Waumini wa kikristo mnafuata muongozo gani? Nijibu maswali haya

Kabla ya hoja zako. Tambua hata huo uislamu ulianzishwa na Wakatoliki. Madhehebu yote uyaonayo ni matawi ya ukatoliki. Ukatoliki ndio umeitunza Biblia na Ukristo.
Thus Quran imekopi zaburi, torat na injili toka kwenye Biblia.
 
Upo vizuri kwenye dini ungekuwa haujaolewa ningekupa zawadi ya kukuoa
 
Unataka kufananisha Biblia na vitabu vya hadithi?...
Unataka kufananisha maisha ya Kristo na mbakaji wa watoto wadogo?...

Endelea kumfata asiyejua aendako na wala hajui hukumu yake siku ya kiama.
 
Biblia ni nini?
Neno wa Mungu anaongea na watu wake, kizazi na kizazi.

Nabii gani aliyepokea hiyo biblia au kuletewa hiyo biblia
Siyo kitabu, ni uhusiano wa Mungu na wanadamu aliowaumba... kizazi na kizazi, tangu kuumbwa kwa dunia.

Injili ni kitabu cha wakina nani? Na yesu alitumwa kwa Mataifa mangapi ili akafikishe ujumbe?
Injili ni habari njema iliyoletwa na Masihi na Kristu - Mungu Mwana, Mungu nafsi ya pili, Mungu-mtu.

Yesu alisujudu , wewe mkristo unayedai unamfuata yesu kristo unasujudu? na kama husujudu unafuata nini kwa yesu alichokifanya?
Kumfuata Kristu ni kuishi amri kuu ya upendo.

Yesu alioa? Kama akuoa wewe mbona unaoa?
Kuna miito ya aina tatu:
  • Wito wa kwanza sote tumeitwa kuwa watakatifu
  • Wito wa utume - daraja takatifu, ndoa, maisha pekee (single life)
  • Wito wa huduma - kazi

Kristu aliamua kuishi useja kama wito wake wa utume.

Yesu akuvaa msalaba je, we mkristo unavaa msalaba Shingoni kwa andiko gani? Au kwa kumfuata nani?
Msalaba ni ishara ya upendo. Kwamba njia pekee ya kutufikisha mbinguni ni kuiuishi upendo.

Kipimo kikubwa cha upendo ni kuwa tayari kutoa maisha yetu kwa ajili ya wengine kama alivyofanya pale msalabani.

Huo ni Ukristu.

Kama unamashaka kuhusu Mtume Mohammad sio mtume wa mwisho na Qur'an sio katiba ya Mungu ili ikatuongoze Waanadamu, mbona unakubali zaburi na torati? Unakifahamu kilichoandikwa kwa torati na zaburi?
Usijifunze Biblia kwa kutumia Quran, ama vice versa. Usijifunze Ukristu kwa kutumia Uislam.
 
Yesu ndo kafanya watu wavae msalaba. Alisulubishwa msalabani.
Wanavaa ili kukumbuka mateso ya Yesu.
Imeandikwa katika Kutoka 20: 4
Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini ya dunia, Usivisujudie wala kuvitumikia, kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao na kizishika amri zangu.
 
Hakuna ulichojibu. Unajua maana ya kupata elimu usiogope kujifunza.
 
Achana nao, usibishane nao kwanza Yesu Kristo na Nabii Isa bin Maryam ni watu wawili tofauti.
 

Attachments

  • Screenshot_20230405-145844.png
    135.1 KB · Views: 3
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…