Kuna maswali machache.
1. Hao watumishi walikuwa wameajiriwa wakijulikana kwamba hiyondiyo elimu yao au ni watu ambao walijifanya kuwa na elimu zaidi? Kama walijulikana, mkataba wao na serikali ulitambua elimu yao hiyo kwamba inafaa kwa kazizao.
2.Elimu ni muhimu. Kujiendeleza kielimuni muhimu. Walipewa taarifa na nafasi za kujiendeleza?
3. Ni watumishiwa kazi gani? Kuna kazi nyingine hazihitaji kisomo sana zaidi ya kujua kusoma na kuandika.Je, kuwaondoa watu wenye kisomo cha chini kunaangalia vigezo gani? Mfagizi wa ofisi hahitajikujua calculus kuweza kufagia.
4. Inakuwaje mtumishi halali aondolewe kazini bila kulipwa mshahara?
5. Wamelipwa mafao yao?