Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Kila jambo msilolipenda linalofanywa na serikali ya Mh.Samia lawama mnamsukumia Mh.Kikwete!!!

Hii siyo sahihi, mengine huyo mzee hausiki ni udhaifu wa aliyepo kwenye kiti.
Ifike wakati huyu mama awajibike yeye kwa makosa yake.
 
Kwan baraza zima la mawazir wengi islamic au christian?
 
Huu ni upumbavu na hatari kubwa!

Serikali inataka kujenga makanisa na misikiti? Serikali inataka kutengeneza taratibu za kufanya matambiko?

Mwalimu must be rolling in his grave!
Kwenye usajili wa vyeti mbona hampingi udini na ukabila? We ukiombwa cheti cha kuzaliwa dini na kabila lako halipo?
 
Nafikiri hio itakuwa sio mandatory field...

Yaani haina ulazima wa kujiza sana kwasababu kuna watu ambao hawa amini katika dini yoyote.
 
Mkuu sio kundi dogo, ni udini, element of Christianity, they want uchifu na uislamu na mambo maovu kama mimba mashuleni, wanawake kutawala dunia, kuweka nchi rehani kwa matajiri na mabeberu n.k ndio uelekeo unaoonekana kwa dots zilizopo,
Sasa kwa ushetani huu, tunafanya nini?
 
Kama mbwai mbwai tu , lakini lazma tuchunguze na kuleta uwiano sawa kwenye sirikali, sio dini fulani au kabila moja mkurugenz hadi mfagiaji.
Sheikh leo hitma inasomwa wapi nije kula ubwabwa.
 
Point kubwa sana hii.
Halafu nashangaa kwa nini watu wanataka ku justify mambo haya eti kisa mazishi.

Nani aliwaambia serikali inazika watumishi waliokufa?!
 
Tanzania ni ya watu wote na uwakilishi serikalini unapaswa kureflect makundi yote ya watanzania. Huwezi ukawa na Serikali ya wanyakyusa pekee halafu ukasema Tanzania ni ya watu wote. Huwezi ukawa na Serikali ya wakristo pekee halafu ukasema Tanzania ni ya watu wote. Lazima kuwe na uwiano wa makundi ya watu na watumishi wa umma. Kumbuka Serikali ndio inaamua kwa niaba ya watu wote, kama hakuna uwiano, maamuzi yatakuwa ya upendeleo na kuathiri makundi mengine.

Mambo aliyokuwa akifanya JPM kama akifanya mama Samia leo hii nina hakika patachimbika, waislamu ni wavumilivu sana hakika, wakristo ni wadini sanaaa. Imagine mama Samia ateue wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, makatibu wakuu, wakurugenzi, makatibu tawala halafu katika hao wote 80% wawe waislamu. Nina hakika wakristo mtapiga makelele kwenye kila kona nchi hii. JPM alifanya hivyo lkn hamkusema chochote zaidi ya kumsifu, ajabu sana. Leo Samia kajaribu tu kuweka mizani ikae sawa, mmeanza kupiga makelele, mlitaka muendelee kupendelewa pekee yenu? nchi sio yenu peke yenu ndugu zangu.
 
Hujui kuna mfumo wa kidini unapendelewa, wacha uvunjwe
 
Ulipokuwa unasikia CHADEMA wakidai katiba mpya wewe ulidhani ni wajinga?
Sasa anza hapo hapo ulipo kudai katiba mpya.
 
Naunga mkono hoja, tunaficha nini? Kwanini tufiche? Siri ya nini wakati mtaani tunajuana kwa dini zetu na hata umoja wa kidini upo makazini na mitaani, kwanini iwe Siri serikalini? Lazima kuna kundi linanufaika na halitaki ijulikane.
 
Asante Sheikh zmohamed,japo uzi wa shura ya uramaa umefungwa na moderators.
 
Hii takwimu sio ngeni, umeamua tu kuleta taharuki. Takwimu hizi zipo karibu kila sehemu kwenye nchi hii.
 
Swali la kuulizwa dini yako linaulizwa sehemu nyingi kama vile hospitalini, mahakamani, polisi n. k
Kwa nini iwe nongwa kuulizwa wakati wa ajira?

Serikali lazima iwe na data ili kuweza kudhibiti ubaguzi katika ajira
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…