Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Pengine upo sahihi!
Sasa hilo dhumuni linasomewa kozi gani ili lieleweke??
Mimi nadhani ifike mahali tukubaliane kuwa tuna vitambulisho rasmi vinavyopaswa kututambulisha kokote pale. Na hivyo vitambulisho vimebeba taarifa nyingi na nyeti sana! Kwanini zisiwe synchronized??
Mbona mitandao ya simu imefanikiwa?? Kwamba namba ya NIDA au kivuli cha kitambulisho husika kinatosha kutumika kutafuta taarifa nyingine pindi zinapohitajika.
Huko maofisini na kwingineko watu wasiombwe ombwe tena hizo taarifa sensitive!

NB: Kwa kuwa mnawaomba omba hizo taarifa wakiwatuhumu kwa udini na ukabila msikatae...!
 
Mzee hii ni simple sana kung'amua.

Mfumo wa nchi umeshakwama kutambua raia wake na wale wa kigeni

Kuna baadhi ya taarifa zinasema kuna mapandikizi wa kigeni mpaka kwenye mifumo yetu ya usalama.

Sasa katika kushindwa huko, sasa wanatonesha dhahiri kuwa shughuli ewashinda na hii mannual aunthentication ndo inaenda kuharibu zaidi. Hawajui kukimbiza mwivi kimya kimya.

Hii mifumo yetu ya usalama ingelikuwa chama cha siasa, tungebadili tuweke wengine. Lakini mfumo wetu imara umejengwa kwenye misingi ya kisiasa ndo maana hata teknolojia ya udukuzi hawaumizi vichwa kuja na gadgets bali wanaagiza Israel ambao nao pia wanawadukua

Hii fomu ni kinyume na Katiba ya Tanzania
 
Polisi wanachukua taarifa za dini ya mtu na kabila lake, sijawahi kuona watu wakihoji hili
Ni makosa sana... Ni sawa na wale wanaochukua taarifa za jinsia ya mtu... Unaweza kuta mtu mwenyewe hana uhakika na jinsia yake!!

Tupinge dalili za ubaguzi pindi tuzionapo!!
 
Usawa wa kidini ni ushenzi tu.

Ina maana nchi hii ni ya wakristo na waislam pekee?

Nawaambia itakuja mvua kufagia fagia hizi taka za udini mshangae
 
Kwa leo zinahitajikaje?
 
Ni makosa sana... Ni sawa na wale wanaochukua taarifa za jinsia ya mtu... Unaweza kuta mtu mwenyewe hana uhakika na jinsia yake!!

Tupinge dalili za ubaguzi pindi tuzionapo!!
bora wewe uko fair.

Wengine hawana tabu na tatizo kuchukua taarifa za jinsia, marital status ila inapokuja suala la Dini wanang'aka kwelikweli. Huenda ni kwa sababu wanataka ajira za serikalini ziende kwa watu wa dini yao halafu hayo yafanyike gizani
 
Kwa leo zinahitajikaje?
Ni jambo la kawaida, sio jambo geni labda kama wewe ni mgeni kwenye utumishi wa umma. Hizo takwimu, ni muhimu sana kujua, kwasasa Serikalini waislamu ni wa kumulika na tochi, binafsi sijui ni kwa nini.
 
kwa hiyo wako sahihi ila tu kwa nini wahoji leo? weka facts acha kulialia. Logic ya kutaka dini na kabila ni ipi,weka facts
Tunapinga udini na ukabila
Twende kwenye hizo facts;

2015-2020 ulikuwa na miaka miwili (infant) kwamba hukuona lolote linaloendelea?!!

Ulikuwa na usonji kwamba hukuona chochote chenye uashiria wa udini au ukabila ukakikemea?!!

Kama issue ni kufuta hivyo vipengele, kwanini mng'ang'anie kumshambulia huyu mama kuwa mdini wakati kavikuta wala hajavianzisha yeye?!! Si angalau mngetoa ushauri kwa serikali kwa ujumla wake kuwa iviondoe. Sasa suala la anataka kuweka waislamu wenzie linatoka wapi km sio chuki za kidini?!!

Mna chuki sana nyie!!
 
Tanzania ni nchi ya kijinga sana.

Sasa kwa mfano hali ya ndoa ya mtu inahusu nini? Inahusiana nini na kazi aifanyayo mtu?
Ni mengi ya kushangaza. Hawakusaidii kulea mke au hawara, ila wanataka mtumishi uwaambie.
Ni kama vile ofisi za umma hazina KPIs..
 
Mbona jinsia imewekwa hapo na huoni Kama tatizo!?..kinachokutisha kujua dini za watz ni nini!?
 
Unajua kuna mtu ukisoma comment yake unajua kabisa ana akili na anaitumia ipasavyo, wewe ni mmoja wao mkuu, hongera! Umeeleza vizuri sana. Na kama kuna wadau wa mamlaka zinazohusika na hili basi hawanabudi kuufanyia kazi ushauri wako.
 
Du hata kwenye sensa kipengele cha dini na kabila halipo,kwa kuamini Tanzania haina udini na ukabila, hata ukitaka kufanya tafiti mojawapo ya masharti ya kupitishwa kwa dodoso la utafiti ni kutokuweka kipengele cha dini na kabila.
Ni kweli, unataka kufanya utafiti, utalazimika kutouliza Dini, Kabila. Na hii ni sahihi kabisa.
Umri sawa, una maana. Jinsia, ina maana. Elimu ina maana
Dini na Kabila vinatija gani? Tunataka kuamua jambo gani?
 
Unataka kujaza wat Serikalini kwa dini zao na si kwa ubora wa viwango? Ndiyo sababu mmemtoa Lukuvi na kumweka Riziwani? Hii nchi si ya kidini. Kama mnataka kujenga nchi kwa misingi ya dini nendeni mkaanzishe himaya kwenye jangwa la Syria halina watu. Tanzania ni ya watu wote bila kujadli dini wala makabila yao. Usinipe hasira kwa kuonyesha ujinga.
Ni jambo la kawaida, sio jambo geni labda kama wewe ni mgeni kwenye utumishi wa umma. Hizo takwimu, ni muhimu sana kujua, kwasasa Serikalini waislamu ni wa kumulika na tochi, binafsi sijui ni kwa nini.
 
Data na information yoyote ya mambo ya kijamii ni muhimu kwa serikali. Inasaidia serikali kwenye mambo mengi ikiwemo affirmative action ikibidi au kwenye kuzuia udini na ukabila kwenye ajira.
Basi tufufue na matamasha ya kikabila na kidini, na yafanyike Kila mkoa, na serikali isimamie.
Na hizi Ngoma za kikabila zifanywe Kila shule, na ziende hadi Taifa.
Tushindanishe na Dini,
Tufungue kabisa, serikali ijue watu wake.
Asante.
 
Mkuu mbona hiyo form Ina mambo mengi mkuu, umeona dini na kabila tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…