa na Kifungu cha 29 (1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma SURA 298 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya 2007. PSRS ilianzishwa ili kuwezesha mchakato wa kuajiri kwa niaba ya Serikali.

Kumekuwapo na taarifa kuwa watumishi wa umma waliofukuzwa kazini kimakosa mwaka 2018 mpaka 2023 watarudishwa kazini,


Je ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck ulibaini kuwa Barua iliyo na taarifa hiyo si ya kweli kwani haikutolewa na Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Aidha tovuti na kurasa za mitandao ya kijamii za sekretarieti ya ajira ndizo huchapicha matangazo yenye taarifa zihusuzo ajira katika utumishi wa umma.

Aidha barua hiyo imebainika kuwa na mapungufu kadhaa yanayoitofautisha na barua rasmi ambazo huchapishwa katika kurasa za mitandao ya kijamii, za Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wala, mapungufu hayo ni pamoja na uwepo wa namba ya mtandao wa Whatsapp kwa ajili ya kuwasilishia nyaraka tofauti na utaratibu rasmi.

Pia kutofautiana kwa namba ya simu ya ofisi iliyopo kwenye anwani, ambapo Ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora hutumia Simu Na: +255 (026) 2963630 Nukushi: +255 (026) 2963629 tofauti na iliyohaririwa katika barua iliyopotoshwa ikionekana Simu Na: +255 615 976 097 Nukushi: +255 (026) 2963629

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeikanusha barua hiyo kwani si ya kweli huku ikiwataka wananchi kuipuuza.


Aidha upotoshaji wa aina hii si mara ya kwanza kufanyika rejea hapa na hapa kuona barua isiyokuwa ya kweli inayofanana maudhui yake na barua hii ya sasa.​
Mtindo anaoutumia Samia ni kama tu wa JK yaani wqnajifanya wanawahurumia sana wafanyakazi huku wakipora rasilimali za taifa kwa kiwango cha kutisha, na ni kwasababu wapiga kelele wengi ni wasomi so wakipozwa kidogo tu wanawaona watawala wa namna hii wana huruma kumbe nchi inatafunwa vibaya sana mnachopewa ni punje ya mchanga katika mchanga wa bahari. Usalama wa taifa fanyeni kazi yenu ya kulinda rasilimali za nchi nyinyi ndiyo mmeapa kwa hilo haya maswala la watu wachache kujilimbikizia kulikopotoliza ni kulinyonya taifa hili ambalo litakuwepo kwa muda mrefu kuliko sisi ambao hata kama utaiba namna gani au utauza rasilimali za nchi namna gani na kupata mihela ya kutosha bado huna uwezo wa kuishi hata miaka 100 ila utakuwa umevigharimu kwa kiwango kikubwa vizazi vijavyo.
 
Utumishi😀
 

Attachments

  • C5D74CE6-2AD6-4FD5-A944-F6297B14EDC2.png
    C5D74CE6-2AD6-4FD5-A944-F6297B14EDC2.png
    1.5 MB · Views: 4
Watapata watu wa kuwatapeli maana wajinga bado ni wengi.
 
Wakuu kuna hii taarifa kuwa watumishi wa umma waliofukuzwa kazini kimakosa 2018-2023 watarudishwa kazini, tafadhali naomba msaada wa kupata uhalisia wake
1736312050458.png
 
Hapo kuna.watu wanatafutwa kupigwa,,,,ukishaona tangazo lina namba za simu ujue ni UTAPELI
 
Back
Top Bottom