Waumini wa Kanisa la Gwajima wafanya maombi na Ibada nje ya Kanisa hilo Ubungo

Waumini wa Kanisa la Gwajima wafanya maombi na Ibada nje ya Kanisa hilo Ubungo

Washauri wa Sa100 wamemuingiza Chaka wao ndio waliomuondolea Kigali alichokuwa nacho kwa wanachi.Matendo maovu wanafanya wao ila mama yao ndio anayoyabeba haijalishi katoa oda au hajatoa oda
 
Baadhi Waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo Ubungo, Dar es Salaam ambalo limefungiwa na Serikali, wamejitokeza eneo la pembezo na Kanisa hilo wakiimba nyimbo mbalimbali za Dini.

Hata hivyo, wakati hayo yakiendelea Kanisa hilo limefungwa na limezungukwa na Askari Polisi waliovalia sare tangu siku ilipotolewa taarifa ya zuio la Kanisa hilo (Juni 2, 2025) linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima kuendelea kutoa huduma kwa kile kilichoelezwa kutoa matamshi ya Kisiasa yenye lengo la kuichonganisha Serikali na Wananchi.
Pia soma ~ Waumini wa Gwajima watakiwa kusalia nyumbani
Hapo undercover police wapo nao wanaimba na kurukaruka, nimewaona kama watatu hivi. Jichanganye.
 
Hv CCM mnafeli wapi mambo madogo hvyo, nchi hii hakikisha tu huku Kwa Simba na Yanga mambo yanaenda vizuri then kwenye dini huku hakikisha kunaenda vizuri. Huko kwingine hata uvurunde vipi watu hawana time nako
 
Hii dhambi ya kuwanyima watu Uhuru wa kuongea na Mungu wao haitowaacha salama, ni ishu ya muda tu! Wangetubu mapema
 
Sisi ndio SuperPower nchi hii #UkikaidiUtapigwa2
Bado vilio kusikika ndio mkileta upuuzi mtapigwa tu hakuna namna
Sawa sisi tunavumilia, ikifika zamu yenu tusisikie vilio. Maana huwa mnalia kwa sauti kubwa sana
 
Back
Top Bottom