Wavaa nywele bandia wakiona picha hizi wanaumia sana

Siku zote Wanawake hufanya kile ambacho Wanaume huvutiwa nacho!
Sidhani kama wanaume tunavutiwa na hizo kitu hebu fanya tafiti tena.

Sayansi inaonyesha kuwa wanawake hupenda kushindana wao kwa wao. Hivyo swala la mawigi sijui kupakaa zile Niru zao usoni ni kwa minajiri ya kushindana urembo si matakwa ya wanaume.

Wengine hufanya fake make up ili kuficha dosari za kimwili kama nywele mbaya kichwani zinazopunyuka kama mtu mwenye terminal illness, makovu au mabaka, etc.

Wengine hufanya fake make ups kuficha dosari za kiakili au za kitabia. Yote kwa jumla ni kuwa watu huvaa make ups kuficha madhifu yao na hii ni matokeo ya kutojiamini.
 
Ila Rihanna anac komwe.... Mawigi yake huwa anaficha komwe....
 
Kuna miaka ya 1990 enzi za nyimbo za akina Kandabongo man kutamba, wakina dada walikuwa na urembo wa kivaa manywele kama kalikiti hiviu, wapakaa shedo nyekundu halafu wanajisiliba mapoda usoni.

Walahi zile picha ukikiziona nyakati hizi unajisemea daaaaaaaah[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kweli fashion ni swala la muda tu linageuka kuwa kituko.

Watu walikuwa wanatokea kama mazombie au vampire waliotoka kunywa damu.

Auntie yangu ukimuonyesha hizo video anatamani kitoka nduki anakwambia chana hizo picha.
 
Wengine ni wanawake, tumezaliwa na tutakufa bila nywele za marehemu wa India na nchi zinazozalisha nywele hizi. Hizo ni kwa wanaojiweza, wasiojiweza wanaishia mipira.

Wigi na haya majitu ya kuweka kichwani yanakula nywele. Wataishia kuwa vipara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…