Unashindwa kuelewa hawa either ni wapinzani au ile kitchencabinet iliyoachwa na huwa wanatafuta kila upenyo kui discredit serikali ili Rais aonekane hafai,,Boss sio kweli mm wakati naanza ajira kuna kipengele kwenye mkataba wangu ajira za serikali kinauliza dini.Hili jambo sio jipya nashangaa kuona mleta mada analikuza kana kwamba limekuja leo.Au kwakuwa kwenye ajira za serikali ni mgeni.
Wanaoenda kufanya ibada ijuma inabidi wafidie huo muda Jumamosi au Jumapili.Inawezekana ikaileweka vibaya kwasababu tayar Kuna mitizamo tofauti juu ya Kiongozi mkuu.
Ila hili jambo lipo na lilikuwepo kwa watumishi. Kuna muda watu walihoji na majibu yalionyesha ni kwa nia njema, Mfano mtumishi anapofariki zipo taratibu za kumhifadhi kiimani kabla ndugu zake hawajapatikana au kufika eneo husika, lakini pia kulikuwepo na mgongano wa nyakat za ibada hasa kwa Wasabato na Waislam.
Kuna maeneo ijumaa hawana break kabisa kwakuwa idadi kubwa ya wakaazi ni Wakristo kwahiyo hili la kuwatambua inaeezekana halina sura ya udini au ukabila.
Kama uliwahi kumsikiliza Nyerere (1960 - Marekani), tulipo pata uhuru 1961 yaliongezeka makabila mapya! Wahindi, waarabu na wazungu. Hivyo kama wewe ni Mhindi, usihofu wewe ni mtanzania kama Mjita alivyo.Ndio hali imefikia hapo
Nakushauri andika wewe unatokea Zanzibar na dini yako ni mkojani
Hapo sisi wahindi itakuaje sasa na ni watanzania
Jumamosi ni siku ya mapumziko kwa serikaliNi demographics, kama ni msabato utapewa ruhusa jumamosi
Kelele hizi za dini sio bure lazima zinagusa maisha ya watu direct ndio maana mayowe mengi. Hizo taarifa hazina effects zozote kwa anayetoa kwani hataachishwa kazi kwa kuwa dini au kabila fulani. Uzuri wake serikali inapotoa ajira CV yake haina kipengele hicho ila ukishapata kazi ndipo utatakiwa kutoa taarifa hizo.Sio lazima kujaza dini, huwezi kulazimishwa kujaza ukiweka deshi.
Serikali haina dini wala kabila, ila watu wake wana dini na makabila...
Hata nyumba ya wageni unaulizwa hayo maswali ya dini yako na kabila lako.Mbona uliingia MAHABUSU unaulizwa hayo maswali tatizo lipo wapi?
Bado hakuna justification yoyote hapo. Kuna mambo ni ya kitaifa au ya kibinaadamu zaidi kuliko keep kabila. Hicho mnachoita "tabia za kikabila" ni matokeo ya kimazingira zaidi na wala siyo genes hivyo huathiriwa zaidi na mazingira anayoishi kuliko kabila lake. Haya ni miongoni mwa masalia ya ukoloni kama yale ya binaadam alikuwa nyani. Hizi ni sawa na stori za kuamini eti kuna makabila ni malaya kuliko mengine: siyo kweli. Much as satisfaction level au sababu za sex almost sawa, ni mazingira tu aliyoishi mtu ndiyo hutoa tafsiri ya jambo flani litendeke vipi au alipe value gani kiasi mtu huyo akiishi mazingira mengine tabia hiyo hubadilika. Infact, kuendelea kuwepo kwa vijitabia vya hovyo vinavyonasibishwa na ukabila ni matokeo ya elimu mbovu inayoshindwa kuleta "convergence" kwenye hayo mambo ya msingi. Mhehe aliyezaliwa au aliyeishi na kusomea Texas definitely hatakuwa sawa na mhehe aliyeishi huko Mufindi. Then essence ya kabila kwenye tabia inatoka wapi hapa!
Mfano mwingine, jamii inamuona mmasai kama ni mtu mshamba, duni, anayefaa kuishi porini tu na mifugo yake. Is that true? Je hakuna wamasai wengine ambao kwa kupata Elimu, au exposure au kuishi na jamii/ mazingira mengine wamekuwa tofauti na mfumo wa asili waliouzoea.
Ukabila ni jambo ambalo halina afya yoyote na popote kwenye society ya Tamzania au jamii iliyostaarabika.
Kwanza nashangaa, kwani mtu anapoajiriwa si details zote hizi anatoa kwa mwajiri wake. Ina maana MOF walikuwa wanafanya kazi na watu ambao hawajui siku zote hizi. Unamwuliza mwajiri wako jina lako, wewe ulikuwa unamlipa nani mshahara?ila wachaga mnapata tabu sana, anyway logeni ccm itoke madarakani ndio itakua nafuu kwenu
Kwenye kumbukumbu za ajira,kabila,dini ni viyu vya kawaida tu hata enzi za nyerere sharti hili lilikuwepoHabari wana JF ..
Mimi niliahidi sitamkosoa Rais Samia, kwa sababu nilishawakosoa sana ma Rais wa nchi hii hadi nachoka; lakini Kuna mambo ni mazito huwezi hata kufikiri yanaweza kufanyika kwa karne hii.
Mimi niwaombe Serikali, niwaombe CCM, niwaombe washauri wa Rais, kama mmechoka, mtuachie hili Taifa.
Wengine bado tunataka kuliona Taifa letu likiwa moja.
Vyombo vya usalama, basi mshaurini mheshimiwa Rais vizuri, msijisahau sana mkaiacha nchi kwenye auto-pilot.
Niwakumbusheni Taifa hili halikujengwa kwa matofali, la hasha!
Mpitisheni Mh. Rais katika historia ndogo ndogo zile njema, zilizotufanya Watanzania japo tukawa wamoja, potelea pote na umaskini wetu.
Sasa hamuwezi amini, leo hii Hazina inaomba taarifa za watumishi (CV), na miongoni mwa taarifa wanazotakiwa kujaza hao watumishi ni:-
1. Kabila lako .....
2. Dini yako .......
Zipo taarifa zingine, za kipuuzi zinazoombwa, ila haina haja sana kuzitaja, kwani hazina athari sana kama hizi mbili.
Hivi kweli, leo mnataka DINI ya mtumishi, iwasaidie nini?
Hii taarifa mnaitumia kuboresha nini?
Udini wa nini katika Tz ya leo.
Tuna ajenda gani na Dini za watu, (watumishi). DINI, DINI.....DINI...!!!!?....,leo tunauliza DINI yako ni ipi? Kweli mh. Rais Samia.
Halafu mnataka na KABILA, kabila la mtumishi litumike kuboresha nini?
Mna ajenda gani huko?
KABILA, leo mnamuuliza mtu KABILA. Kweli mh Rais Samia , ulisema wewe huna kabila, sijui ni Mzanzibar, sasa hawa watumishi, karne ya 21, mwaka 2022, wawajazie makabila yao, muyajue, myafanyie nini?!
Mh Rais Samia, hebu kataa mambo mengine.
Siku Taifa hili likiparaganyika mikononi mwako, hao unaowaona, watakukataa.
Mfumo wa CV (format) na taarifa zinazotakiwa nimeambatanisha hapa.
denooJ , MTAZAMO , barafu , Tindo , Chige , shige2 , Malcolm X5 , MALCOM LUMUMBA ,
View attachment 2095758
Kama ndio hivi hatuna rais hapa..haya masuala ya ukabila na udini..hayana maana..uwiano apeleke huko mchamba wima.
Mind you katika dunia hii superiority huwezi ikwepa ndani ya jamii...mana kuna wajanja na vilaza tu hata ufanyeje.
#MaendeleoHayanaChama
Sio lazima kujaza dini kwenye hiyo CV, hauwezi kufanywa chochote kwa kutokua na dini. Pia watu wengi tu wanaishi pamoja na wakiwa na familia bila kuoana na zipo ndoa za kiserikali ambazo sio lazima kuwa na dini.Kelele hizi za dini sio bure lazima zinagusa maisha ya watu direct ndio maana mayowe mengi. Hizo taarifa hazina effects zozote kwa anayetoa kwani hataachishwa kazi kwa kuwa dini au kabila fulani. Uzuri wake serikali inapotoa ajira CV yake haina kipengele hicho ila ukishapata kazi ndipo utatakiwa kutoa taarifa hizo.
Mnajifanya dini na kabila sio msingi wa maisha kwako na wakati leo hii ukitaka kuoa au kuolewa lazima familia kwabza watake kujua dini then kabila. Udini na Ukabila ndio vitu vya kila siku katika maisha yetu ba hadi tunataniana humo humo. Serikali inapofanya kazi yake tena kwa umakini kama hii usiingiliwe lazivyo hata JF hii itafungwa permanently kwa kuwa inakiuka masharti na malengo ya kuanzishwa kwake. Kama humu wakenya mmezidi kwa mgongo wa CHADEMA semeni tujuwe moja, inakera na kusikitisha kwa namna mnavyomshambulia mama utadhani ni hambazi au mpiga dili fulani. Kama hamuuoni usafi wake basi mpotezeeni tu
Hii haiko sawa mfano kuna kasi kubwa vijana wengi kuoa au kuolea na makabila mengine. Ni vema tutengeneze kabila liitwalo mtanzania.Habari wana JF ..