Wauza smartphone tukutane hapa

Anayefaham bei ya Samsung galaxy S9 plus na S10 plus anijuze tafadhal ili nijipime
s9 plus model ya uhakika SM-G965F/DS ni kama 1.2 - 1.5M, S10 Model ya SM-G975F/DS ni 2.2-2.5M.
kumbuka hizi s10-series LEO mida ya usiku kwenye saa tano hv ndio zinaanza kuingia sokoni/kusambazwa rasmi kwa zones and carriers zote.
Watu hawajui tu ila models namba zina matter SANA hasa kwenye samsung na iphones, sasa jichanganye ununue samsung yyt models namb mwisho umeandikiwa V,T,S,ATT n.k, ukipata ambayo haitakusumbua NETWORK kwa mazingira yetu haya shukuru na nenda katoe sadaka, na ukiona inapiga kazi vizuri ujue ilipaswa iwe zaidi ya hapo na ukitaka uone utofauti tafuta F/DS ulinganishe kwenye signal strength (-dbm) au nenda sehem yenye shida ya network ndio utaona tofaut zao
 

Mkuu vp kuhusu iphone model ipo sahihi kwa ukanda wetu?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
200k ipo hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu vp kuhusu iphone model ipo sahihi kwa ukanda wetu?


Sent from my iPhone using JamiiForums
kwa iphone kujua ni mpk utaje kbsa ni iphone ngapi, maana wao Models zao nying kama sio zote hawaweki herufi za kuonyesha/tambua zones/carriers mwishoni, zinakua kama A1688, A1668, A1865, A1900 n.k, ila samsung wao models zao karibia zote humalizia kwa herufi mfano SM-G950F/DS, SM-G950T,SM-G950V n.k na ndio inatambulisha kama simu ni free/global/international, factory unlocked, carrier unlocked au locked,

yaani kwa ufupi hapa tunazungumzia zile simu ambazo kibongo bongo tunaita zilizoflashiwa, mfn unanunua simu tigo au voda inaingia laini ya tigo au voda tu, kwaio unaenda ku i flash ili utumie laini zote! NAHISI UNAELEWA MADHARA YAKE?, sasa hizi ndio wanaita carrier unlocked, na piga ua wewe ukiipata lazima iwe ni mtumba, refublished au vyote kwa pamoja, hizi simu hasa samsung na iphones 90% ndio zimejaa k.koo
 
Jaman tunakumbushana tu:

unapoenda dukani ukaona smartphone imewekwa show off inameremeta na mastika kibao au inatolewa kwenye boks bila boks kuchanwa popote ujue hio SIO mpya, hakuna smartphone inayotoka kiwandani bila kua sealed, narudia tena HAKUNA.

NOTE: sijasema zote sealed ni mpya, kuna wajanja.
 
Umenena sana mkuu
Unakuta mtu kisa simu imekuja na box anadai ni brand new, zote ni refub tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…