Wavuta sigara tukutane hapa: unapenda sigara ipi, unapenda kuvutia mazingira yapi na una lipi la ziada ?

Wavuta sigara tukutane hapa: unapenda sigara ipi, unapenda kuvutia mazingira yapi na una lipi la ziada ?

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
hamuwezi kuamini hata rafiki zangu wa karibu na ndugu mpaka leo hawajui kama navuta 😂😂 nikiwa maeneo ya karibu na home napenda kuvuta kwa kujificha ila nikiwa mitaa ya mbali au nje ya mkoa naweza kuvuta wazi.

Binafsi nimevuta sigara za aina nyingi kuanzia embassy, club, spoti, nyota, winston, master, sm na hata za nje kama malboro lakini nimesalia kwenye spoti na winston.

Sipendi sigara zenye harufu kali kama sm na nyota.

Napendelea kuvuta nikiwa nimesimama, sijui kwanini nikikaa hainipi burudani.
 
fe862e634a0e8b63011910415fd79e0b.jpg
 
Kilevi kibaya sana hiki sijui nilidumbukiaje humu ila siku moja kwa uwezo wa Mungu nitaiacha.... Napenda kuvuta nikiwa melala au mekaa inanipa uvivu sana kiasi kwamba sitamani kufanya chochote baada ya kuvuta napenda kuvuta nikiwa mwenyewe
 
Mi nataka nianze kuvuta mneli.

Starehe ambayo nimefanikiwa kuiepuka hadi Sasa umri huu wa miaka 30 na kitu.

Nataka nijaribu kijiti nione ladha Yake. [emoji1787]
 
Kilevi kibaya sana hiki sijui nilidumbukiaje humu ila siku moja kwa uwezo wa Mungu nitaiacha.... Napenda kuvuta nikiwa melala au mekaa inanipa uvivu sana kiasi kwamba sitamani kufanya chochote baada ya kuvuta napenda kuvuta nikiwa mwenyewe
Usikata tamaa mkuu, ipo siku utaacha hutaamini! Nlikuwa mtumiaji mzuri sana wa sigara ..yaani kwa siku nlikuwa nikitumia pakt 1 ya embassy. Ila siku moja nikakata sharing nikwanini napata tabu haswa napokuwa ktk mikusanyiko ya watu nikaa nikarafakari nikajiwekea dhamira yakujaribu kuacha kwa miezi 6, baada yakupita hiko kipindi nlipokuja kujaribu tena mara kadhaa ilishindikana yani kifua kikawa kinanibana sana huo ndio uliokuwa mwisho wa kuvuta sigara huu nimwaka wa
 
Usikata tamaa mkuu,ipo siku utaacha hutaamini! Nlikuwa mtumiaji mzuri sana wa sigara ..yaani kwa siku nlikuwa nikitumia pakt 1 ya embassy. Ila siku moja nikakata sharing nikwann napata tabu haswa napokuwa ktk mikusanyiko ya watu .nikaa nikarafakari nikajiwekea dhamira yakujaribu kuacha kwa miezi 6, baada yakupita hiko kipindi nlipokuja kujaribu tena mara kadhaa ilishindikana yani kifua kikawa kinanibana sana .huo ndio uliokuwa mwisho wa kuvuta sigara huu nimwaka wa
Mwaka wa 9 unaisha nanlikuwa nmeshatumia kipindi cha miaka ya nyuma takribani miaka 7
 
Kokote Duniani utafiti umekuja na majibu yale yale kwamba watu wanaovuta sigara wana akili ndogo sana kulinganisha na wasiovuta.

Wavuta sigara ni kama mabata, bata akijisikia kunya hata kwenye sufuria ya ugali anakunya tu, hajali kitu. Mvuta sigara hivyo hivyo, akishikwa na kiu mahala popote anawasha sigara bila kujali kuna watoto ama watu wengine.

 
Binafsi nimevuta sigara za aina nyingi kuanzia embassy, club, spoti, nyota, winston, master, sm na hata za nje kama malboro lakini nimeasalia kwenye spoti na winston.

Sipendi sigara zenye harufu kali kama sm na nyota.

Mazingira nayopendelea kuvuta ni yale ambayo hayana watu wengi na kuna kivuli ama kaubaridi.

Napendelea kuvuta nikiwa nimesimama, sijui kwanini nikikaa hainipi burudani.

Nimejaribu kuacha kwa miezi kadhaa katika vipindi vinne tofauti lakini nilirudi.
napenda sana sigara kali napenda sana kuvuta sigara ukweni mbele ya baba mkwe
 
Nshakuwa na tabia yakuvuta SM bia zikikolea, ila zikiisha sina hata hamu nayo kifupi sijawahi kuwa addicted ni mpaka nile bia tena rafiki zangu wakiwasha ndo nagongea ila sio kuifata dukani.
Nashukuru Mungu hicho kilevi kimenpitaga kushoto sana
 
Back
Top Bottom