Son of Gamba
JF-Expert Member
- Oct 26, 2012
- 4,720
- 6,957
Binafsi nakerwa sana na Wanawake wenye tabia ya kuvaa wigs kichwani au kushonea nywele za bandia. Hii ni tabia ambayo kwakweli mimi huwa siipendi kabisa na huwa namwona Mwanamke wa namna hiyo kuwa ni mchafu na limbukeni.
Kwanini Wanawake msiridhike na kile mlichonacho? Kama nywele zako ni fupi, zitunze hivyo hivyo na unaweza ukazipendezesha bila kuvaa nywele za marehemu usiowajua wewe. Kuna mawigi mengine ni nywele halisi za watu, wengine ni marehemu, na wengine wana mikosi yao huko na wewe unavaa tu kichwani bila hata kutafakari. Wengine wameachiwa "laana" zisizofutika na wewe unavaa nywele zake na kumsaidia kubeba laana zake. Ndiyo maana Wanawake mnaandamwa na matatizo yasiyokwisha na mengine hata hamjui chanzo chake ni nini.
Naamini wavaa "mawigi" wakimtazama huyu binti na nywele zake za asili, wanaona wivu sana, roho zinawauma. Lakini binadamu siku zote tunafundishwa kushukuru kwa kila jambo. Mimi naamini MUNGU aliyewaumba wenye nywele fupi hakukosea, basi msivae mawigi, kwani kwa kufanya hivyo mnakuwa kama mnaukosoa uumbaji wa BABA MUNGU. Na wale wenye kunyoa nyusi zao pia, mnakera sana tena sana. Kwanini usitulie na uzuri wako wa asili?? Kwanini wanawake mnapenda kuwa FAKE?
Jamani hata bila kuvaa "nywele za marehemu"(mawigi), kichwani bado mnapendeza sana tu. Ladies, be real!