Watumishi wa Umma waliotia nia kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa kukatwa mshahara wa mwezi Julai

Watumishi wa Umma waliotia nia kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa kukatwa mshahara wa mwezi Julai

Zipo taarifa za kuzuia mishahara ya watumishi waliogombea nafasi mbalimbali katika mwezi huu wa Julai, aliyetoa ushauri huu ana nia ya kutaka kumuharibia Rais Magufuli 2020, Oktoba 28.

Rais Magufuli nikuombe uingilie kati hili, si jambo la afya na ukingazatia watia nia hao wataombwa kwenda kusaidia kuweka umoja katika majimbo waliogombea, nani atakubali kwenda kusaidia chama wakati mshahara wake ulikatwa...
Mkuu, ndiyo tayari wameshatia nia .je hadi Leo hii umesiikia kusitishwa mshahara kwa mtumishi yeyote ndani ya nchi yetu Tanzania.
 
Kuna tangazo linazunguka juu ya kutolipwa mishahara kwa wafanyakazi wa umma ambao walichukua fomu za kuomba kupata ridhaa kutokak chama cha mapinduzi ili wapeperushe bendera ya kuwania nafasi za ubunge.

Binafsi naunga mkono katazo la kutolipwa mshahara wa mwezi huu wa julai, ila kwa mtazamo wangu hawa wangefukuzwa na kufutwa kabisa katika utumishi wa umma..
Mkuu kwani.sifa kuwania ubunge ni zipi? Kama mtu ndoto yake siku moja kuwa MP.
Kuwa mtumishi wa umma siyo hoja.atatoka huyu aliyemaliza chuo nae atacover naafasi hiyo.wote lengo lao kulijenga taifa.
 
Unajua maana umma ni nini?
Mimi mwenyewe ni mtumishi wa umma na ninajua. Watumishi wa umma ni wale walio chini ya sheria ya public service act. Kumbuka Wapo watumishi wengi tu ambao hawapo chini ya sheria hiyo ikiwemo polisi JWTZ n.k
 
Mimi mwenyewe ni mtumishi wa umma na ninajua. Watumishi wa umma ni wale walio chini ya sheria ya public service act. Kumbuka polisi, JWTZ hawapo chini ya sheria hii. Wapo watumishi wengi tu ambao hawapo chini ya sheria hiyo
Umma ni nini?
 
Umma ni nini?
Umma ina maana yake kilugha lkn neno "watumishi wa umma" lina maana yake pia kisheria kwa mujibu wa public service act. Kwa lugha nyepesi ni kuwa Watumishi wa umma ni wale walio chini ya sheria ya public service act. Kumbuka Wapo watumishi wengi tu ambao hawapo chini ya sheria hiyo ikiwemo polisi JWTZ n.k
 
Waajiri wengi wamezingatia maelekezo ya kuwasimamishia wafanyakazi wao mishahara Mwezi Julai kwa sababu eti wametia nia na kuchukua fomu za kugombea uongozi.

Hili jambo linafanyika vibaya sana na kukomoana. Kuna mtu anaenda kazini na anafanya kazi zake kama kawaida na anachukua ruhusa ya majuma mawili au moja anaenda anachukua fomu anaijaza anairudisha anashiriki mchakato anajiona amepata kura moja au sifuri anarudi kazi kwake faster anaendelea na kazi, eti leo unamkata mshahara wote wa Julai!? Hizi hii ni akili au utopolo au matope? Serikali acheni hizo bhana!

Kwa nini nchi hii mnanyanyasa sana wafanyakazi wa umma? Hivi wamekosea nini? Pyuu!
 
Sio julai tu, hutakua na mshahara mpaka September.
Kama ulikurupuka na laki moja yako bila kusoma waraka wa utumishi, jiandae kisaikolojia.
 
Vijana kibao hawana ajira nyie mnaajira na bado mnatamaa.sasa ngoja yawakute
 
Back
Top Bottom