Watumishi wengi wa serikali mnatia huruma mno, ni katikati ya mwezi ila nimepokea zaidi ya simu 10 mkiomba msaada wa pesa

Watumishi wengi wa serikali mnatia huruma mno, ni katikati ya mwezi ila nimepokea zaidi ya simu 10 mkiomba msaada wa pesa

nyboma

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2021
Posts
2,308
Reaction score
7,366
Ni watumishi wa serikali kutoka idara tofouti tofouti nyeti na zisizo nyeti, watumishi hawa wa Mama Samiah Suluhu Hassani wanatia huruma mno kila ifikapo katikati ya mwezi.

Na kwa hili ilivyo kwa sasa ya vitu kupanda bei, kuna kufanya maendeleo kweli ukiwa mtumishi wa serikali?

Niwaase watumishi, pindi mnapopata mishahara yenu muache kutumia hovyo kwenye mabaa na kuhonga wanawake hovyo pasipo kufanya seaving ya 40% ya kile unachopata mwisho wa mwezi, maana kwa simu za leo nimejisikia vibaya mno na mwisho nimeshindwa kuwaelewa? Kama hiyo mishahara mnayolipwa inawatosha kweli au ni vile mmeridhika na maisha ya mishahara kwamba mna uhakika wa kuupata kila mwisho wa mwezi, na imewapelekea nyie kubweteka pasipo kufikiria kuwa na kitu cha ziada cha kuwaingizia kipato?

Ushauri kwenu mjitahidi kubadilika muishi kulingana na kipato chenu, hizi starehe mnazofanya mjini mkumbuke zina mwisho mbaya mtakuja kukumbuka umri umewatupa mkono na hakuna cha maana mlichofanya pindi mkiwa watumishi.

Mwisho kabisa niwapingeze waalimu, katika watumishi wa serikali hawa wanaongoza kuishi ndani ya mishahara yao, sijawahi kuwasikia wakililia shida kama watumishi wengine, popote mlipo walimu pokeeni pongezi zangu za dhati.
 
Daaah!! Sawa bwana we tusimange tu.
Sijawasema kwa ubaya huwa nawasaidia sana, sena leo simu zimekuwa nyingi sana sijui huwa wanaambiana kwamba fulani ukimtafuta atakusaidia.

Pia kuna watumishi wengine sio waaminifu kuna wakati unawaazima kwa moyo mmoja ila mwisho wa siku kurudisha deni inakuwa shida.

Hivyo nimeweka azimio ya kwamba sitowakopesha pesa nyingi tena.
 
Labda watumishi wa local government a.k.a tamisemi.
Sisi ambao tuna posho zaidi ya moja na asante za hapa na pale hatujakupigia simu ndugu acha uongo
Mkuu kuna watu wako taasisi fulani fulani huwa wanaposho nzuri na safari nyingi tu ila ndio hao wananipigia simu kuomba msaada.

Pongezi kwako kwa kufanya kazi kwenye mamlaka, jitahidi sana kufanya saving hawa vijana na maisha yao ya mjini wasikuhadae kabisa
 
Mkuu kuna watu wako taasisi fulani fulani huwa wanaposho nzuri na safari nyingi tu ila ndio hao wananipigia simu kuomba msaada.

Pongezi kwako kwa kufanya kazi kwenye mamlaka, jitahidi sana kufanya saving hawa vijana na maisha yao ya mjini wasikuhadae kabisa
Ngono + pombe= mauti
Mlevi hata umlipe million 2 bado ataendelea kuwa mhitaji tu.
 
Ngono + pombe= mauti
Mlevi hata umlipe million 2 bado ataendelea kuwa mhitaji tu.
Vijana wanatia huruma mno, unakuta kijana anapokea zaidi ya 2M posho humo humo ila katikati ya mwezi hana kitu na hapo wiki mbili alikuwa anakunywa pombe za laki 7 kwenye lounge huku akizungukwa na wanawake wa mjini.

Wanasikitisha sana
 
Yule wifi yetu wa Ulaya nae anaomba?
Yule yuko sehemu nzuri, pia mme wake ana pesa sidhani hata kama anagusa mshahara wake. Ila ni kawaida yenu kuhudumiwa hata kama mna kazi pesa yenu ni yenu tu haturuhusiwi kujua imeenda wapi?
 
Walimu tuna haiba ya ustaha na aibu kuombaomba lakini siyo kwamba hatuishiwi ni ile tu tunatumia kwa level yetu ya salary ndogo yenye kulengwa na machoz
Pongezi za dhati kutoka kwangu, mna nidhamu ya fedha sana pia ndoa nyingi ambazo zinahusisha mwalimu huwa zinadumu sana sijajua mna siri gani ya kipekee kiasi hicho?
 
Back
Top Bottom