Waumini wa FGBF wampa zawadi ya nyumba Askofu Kakobe na Mkewe

Supportive document ni muhimu sana, hapo nimeona picha ya funguo tuu itapendeza tukipata na picha ya nyumba yenyewe ambayo baba wa kiroho amezawadiwa na waumini wake.
 
Uhuni wa hawa viongozi wa dini(sio Kakobe pekee yake) ni kwamba wamepindua maandiko kichwa chini miguu juu.

Wakati wa Bwana Yesu, wanyonge ndio walikuwa wanahudumiwa. Ila wakati huu wanyonge ndio wanawahudumia watumishi. (Wakati ule Bwana alilisha watu wenye njaa elfu tano....siku hizi wenye njaa elfu tano wanamhudumia mtu mmoja aliyeshiba)

Hizo Bilion nane alizokutwa nazo, alikuwa amezilundika za nini wakati nina hakika ndani ya waumini wake kuna wenye uhitaji mkubwa wa chakula, matibabu, malazi hata elimu kwa watoto.

Angetoa kiasi (hata bilioni moja tu)na kuwajali waumini wake kwenye mahitaji yao angekuwa ametenda alichotenda Bwana Yesu.

Huo ndio Usanii unaozungumziwa hapa.
 
Billion 8 za nn kwenye account ya mtumishi wa Mungu while makanisa ya Full Gospel mengi mikoani hayajasakafiwa, achilia mbali wachungaji wasio hata na makazi.
Eehee! Ila Waumini wakitaka nyumba na mali,anawaombea kwa Mungu,maana ndio mtoa vyote
 
Uko sahihi
 
Billion 8 za nn kwenye account ya mtumishi wa Mungu while makanisa ya Full Gospel mengi mikoani hayajasakafiwa, achilia mbali wachungaji wasio hata na makazi.
wachache wanafaidi jasho la walipa tenth. Na hao wanaolipa fungu la 10 wengi ni maskini hoe hae.
 
wachache wanafaidi jasho la walipa tenth. Na hao wanaolipa fungu la 10 wengi ni maskini hoe hae.
Halafu imekuwa fashion siku hizi kila mchungaji anawaza kuishi kwenye ghorofa na kuendesha V8 bila kuangalia hali za kiuchumi cha waumini. Lakini kibaya zaidi kazi ya Mungu haifanyiki kwa kiwango cha miaka ile ya kina Moses Kulola at the expense of kuwatajirisha watumishi. Watu wapo tayari kumchangia mchungaji gari lakini mwaka mzima wasifanye mkutano wa injili.
 
Hiyo nyumba nadhan naijua. Ni kasri kubwa balaa.

Ipo junctiin ya rainbow mbezi chini, next to GBP petrol station.

Hiyo kighorofa ni balaa kubwa. Jioni nitakipiga kapicha aisee
Teh teh ile ni yke mwenyewe
Kataka ionekane kama kajengewa kmbe watu kitambo wanajua

Ova
 
Hiyo nyumba nadhan naijua. Ni kasri kubwa balaa.

Ipo junctiin ya rainbow mbezi chini, next to GBP petrol station.

Hiyo kighorofa ni balaa kubwa. Jioni nitakipiga kapicha aisee
tuwekee hapa tuone. Na siyo kuwa ni waumini, no ni pesa anazopiga waumini, sasa kuepuka maswali, ........ wamenijengea waumini. JANJA YA NYANI
 
Waumini wake wamenyong'onyeaaaa kama wanaumwa.

Wako full radicalized aisee.

Katika maisha haya kuna vitu ni underated sana.

Uhuru wa fikra ( hasa ukidhibiti njaa ), Utu, na

Kujitegemea kimawazo
Ipo siku atawafungia mle kwenye lile banda lake halafu awalishe moto wa petrol
 
Teh teh ile ni yke mwenyewe
Kataka ionekane kama kajengewa kmbe watu kitambo wanajua

Ova

Watanzania wanamsubiri Mtu akifariki ndio waeleze mazuri yake ! Huu utamaduni ubadilike katika Jina la Yesu.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…