KERO Watumishi Wapya Halmashauri ya Wilaya ya CHATO - GEITA bado hatujalipwa kabisa Fedha za kujikimu

KERO Watumishi Wapya Halmashauri ya Wilaya ya CHATO - GEITA bado hatujalipwa kabisa Fedha za kujikimu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Idara ya Maendeleo ya Jamii, bado hatujalipwa kabisa Fedha za kujikimu hadi sasa katika kipindi cha miaka mingi sana. Tangu tumeajiriwa mwaka 2023, mwaka 2024, mwaka 2025, na mwaka huu 2026.

KERO, yetu ni hiyo yaani kila muda tunaulizia, wanasema andikeni barua... Ukweli ni kwamba Barua tumeshaandika nyingi sana na hatujawahi kulipwa kabisa hizo Fedha tunapitia changamoto.

Jambo lingine yaani wakiona kuna Ukaguzi au kuna Kiongozi mkubwa anakuja eneo karibu na Halmashauri ya Wilaya ya CHATO wanatowa taarifa watumishi wote wanaodai Fedha za Kujikimu andikeni Barua tunaandika lakini, hakuna Malipo yeyote.

Tunaomba utusaidie kuripoti katika Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri mkuu, Ofisi ya TAMISEMI na Mamlaka zingine husika.
 
Back
Top Bottom