Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Kila jambo msilolipenda linalofanywa na serikali ya Mh.Samia lawama mnamsukumia Mh.Kikwete!!!

Hii siyo sahihi, mengine huyo mzee hausiki ni udhaifu wa aliyepo kwenye kiti.
Ifike wakati huyu mama awajibike yeye kwa makosa yake.
 
Mama anataka kufanya usawa wa kidini kwenye uteuzi.

Huoni leo akiteua mkirito lazima ateue na musilamu, akiondoa mkiristo anaweka muislamu.

Angalia baraza la mawaziri toka ameingia, ameondoa wakristo 7 akateua waislamu 7 ila akawawekea wasaidizi wakristo.

Yeye mama akiteua boss muislamu basi msaidizi wake ni mkiristo.

Kwa sasa anataka dini zenu ili anapofanya uteuzi ajue wewe ni dini gani akupe ama ampe mwingine.

Wanasema wanataka kuvunja mfumo kristo.
Kwan baraza zima la mawazir wengi islamic au christian?
 
Huu ni upumbavu na hatari kubwa!

Serikali inataka kujenga makanisa na misikiti? Serikali inataka kutengeneza taratibu za kufanya matambiko?

Mwalimu must be rolling in his grave!
Kwenye usajili wa vyeti mbona hampingi udini na ukabila? We ukiombwa cheti cha kuzaliwa dini na kabila lako halipo?
 
Nafikiri hio itakuwa sio mandatory field...

Yaani haina ulazima wa kujiza sana kwasababu kuna watu ambao hawa amini katika dini yoyote.
 
Mkuu sio kundi dogo, ni udini, element of Christianity, they want uchifu na uislamu na mambo maovu kama mimba mashuleni, wanawake kutawala dunia, kuweka nchi rehani kwa matajiri na mabeberu n.k ndio uelekeo unaoonekana kwa dots zilizopo,
Sasa kwa ushetani huu, tunafanya nini?
 
Kama mbwai mbwai tu , lakini lazma tuchunguze na kuleta uwiano sawa kwenye sirikali, sio dini fulani au kabila moja mkurugenz hadi mfagiaji.
Tulizeni mishono dawa iwaangie, tuhuma za udini na ukabila kwenye taasisi za sirikali zimekithirini sana, sasa mama anachunguza je ni kweli ama laa? Hakuna ubaya kuchunguza tuhuma nzito kama hizo ,

Kama mbwai mbwai tu , lakini lazma tuchunguze na kuleta uwiano sawa kwenye sirikali, sio dini fulani au kabila moja mkurugenz hadi mfagiaji.

Keki ya taifa lazma watu wote wapate . Haki na usawa
Sheikh leo hitma inasomwa wapi nije kula ubwabwa.
 
Unataka ushughulike na marehemu kama nani?
Mfanyakazi anapashwa kuweka contact information ya ndugu jamaa kama kuna jambo la dharura... hao ndio watajua imani ya Mtumishi
Hii dini kabila is nonsense
Vitambulisho vya Taifa ndio muhimu mengine hayawahusu (Uraia ndio muhimu) tumeajiri wageni wengi mno

Mtumishi aelimishwe namna ya kuandaa 'Will'
Point kubwa sana hii.
Halafu nashangaa kwa nini watu wanataka ku justify mambo haya eti kisa mazishi.

Nani aliwaambia serikali inazika watumishi waliokufa?!
 
Unataka kujaza wat Serikalini kwa dini zao na si kwa ubora wa viwango? Ndiyo sababu mmemtoa Lukuvi na kumweka Riziwani? Hii nchi si ya kidini. Kama mnataka kujenga nchi kwa misingi ya dini nendeni mkaanzishe himaya kwenye jangwa la Syria halina watu. Tanzania ni ya watu wote bila kujadli dini wala makabila yao. Usinipe hasira kwa kuonyesha ujinga.
Tanzania ni ya watu wote na uwakilishi serikalini unapaswa kureflect makundi yote ya watanzania. Huwezi ukawa na Serikali ya wanyakyusa pekee halafu ukasema Tanzania ni ya watu wote. Huwezi ukawa na Serikali ya wakristo pekee halafu ukasema Tanzania ni ya watu wote. Lazima kuwe na uwiano wa makundi ya watu na watumishi wa umma. Kumbuka Serikali ndio inaamua kwa niaba ya watu wote, kama hakuna uwiano, maamuzi yatakuwa ya upendeleo na kuathiri makundi mengine.

Mambo aliyokuwa akifanya JPM kama akifanya mama Samia leo hii nina hakika patachimbika, waislamu ni wavumilivu sana hakika, wakristo ni wadini sanaaa. Imagine mama Samia ateue wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, makatibu wakuu, wakurugenzi, makatibu tawala halafu katika hao wote 80% wawe waislamu. Nina hakika wakristo mtapiga makelele kwenye kila kona nchi hii. JPM alifanya hivyo lkn hamkusema chochote zaidi ya kumsifu, ajabu sana. Leo Samia kajaribu tu kuweka mizani ikae sawa, mmeanza kupiga makelele, mlitaka muendelee kupendelewa pekee yenu? nchi sio yenu peke yenu ndugu zangu.
 
Hujui kuna mfumo wa kidini unapendelewa, wacha uvunjwe
 
Habari wana JF ..

Mimi niliahidi sitamkosoa Rais Samia, kwa sababu nilishawakosoa sana ma Rais wa nchi hii hadi nachoka; lakini Kuna mambo ni mazito huwezi hata kufikiri yanaweza kufanyika kwa karne hii.

Mimi niwaombe Serikali, niwaombe CCM, niwaombe washauri wa Rais, kama mmechoka, mtuachie hili Taifa.
Wengine bado tunataka kuliona Taifa letu likiwa moja.

Vyombo vya usalama, basi mshaurini mheshimiwa Rais vizuri, msijisahau sana mkaiacha nchi kwenye auto-pilot.
Niwakumbusheni Taifa hili halikujengwa kwa matofali, la hasha!

Mpitisheni Mh. Rais katika historia ndogo ndogo zile njema, zilizotufanya Watanzania japo tukawa wamoja, potelea pote na umaskini wetu.

Sasa hamuwezi amini, leo hii Hazina inaomba taarifa za watumishi (CV), na miongoni mwa taarifa wanazotakiwa kujaza hao watumishi ni:-
1. Kabila lako .....
2. Dini yako .......

Zipo taarifa zingine, za kipuuzi zinazoombwa, ila haina haja sana kuzitaja, kwani hazina athari sana kama hizi mbili.

Hivi kweli, leo mnataka DINI ya mtumishi, iwasaidie nini?
Hii taarifa mnaitumia kuboresha nini?
Udini wa nini katika Tz ya leo.
Tuna ajenda gani na Dini za watu, (watumishi). DINI, DINI.....DINI...!!!!?....,leo tunauliza DINI yako ni ipi? Kweli mh. Rais Samia.

Halafu mnataka na KABILA, kabila la mtumishi litumike kuboresha nini?
Mna ajenda gani huko?

KABILA, leo mnamuuliza mtu KABILA. Kweli mh Rais Samia , ulisema wewe huna kabila, sijui ni Mzanzibar, sasa hawa watumishi, karne ya 21, mwaka 2022, wawajazie makabila yao, muyajue, myafanyie nini?!

Mh Rais Samia, hebu kataa mambo mengine.

Siku Taifa hili likiparaganyika mikononi mwako, hao unaowaona, watakukataa.

Mfumo wa CV (format) na taarifa zinazotakiwa nimeambatanisha hapa.
denooJ , MTAZAMO , barafu , Tindo , Chige , shige2 , Malcolm X5 , MALCOM LUMUMBA ,

Ulipokuwa unasikia CHADEMA wakidai katiba mpya wewe ulidhani ni wajinga?
Sasa anza hapo hapo ulipo kudai katiba mpya.
 
Kwanini unashangaa hili, mbona mashuleni ni kitu cha kawaida miaka yote kuulizwa DINI yako na KABILA lako. Hii ipo siku zote mashuleni toka chekechea mpaka chuo kikuu. Nami kwa kweli siku zote nilikuwa najiuliza kwanini mwenendo huo uishie chuo kikuu na mavyuoni, katika ajira ni marufuku?

Nimefuatilia nchi nyingi (hata zilizoendelea UK, Amerika, Ufaransa n.k) kipengele cha dini kipo, kwanini kisiwepo TZ. Hivi tunaficha nini? Kwani huko makazini na mitaani hatujuani kuwa wewe ni dini hii na mii ni dini ile, kuna shida gani katika hilo au ikiwa katika makaratasi ndio tabu. Hivi tunaficha nini? Tusingejua dini za wabunge wetu hivi wangeapa kwa kutumia kitabu kipi, inamaanisha waliziandika dini zao katika fomu za ugombea. Tuache unafiki, kama tunataka transparency/uwazi mambo hayo ni lazima yawepo katika ngazi zote, kwa vile hiyo ndio identity yetu.

Kuna mashirika yanafahamika kuwa usipokuwa kabila fulani si rahisi kupata kazi. Niliwahi ambiwa kuwa TANROAD usihangaike kama si kabila fulani si rahisi kupata kazi, halikadhalika BIMA, BOT, n.k. Kama hii itawagusa poleni, ila ni njia sahihi kuelekea kwenye uwazi.
Naunga mkono hoja, tunaficha nini? Kwanini tufiche? Siri ya nini wakati mtaani tunajuana kwa dini zetu na hata umoja wa kidini upo makazini na mitaani, kwanini iwe Siri serikalini? Lazima kuna kundi linanufaika na halitaki ijulikane.
 
Inside 10,
Napenda kwanza kukufahamisha kuwa hii ratio ya 20:80 kuonyesha uwiano baina ya Waislam na Wakristo katika kuhodhi nafasi katika serikali ya Tanzania si zangu mimi kama ulivyoandika.

Hii ratio ipo katika Waraka wa Uchaguzi wa Shura ya Maimamu wa Tanzania uliotolewa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Umesema kuwa mimi nimekoshwa na hatua ya serikali ya kutaka kujua dini na kabila.

Kwa kauli yako hii nachukulia kuwa jambo hili limekuudhi na ningependa kufahamu kwa nini hulipendi?

Unaweza kusoma waraka wa Shura ya Maimamu hapo chini:
Asante Sheikh zmohamed,japo uzi wa shura ya uramaa umefungwa na moderators.
 
Hii takwimu sio ngeni, umeamua tu kuleta taharuki. Takwimu hizi zipo karibu kila sehemu kwenye nchi hii.
 
Swali la kuulizwa dini yako linaulizwa sehemu nyingi kama vile hospitalini, mahakamani, polisi n. k
Kwa nini iwe nongwa kuulizwa wakati wa ajira?

Serikali lazima iwe na data ili kuweza kudhibiti ubaguzi katika ajira
 
Back
Top Bottom