Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,587
Unakuta mtumishi wa serikali anaingia kazini saa 2 asubuhi. Saa 3 anatoka kwenda mtaani kutafuta chai...anarudi ofisini saa 5 au 6 mchana. Anavuta muda ikifika saa 7 mchana anatoka kwenda kutafuta chakula cha mchana. Anarudi saa 8 mchana. Saa 9 huyo anaondoka zake.
Ni watumishi wengi sana wa Umma wana hii ratiba kila siku, kila wiki, mwezi na miaka kadhaa... Cha ajabu mwisho wa mwezi mshahara unaingia.
Viwango vya mishahara na faida au output ya mtumishi wa Umma havilingani kabisa. Mtu anaweza kukaa miaka 3 hadi 5 au 10 hajawahi kufanya kazi yoyote kabisa. Lakini unamkuta kachomekea, kaulamba mkanda nje.
Halafu unakuta mtu ana elimu nzuri kabisa.
Hii nchi dah.