Wauza chapati tuwape maua yao, wanatuokoa sana sisi mabachela

Hapa town kwa sasa kila kona hawa jamaa wapo, wanapika chapati nzuri na napenda sana namna wanavyo pika na kugeuza chapati kwa madoido.

Wanatuokoa sana sisi mabachelor, kwa 500/= tu unachukua chapati ya uhakika, sio zile za mama lishe ambazo ni nyepesi kama vitambaa.

Wanaofanya biashara hii wengi ni vijana wakiwa kama kundi, napenda ninunue kwao ili niwasapot katika biashara zao.

Big up sana kwa vijana wote walio ungana na kufanya hii biashara naamini inawalipa vizuri kwani wateja ni wengi sana kwa sasa.

Hapa nipo njiani narudi home na nitapita sehemu nipate zangu mbili tu, na kasupu kamato ka utumbo hapo nimeimaliza siku kibingwa kabisa.
Umenikumbusha na leo jioni napita pale karibu na kwetu,kuna jamaa yeye anapika hizi chapati ila kajiongeza na supu ya utumbo buku 2 kibakuli kinajaa...
 
Mama Swaumuu leo umepewa maua yako hapa JF, kila nikikusifiaa unasema nataniaa, leo umepewa JF hapa.

Chapati unajua kupika, zinapikika, na zinalikaaaaa, huna bayaaaa.

Mie nahamia kwenye vitumbua pia, Da Zulekha vitumbua vyako viko vyedii, hakika kila jioni yangu inasindikizwa na vitumbua vyakoo.
Huna hiyanaa Da Zuu.

Waishi sana hawa watuu, weraaaaaah [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Umenikumbusha na leo jioni napita pale karibu na kwetu,kuna jamaa yeye anapika hizi chapati ila kajiongeza na supu ya utumbo buku 2 kibakuli kinajaa...
Usisahau kukamulia ndimu na kuweka pilipili
 
Hayo ndo maisha yetu sisi waswahili,Kam ww wakishua tupishe kidogo maan hv vitu ni adimu pande flani hv,afu majina maaruf ya watoa huduma hizi:
Kwa wanawake;-akina mam Amina&swaumu
Kwa wanaume;akina ommy na ramadhan
 
Na chapati zinazo pikwa na wanaume ndy huwa nzuri zaidi
 
Hapa town kwa sasa kila kona hawa jamaa wapo, wanapika chapati nzuri na napenda sana namna wanavyo pika na kugeuza chapati kwa madoido.

Wanatuokoa sana sisi mabachelor, kwa 500/= tu unachukua chapati ya uhakika, sio zile za mama lishe ambazo ni nyepesi kama vitambaa.

Wanaofanya biashara hii wengi ni vijana wakiwa kama kundi, napenda ninunue kwao ili niwasapot katika biashara zao.

Big up sana kwa vijana wote walio ungana na kufanya hii biashara naamini inawalipa vizuri kwani wateja ni wengi sana kwa sasa.

Hapa nipo njiani narudi home na nitapita sehemu nipate zangu mbili tu, na kasupu kamato ka utumbo hapo nimeimaliza siku kibingwa kabisa.
Tena kasupu ka buku ..loh, safi kabisa. Vijana hao kweli wanafanya vema
 
Mixer masharo waajiriwa hasa bank na kampuni za simu.

Wanajifanya hawana appetite kumbe ndio mkombozi wa tumbo hasa tarehe za kati ya mwezi.
Yaani mtu akintajia tu mihogo nahs kama uchizi natamani hapo hapo niipate. Hapa nishawaza wapi ntapata mihogo mizuri mibichi ninunue nkaange mwenyewe. Maana mihogo ina mburo siku umeitamani ndio unapata mibaya mpaka inakutumbukia nyongo
 
Back
Top Bottom