Tufahamu hivi,... Kuna seller refurbished na manufacturer refurbished. Sasa nyingi zinazoletwa na wafanyabiashara wa TZ ni seller refurbished, simu inakuwa imepungua ubora wa hardware kwa zaidi ya asilimia thelathini.
Mfano: Hutolewa battery halisi na kuwekwa battery ambalo sio original kitu ambacho kinaweza kupelekea simu kutokutunza chaji kama ile brand new.
Hardware ubadilishwa baadhi ya vifaa na kupekekea kupungua ubora. Mf: simu inabalishwa housing na inawekwa housing isiyokuwa na watertight seals, na kupelekea kuondoa umadhubuti kwa simu yenye IP Certified Waterproof & Dustproof.
Cha niongeza,... Kweli, kwa nchi zilizoendelea refurbished phone zipo ila ni zile manufacturer refurbished ambazo ni kama mpya kwa asilimia 90
Ahsante.