Wavaa nywele bandia wakiona picha hizi wanaumia sana

Wavaa nywele bandia wakiona picha hizi wanaumia sana

Binafsi nakerwa sana na Wanawake wenye tabia ya kuvaa wigs kichwani au kushonea nywele za bandia. Hii ni tabia ambayo kwakweli mimi huwa siipendi kabisa na huwa namwona Mwanamke wa namna hiyo kuwa ni mchafu na limbukeni.

Kwanini Wanawake msiridhike na kile mlichonacho? Kama nywele zako ni fupi, zitunze hivyo hivyo na unaweza ukazipendezesha bila kuvaa nywele za marehemu usiowajua wewe. Kuna mawigi mengine ni nywele halisi za watu, wengine ni marehemu, na wengine wana mikosi yao huko na wewe unavaa tu kichwani bila hata kutafakari. Wengine wameachiwa "laana" zisizofutika na wewe unavaa nywele zake na kumsaidia kubeba laana zake. Ndiyo maana Wanawake mnaandamwa na matatizo yasiyokwisha na mengine hata hamjui chanzo chake ni nini.
View attachment 753448
Naamini wavaa "mawigi" wakimtazama huyu binti na nywele zake za asili, wanaona wivu sana, roho zinawauma. Lakini binadamu siku zote tunafundishwa kushukuru kwa kila jambo. Mimi naamini MUNGU aliyewaumba wenye nywele fupi hakukosea, basi msivae mawigi, kwani kwa kufanya hivyo mnakuwa kama mnaukosoa uumbaji wa BABA MUNGU. Na wale wenye kunyoa nyusi zao pia, mnakera sana tena sana. Kwanini usitulie na uzuri wako wa asili?? Kwanini wanawake mnapenda kuwa FAKE?

Jamani hata bila kuvaa "nywele za marehemu"(mawigi), kichwani bado mnapendeza sana tu. Ladies, be real!
Nywele bandia ni kichaka cha mapepo na maruhani
 
ni wanawake wachache sana wanaweza kumudu kuvaa nyele za watu wengine lakini wigi nyingi ni plastic material na wala sio nywele halisi za binadamu! zilizo halisi zinauzwa bei mbaya na kwa bahati mbaya wengi wenye uwezo wa kuzinunua hawako tayari kuzitumia -over!
 
Binadamu hatufanani, as long as mwanamke apendeze kwa kujiremba vyema, haijalishi kavaa wigs, kavaa mini skirt n.k
 
Binafsi sipendi hayo mawigi,,na wanavyosuka sjui rasta,,,hata girl wangu nimemwambia sana kuacha kusuka rasta but hasikii
 
Wanaboa sana hawa wanawake unamkuta kaweka hayo manywele yake ana wiki hajaweka maji kichwani,kichwa kinanuka tii akikupita unatamani usikutane nae tena. Mnakera sana nyie basi tu!!
 
Kapendeza.


1629324135941.png
 
Kama nakuona vile na wewe umevaa nywele za marehemu usiyemjua au umevaa maplastiki kichwani..... Tunakereka ndiyo sababu ninyi mpo ndani ya jamii hii hii na kila mnalolifanya linaweza kuwa linatupendeza sisi wanaume ama linatukera. Lile linalotukera lazima tuseme bila kuwaonea aibu.
Mitumba ya magari nguo! mashine, ndege unazo panda ni vya marehemu!! wewe usitutishe! kafa ulaya matumizi africa !!! ndo dunia ilivo! haya ya kwako ni mambo ya wana vijiji!! waafrica mna nini cha kwenu? cha kulingishia DUNIA? Wee umefanya nini? hapa duniani?

km hutaki wavae tuachie sisi born town tunaojua kuyatumia, tutawapa sana, ni sisis tunataka wapendeze hivo!!! hiyo harufu ya kunuka tuachie sisi ndo tunataka, wewe kafukuzane na wala milenda huko kjijini! kalime nyanya!!

wadada pigeni kazi tu! m puuzeni huyu mkulima, msimjali,... ma born town tuko nyuma yenu!! na hawagusi mtu hapa!
 
Mnajivisha vichwani mwenu matatizo ya watu msiyoyajua. Inasemekana eti kuna wengine huwa wanamajini mahaba na mapepo, sasa wanaponyoa nywele zao na kuziuza, siku wanapofariki, yale majini mahaba au mapepo yanamfuata yule mwanamke anayevaa zile nywele na kumfanya kuwa "mke".

Ndiyo maana wanawake wengi wanasumbuliwa na matatizo ya maroho machafu bila wao kujua yanatoka wapi. Nywele za mwanadamu zinabeba mambo mengi sana. Ndiyo maana hata Waisraeli walipokuwa wakitubu dhambi, walikuwa wananyoa nywele zote kichwani na mwilini ili kujisafisha upya. Sasa wewe unaponunua nywele za mwenzako ni kama unachukua matatizo yake na kujitwika kichwani. Huu ni mpango wa shetani kuwamaliza bila ninyi kujua.

Ukitaka kujua kama ni mpango wa Shetani, tazama jinsi biashara hii ya mawigi jinsi inavyoshika kasi duniani. Siku zote ukiona kitu kinapendwa sana na wanawake duniani, basi fahamu kuwa shetani ana mkono wake hapo.
Usabato wa kizamani huu unaleta hapa...... majini hayakai kwa nywele!! umedanganywa sana, likae hapo wakati kiti yuko kwingine? ulishindwa hata kuwaza tu? hii ni theorojia ya kibwetere, ambae hakusoma, na weye ni mfuasi wke pure! yesu wenu mbona ana wigi?
 
Usabato wa kizamani huu unaleta hapa...... majini hayakai kwa nywele!! umedanganywa sana, likae hapo wakati kiti yuko kwingine? ulishindwa hata kuwaza tu? hii ni theorojia ya kibwetere, ambae hakusoma, na weye ni mfuasi wke pure! yesu wenu mbona ana wigi?
Je wewe ni binti?

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom