Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Napata taabu kuamini kama hili suala ni kweli, na kama ni kweli basi aliye-propose na kulipitisha wote ni viumbe wapumbavu kupita maelezo! Na kama SSH analifahamu hili, na anaacha liendelee, basi nitamdharau sana kwa sababu ni jambo ambalo haliwezi kuwa justified kwa tafsiri yoyote ile!!

I wish hii thread nisingeiona mapema kwa sababu imeniharibia mood sana!
Chige,
Soma hayo hapo chini:

Hotuba ya Mwalimu Nyerere tarehe 10 Desemba, 1962 katika Bunge wakati Tanganyika inakua jamuhuri.

Hotuba ya Nyerere ilijikita kwenye matatizo ya upogo kati ya Waislam na Wakristo.

Hakuna njia nyepesi ya kuondoa tafauti baina ya raia wetu Waafrika na wasio Waafrika; hakuna njia nyepesi ya kuondoa tofauti za elimu kati ya Wakristo na Waislam, au baina ya wachache wenye elimu na wengi wa watu wetu wasio kuwa na elimu; hakuna njia nyepesi ambayo Wamasai na Wagogo wanaweza wakalingana na Wahaya na Wachagga na Wanyakyusa.

Hii ilikuwa kauli ya serikali ya kudhihirisha nia yake njema.

Kauli hii ilikuwa ya kuwapa matumaini na kuwahakikishia Waislam na wale wote walioathirika na dhulma ya wakoloni, kuwa serikali ilikuwa inatambua shida zao na itachukua hatua zifaazo kurekebisha hali hiyo.

Tarehe 5 Novemba, 1985 kabla hajastaafu urais, Nyerere aliwahutubia wazee wa Dar es Salaam.

Hotuba hii ilijaa simanzi, Nyerere akikumbuka jinsi Waislam walivyompokea Dar es Salaam kwa mapenzi makubwa ingawa yeye alikuwa Mkristo.

Wazee hawa wengi wao walikuwa wanachama wa zamani wa TANU waliomuunga mkono Nyerere wakati wa kudai uhuru.

Nyerere aliusifia mchango wa Waislam katika kipindi kile kigumu cha kudai uhuru.

Nyerere alisema kuwa upogo katika elimu uliorithiwa na serikali yake kutoka kwa Waingereza baina ya Waislam na Wakristo yeye ameuondosha katika kipindi cha utawala wake:

''Waislam wametupa nafasi kupitia sera yetu ya elimu, kurekebisha upogo.

Sasa nipo katika hali ya kufarahisha kwa kuwa wakati mwingine sielewi kama Mbunge mpya, Waziri, au Katibu Mkuu katika wizara zetu za serikali, ni Muislam au Mkristo au hana dini labda pale jina lake la kwanza linapotoa utambulisho.

Na hata hivyo hiyo siyo njia ya kuaminika kutoa utambulisho wa dini kwa kuwa tuna Wakristo wenye majina ya Kiislam, na Waislam wenye majina ya Kikristo.

Kuvumiliana huku nyie ndiyo sababu; nilichofanya mimi ni kuzungumzia maadili haya kwa niaba yenu.''

Ni muhimu sana mtu anapotaka kujadili tatizo hili akaangalia historia yake kwanza kabla hajaandika.

Bwana Chige,
Tatizo hili nimelijadili kwa kirefu sana katika kitabu cha Abdul Sykes.
Tatizo hili si tatizo la kupuuzwa na wala halikuanzwa na Rais Samia hivi leo.

Tatizo hili lilianza mwaka wa 1958 na likasababisha ugomvi mkubwa baina ya Sheikh Suleiman Takadir na Julius Nyerere na Sheikh Suleiman Takadir akafukuzwa TANU.


1643170760953.png

Baraza la Wazee wa TANU chini ya Mwenyekiti Sheikh Suleiman Takadir 1957.

1643170590909.png
 
Nchi yetu itajengwa kwa nguvu za pamoja, kwa kushirikiana sisi sote kwa pamoja.

Ukifanya Utafiti mdogo tu kwenye taasisi/idara zote za Serikali utabaini kuwa dini moja imehodhi zaidi kuliko dini nyingine au wasio na dini!! wakati wapo na wanasifa ila kwa maksudi tu wanatengwa au kusahauliwa.

kwakweli mimi ni mkristu nasema kweli kwamba UWIANO wa Dini zote ktk kuendesha nchi ni jambo la Muhimu sana haswa kwenye karne hizi.

Huwezi kujaza watu wa aina moja kwenye kila idara za serikali halafu wengine wametengwa kama vile sio watanzania sio sahihi.

Dini ya mtu sio sifa ya kumpa nafasi ila Sifa za Elimu na uzoefu wake ndio kigezo cha kuzingatiwa, ila kwa karne hii iliyo jaa wasomi wa Dini zote na wazoefu huwezi kuniambia kuwa watu wa dini fulani eti hawajasoma!! hii ni kauli iliyotumika sana miongo iliyo pita na kundi moja kujikuta lina hodhi ktk Idara zote huku jingine likibaki nje ya mfumo!!

Tukumbuke pia Historia inatuonyesha kuwa hata uhuru wa Nchi yetu umepiganiwa na kuletwa na watu wa Dini zote na Hayati J.K Nyerere akapewa kijiti cha kuliongoza Taifa letu.

Ili tujenge Taifa imara na lenye nguvu lazima kuwe na Uwiano sawa katika idara zote za serikali, Haipendezi kuona kwa mfano ndugu zetu waislamu wanalalamika kila miaka kuwa wao wametengwa kwenye kuitumikia Serikali yao halafu uongozi ukae kimya kama vile hawaoni sio sawa.
Endapo wanasifa wapewe nafasi sawa na wengine ktk kulijenga Taifa lao.

Taifa lenye nguvu litajengwa kwa kushirikiana sisi sote.

Nasema kazi iendeleee.................
Rais wetu anajenga Taifa lenye Haki sawa.
 
Habari wana JF ..

Mimi niliahidi sitamkosoa Rais Samia, kwa sababu nilishawakosoa sana ma Rais wa nchi hii hadi nachoka; lakini Kuna mambo ni mazito huwezi hata kufikiri yanaweza kufanyika kwa karne hii.

Mimi niwaombe Serikali, niwaombe CCM, niwaombe washauri wa Rais, kama mmechoka, mtuachie hili Taifa.
Wengine bado tunataka kuliona Taifa letu likiwa moja.

Vyombo vya usalama, basi mshaurini mheshimiwa Rais vizuri, msijisahau sana mkaiacha nchi kwenye auto-pilot.
Niwakumbusheni Taifa hili halikujengwa kwa matofali, la hasha!
Mpitisheni Mh. Rais katika historia ndogo ndogo zile njema, zilizotufanya Watanzania japo tukawa wamoja, potelea pote na umaskini wetu.

Sasa hamuwezi amini, leo hii Hazina inaomba taarifa za watumishi (CV), na miongoni mwa taarifa wanazotakiwa kujaza hao watumishi ni:-
1. Kabila lako .....
2. Dini yako .......

Zipo taarifa zingine, za kipuuzi zinazoombwa, ila haina haja sana kuzitaja, kwani hazina athari sana kama hizi mbili.

Hivi kweli, leo mnataka DINI ya mtumishi, iwasaidie nini?
Hii taarifa mnaitumia kuboresha nini?
Udini wa nini katika Tz ya leo.
Tuna ajenda gani na Dini za watu, (watumishi). DINI, DINI.....DINI...!!!!?....,leo tunauliza DINI yako ni ipi? Kweli mh. Rais Samia.

Halafu mnataka na KABILA, kabila la mtumishi litumike kuboresha nini?
Mna ajenda gani huko?
KABILA, leo mnamuuliza mtu KABILA... Kweli mh Rais Samia , ulisema wewe huna kabila, sijui ni Mzanzibar, sasa hawa watumishi, karne ya 21, mwaka 2022, wawajazie makabila yao, muyajue, myafanyie nini?!

Mh Rais Samia, hebu kataa mambo mengine.
Siku Taifa hili likiparaganyika mikononi mwako, hao unaowaona, watakukataa.

Mfumo wa CV (format) na taarifa zinazotakiwa nimeambatanisha hapa.
denooJ , MTAZAMO , barafu , Tindo , Chige , shige2 , Malcolm X5 , MALCOM LUMUMBA ,

View attachment 2095758
Huwa unasifia kiiiilaa kitu!Endelea kusifu,guniooo!😝😝😝😝😝
 
Sasa serikali yako ikijua dini yako na kabila lako Kuna UBAYA!?
mbona hauulizi kwanini mnaambiwa muandike majina yenu?
Katiba inatamka wazi kabisa kuwa serikali haina dini

Sasa inataka kujua dini ya nini? ni kuvunja katiba ya nchi
 
Kwani serikali inafanya matambiko? Serikali inaswalisha? Kuna kitu gani cha kiimani au kikabila serikali inafanya kwenye hizo dharula?
Haya maswali umeyafkiria vyema?

Umeambiwa ni muhimu serikali kujua ili kuweza kutoa huduma kwa watumishi wake accordingly pale inapobidi.
 
Napenda wapinzani wa mama wanavyotiriruka kwa mgongo wa uzalendo na kuchukia kitendo hiki. CV ni nini? CV ni taarifa za kina na uhakika za mtu na kipawa chake toka azaliwe. CV lazima iseme kabila na dini na hivi ni vitu natural,vinawezaje kukosa katika kumjua mtu?. Mm mwajjili nikijua watumishi wangu hawa ni dini moja au mchanganyiko itanirahisisha hata kuwa manage. Mfano waisilamu kujua mda wao wa ibada na wakristo na kama mm mkristo basi hata wadudu naweza kuagiza tu hadi ofisini tena naagiza kabisa ikauke kama ya mbuzi. Acheni kujifanya mnajua zaidi ya serikali ambayo inania njema na watu wake
 
Du aisee Lakini, kabla ya mama ukabila na udini bado ulikuwepo , ila kimya kimya , hasa Hawa wachaga na wasukuma na ndugu Yao jiwe ameleta sana udini, Kuna siku nasoma CV ya msukuma mmoja, nakuta kaweka kabila lake kwenye CV, ila nilikuwa kuona matokeo yake baada ya yeye kupata kazi na Mimi kukosa.
Mke na mume wameomba pasipoti pamoja, mke ni msukuma na mume ni muha wa kigoma.

Mke hakutakiwa approve chochote kile na pasipoti iitoka ndani ya wiki mbili. Mume alitakiwa approve mambo lukuki japokuwa baba yake anayo asipoti, Immigration officers walifika mpaka kuongea na baba wa mume kumuuliza baadhi ya maswali kuhusu mji wa kigoma na asili ya ukoo wao.

Hatari sana mkuu, hiyo ilikuwa kabla ya Rais Magufuli kufariki
 
Mimi Bora wale rushwa watakavyo, ila wasiguse kabisa hii misingi midogo midogo inayofanya tuendelee kujiona wamoja.

Naumia siwezi hata kuelezea.
Hii issue ni sensitive! Ila wewe, mimi na yeye, tuna juwa kwamba Lilihitaji nani amfunge paka kengele! Bila hivyo hakuna uwiano wa kuridhisha! Kuna makundi yamekuwa ya kila makombo ya keki ya Taifa wakati mengine yana bwia keki nzima. Let's be realistic /honest.
 
Tuliza wenge... Acha kazi tupate kazi.
Pumbavu wewe. Unaweza kufanya kazi gani katika nchi yenye utashi wa kuzingatia dini na ukabila? Una akili kweli wewe? Hujui hata histori ya dunia, na kwa nini dunia iemkuwa iki admire our communal togetherness regardless our poverty? Msittake Tz kuwa kchwa cha mwenda wazimu, kila mtu anafanya majaribio ya iq yake. Nchi hii ina misingi. Na kama ninyi ndio meglikuwa waasisi wa taifa hili, pengine leo hii tusingekuwa tofauti ya nchi zinazopigana vita vya kikabila ama kidini.

Usitake kuuawa kwa taifa eti upate kazi. Huu ni upumbavu na kuifanya nchi ya madenge. Humvumiliki. Tunavumlia mengi sana kwa sababu tenaenzi misingi ya taifa. Watz wangelikuwa na akili kama zenu, bila wasiothamini nguzo za taifa, bila shaka kingeliwaka zamani.

Naona kama tumevamiwa. TISS mnafanya mambo makubwa. Lakini tafadhali lindeni taifa letu.
 
Huu ni upumbavu na hatari kubwa!

Serikali inataka kujenga makanisa na misikiti? Serikali inataka kutengeneza taratibu za kufanya matambiko?

Mwalimu must be rolling in his grave!
Sio lazima kuja dini, unaweka kuweka deshi.
 
Kuanzia 2015 hadi march 17 2020 Askari polisi 89% Walitoka Mara na Arusha na OCD wote walikuwa wenye asili ya familia za kifugaji na wafugaji walisumbua sana wakulima. Kuna vitu havikuwa sawa ila labda kwa upande wako vilikuwa sawa. Hivyo hivyo this time things go ant clockwise
 
Tulizeni mishono dawa iwaangie, tuhuma za udini na ukabila kwenye taasisi za sirikali zimekithirini sana, sasa mama anachunguza je ni kweli ama laa? Hakuna ubaya kuchunguza tuhuma nzito kama hizo ,
Kama mbwai mbwai tu , lakini lazma tuchunguze na kuleta uwiano sawa kwenye sirikali, sio dini fulani au kabila moja mkurugenz hadi mfagiaji.
Keki ya taifa lazma watu wote wapate . Haki na usawa
Sio lazima kujaza dini, huwezi kulazimishwa kujaza ukiweka deshi.
 
Back
Top Bottom