Waumini Wamzawadia gari mpya Askofu Mkuu Mstaafu wa KKKT Dkt. Shoo

Waumini Wamzawadia gari mpya Askofu Mkuu Mstaafu wa KKKT Dkt. Shoo

Sawa, hata huko kwa kaisari huwa wanafanya hivyo, tatizo sie wa chini tunaambiwa nendeni mkawe raia wema
 
Utofauti wa wale wa TEC na wengine huanzia hapa!

Hiyo pesa ni kubwa sana, kama wangejitolea hata kujenga shule au hospital na kuipa jina lake kwa heshima ya mchango wake katika kanisa, nadhani ingekuwa bora zaidi.

Hapo running cost ya hilo gari ( wese+ service) ni gharama, ambazo pengine waumini watalazimika kuwa sehemu ya wahudumiaji.
Msafari wa Bi Tozo magari ya aina hii yanakuwepo zaidi ya 20 hamjalalamika kodi zenu zinachezewa.

Waumini wameamua wenyewe kuchanga na kumzawadia mtumishi wao zawadi ya gari mnapiga yowe mlitaka wampe zawadi ya Vitz !.

Wakuu wa Mikoa,Makatibu tawala wa Mikoa,Mawaziri na Makatibu wakuu wote wanatumia hizi gari Land Cruise 300.

Watanganyika mpo kimya.Mwaka jana Bi Tozo kamzawadia Mzee Mwinyi Benz yenye gharama kubwa kuliko L/C 300 usisahau hizo ni kodi zetu ?.
 
Kwa kanisa katoliki hayo mambo ya kawaida tu Kuna padre mmoja katika mikoa ya nyanda za juu kusini anamiliki hyo chombo ikiwa ni metallic silver
 
Pumbavu.... Unafiki, , upuuzi...

Dini ni kivuli cha unafiki na uzandiki, nadhani huyo mzee wangempongeza tu kwa shukran pekee badala yake fedha za kununulia hilo gari la bei kubwa wangekusanya hizo pesa kusaidia wagonjwa na wahitaji mbalimbali nchini.

Ndio yale yale waumini wanakufa njaa kwa kuyatolea hayo matepeli(wachungaji) na kuaminishwa wataombewa na kubarikiwa na Mungu wakat huo huo hayo matapeli(wachungaji) yakipata shida yanataka kuchangiwa na fedha ked kede.


Ifike mahala watanzania waelewe hilo jambo japo linauma, ukiona humo hata walioshiriki hiyo ibada ni wapigaji+wanafiki watupu.

Note: kuna vichaa watasema nisiwapangie matumizi, hakuna cha kupangiwa wangetaka kumpa zawadi huyo tapeli basi wangetoa nje ya kanisa na kivuli cha dini.
Unawapangia watu matumizi ya hela zao na inakuuma kabisa? Huo ni upambavu wa hali ya juu
 
Pumbavu.... Unafiki, , upuuzi...

Dini ni kivuli cha unafiki na uzandiki, nadhani huyo mzee wangempongeza tu kwa shukran pekee badala yake fedha za kununulia hilo gari la bei kubwa wangekusanya hizo pesa kusaidia wagonjwa na wahitaji mbalimbali nchini.

Ndio yale yale waumini wanakufa njaa kwa kuyatolea hayo matepeli(wachungaji) na kuaminishwa wataombewa na kubarikiwa na Mungu wakat huo huo hayo matapeli(wachungaji) yakipata shida yanataka kuchangiwa na fedha ked kede.


Ifike mahala watanzania waelewe hilo jambo japo linauma, ukiona humo hata walioshiriki hiyo ibada ni wapigaji+wanafiki watupu.

Note: kuna vichaa watasema nisiwapangie matumizi, hakuna cha kupangiwa wangetaka kumpa zawadi huyo tapeli basi wangetoa nje ya kanisa na kivuli cha dini.
Acha makasiriko ndugu yangu, maisha sio magumu kihivyo.
 
Kumbuka Bishop Shoo kastaafu ukuu wa kanisa Tanzania lakini anaendelea na ukuu wa kanisa la Moshi, hivyo hitaji la usafiri madhubuti kutembelea familia ya Mungu katika miji, vijiji, vitongoji, mitaa na vichochoro vyote vya Kilimanjaro ni kubwa. Mnaosema amepewa zawadi na system kwa kuunga mkono dpw na kwa kuichagulia system "mtu wao" hamna hoja, tatizo wabongo hatuna jema, tumwache mzee afanye kazi zake za utume, anakula anakopeleka mboga, yaani anakowajibikia ndiko panapomtunza.
 
Muacheni Askofu anyooshe goti kwenye kiyoyozi mbona imekuwa nongwa.
 
1
Utofauti wa wale wa TEC na wengine huanzia hapa!

Hiyo pesa ni kubwa sana, kama wangejitolea hata kujenga shule au hospital na kuipa jina lake kwa heshima ya mchango wake katika kanisa, nadhani ingekuwa bora zaidi.

Hapo running cost ya hilo gari ( wese+ service) ni gharama, ambazo pengine waumini watalazimika kuwa sehemu ya wahudumiaji.
Moja ya sababu za TEc kuwa wakali ni hofu ya kupoteza eneo Lao karibu na bandari hasa kanisa la St. Joseph.

Ule mkataba wa milele unadai kwamba Mwekezaji akihitaji eneo lolote karibu na bandari kwa ajili ya kupanua serikali itahakikisha inampatia.

Ila wanajipanga kuhamia eneo jingine in case ikitokea hivyo.
 
Daaah waumini wanichangie na mm M 20 Mungu atawabariki
 
Diuuu ina maana ukute gari limetoka DPW sababu kanisa limewakubali....tunadanganywa ni waumini...kwa lipi hasa Askofu Shoo alichofanya kwenye kanisa au nchi kupewa gari hilo bei kubwa sana....? Muda utaongea .....tusubiri tusiache kuomba wale waombaji kazi ni hiyoo
Acheni zenu hizo! Chuki tu.

Mbona watu kama kina msukuma wanamiliki gari kama hizo na mnaona kawaida hamsemi. Muacheni askofu ale maisha na yeye. Kwanza afadhali hata Shoo huwa haogopi kukemea mambo.


Tutamnunulia Jet kabisa ili roho zenu zipasuke😀
 
Yesu alitembea ya mguu,na ilipobidi sana alipanda punda.Farasi ilikuwa ni anasa zama hizo,ila skuizi watumishi wanakula tu Bata......smooth.
Mkuu, kama Yesu angezaliwa zama zetu, pamoja na miujiza yake yote asingekubalika kwa hawa waabudu mali.
 

ASKOFU DKT. SHOO AKOSHWA NA UTENDAJI WA MBUNGE SAASHISHA, ASEMA ANAACHA ALAMA

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Dkt. Fedrick Shoo amesema kuwa wajibu mkubwa wa viongozi wa dini na wale wasio wa kidini kwa maana ya viongozi wa Serikali ni kuhakikisha kuwa wanatimiza yaliyo matakwa ya wanaowahudumia badala ya kujali maisha yao binafsi.

Askofu Dkt. Shoo ameyasema hayo wakati wa hafla ya kumstaafisha kwa heshima Mchungaji Anaeli Masawe ambapo amemtaja Mchungaji huyo kama mmoja wa watumishi waliosimama vyema katika maisha ya utumishi huku wakiutimiza vyema wajibu wao kwa kanisa na washarika.

"Mchungaji Masawe ulitumika ipasavyo na wakati mwingine kwa namna moja ama nyingine safari yako ya uchungaji ilikuwa na majaribu na uliweza kuyashinda kwa kumuamini Kristo, leo unastaafu kwa heshima na kwa umati huu na shangwe hii hakika ulitumika vyema" - Askofu Dkt. Shoo.

Katika hatua nyingine Askofu Shoo hakusita kugusia mambo ya kimaendeleo huku akimtaja Mbunge wa Jimbo la Hai, Mhe. Saashisha Mafuwe kuwa mzalendo katika kufanya kazi yenye kuacha alama na kuleta maendeleo katika jimbo hili.

"Namuona Mbunge wetu Saashisha Mafuwe tupo nae, hakika amefanya mengi na ambayo ni alama kwa Jimbo hili, tuzidi kumuombea afanye zaidi ili iwe alama kwa wananchi na jamii ya Hai" - Askofu Dkt. Shoo

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa zoezi la kustaafishwa Mchungaji Anaseli Masawe, Mbunge wa Jimbo la Hai, Mhe. Saashisha Mafuwe amesema kuwa ameelekeza nguvu kubwa katika kuwasikiliza wananchi na kutii kiu ya kuwaletea maendeleo huku akisema kuwa atahakikisha anashirikiana na makundi mbalimbali ili kufikia lengo hilo.

"Niseme ukweli najaribu kukaa na kila kundi katika Jimbo hili, iwe watoto, vijana, wazee, hata wale ambao wapo kwenye vijiwe najaribu kuwafikia ili nisikie maoni yao na niweze kuwahudumia. Sitopuuzia hata wazo la mtu mmoja kwa manufaa ya Jimbo letu" - Mhe. Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Hai

Ibada na hafla ya kumstaafisha Mchungaji Anaseli Masawe imefanyika katika usharika wa Hai Mjini na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kanisa na Serikali.
 

Attachments

  • SHOO7132.jpg
    SHOO7132.jpg
    508.1 KB · Views: 1
  • SHOO6826.jpg
    SHOO6826.jpg
    920 KB · Views: 1
  • SHOO6587.jpg
    SHOO6587.jpg
    1.1 MB · Views: 1
  • SHOO6402.jpg
    SHOO6402.jpg
    852.2 KB · Views: 1
  • SHOO6792.jpg
    SHOO6792.jpg
    295.5 KB · Views: 1
Itakuwa kwenye ununuzi wa ile gari alitoa kiasi kikubwa, hawa ndugu zangu nao kwenye maslahi hawapo nyuma
 

ASKOFU DKT. SHOO APEWA GARI JIPYA, MBUNGE SAASHISHA ASHIRIKI KATIKA HALFA YA KUKABIDHIWA GARI

Tukio la kukabidhiwa gari jipya aina ya Land Cruiser GR Sport kwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzaniani (KKKT) anayemaliza muda wake Dkt. Fredrick Shoo limewakutanisha viongozi mbalimbali wakiwemo wanasiasa na viongozia wa Serikali katika Jimbo la Hai.

Mbunge wa Jimbo la Hai, Mhe. Saashisha Mafuwe (CCM) na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ni miongoni mwa wageni walikwa waliofika kushuhudia tukio hilo la kihistoria katika Maisha ya Askofu Dkt. Shoo.

Askofu Dkt. Shoo amekabidhiwa gari hilo ikiwa ni ahadi iliyoanza kufanyiwa kazi baada ya mmoja wa waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheria (KKKT) kutoa wazo la ununuzi wa usafiri kwa Askofu Shoo wakati wa ibada ya shukrani ya Mchungaji, Dkt. Eliona Kimaro, Aprili 23, 2023.

Wazo hilo lilipokelewa kwa mwitikio mkubwa na baadae iliundwa kamati ya watu 60 wakiwemo wabunge, wanasiasa, wafanyabiashara na waumini wa madhehebu mbalimbali hatimaye Dkt Shoo amepata gari na kukabidhiwa zawadi hiyo nyumbani kwake Mailisita Moshi mkoani Kilimanjaro.

Aidha, katika halfa fupi ya kupongeza kwa chakula cha mchana, Askofu Dkt. Shoo alimkabidhi sehemu ya kidari cha Ndafu kama ishara ya kumpongeza kwa kazi yake nzuri aliyofanya katika Jimbo la Hai huku akimtaja kama kiongozi wa kuacha alama.
 

Attachments

  • SHOO6402.jpg
    SHOO6402.jpg
    852.2 KB · Views: 1
  • SHOO6784.jpg
    SHOO6784.jpg
    628.8 KB · Views: 1
  • SHOO7053.jpg
    SHOO7053.jpg
    489.3 KB · Views: 1
  • SHOO7013.jpg
    SHOO7013.jpg
    417 KB · Views: 1
  • SHOO7014.jpg
    SHOO7014.jpg
    536.6 KB · Views: 1
  • SHOO6668.jpg
    SHOO6668.jpg
    780.1 KB · Views: 1
  • SHOO6826.jpg
    SHOO6826.jpg
    920 KB · Views: 1
  • y2mate.com - GARI LA GHARAMA LAMSHANGAZA ASKOFUDKT SHOO_480p.mp4
    63.7 MB
Back
Top Bottom