WAWEKEZAJI wakuu katika mradi wa gesi kimiminika (LNG) Tanzania, wachagiza mchakato uharakishwe

WAWEKEZAJI wakuu katika mradi wa gesi kimiminika (LNG) Tanzania, wachagiza mchakato uharakishwe

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
WAWEKEZAJI wakuu katika mradi wa gesi kimiminika (LNG) wahimiza Tanzania iharakishe mchakato, mradi Uanze


View: https://m.youtube.com/watch?v=29vTb7IfVy4

Katika viunga vya mkutano huo wa Wiki ya Nishati India ( IEW India Energy Week) naibu waziri mkuu aliye waziri wa nishati mheshimiwa Dr. Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Petroli na Gesi Asilia wa India, Hardeep Singh kuhusu nia ya hiyo kuzidi kuimarisha biashara kati yake na Tanzania kupitia sekta binafsi, kufanya uwekezaji kwenye Sekta ya Nishati na kujengea uwezo wataalam.

Mazungumzo hayo yamefanyika Februari 11, 2025 jijini New Delhi nchini India katika Maadhimisho ya Tatu ya Wiki ya Nishati (IEW) nchini humo.

Dkt. Doto Biteko amemweleza Waziri Singh kuwa milango ya uwekezaji Tanzania ipo wazi na kampuni mbalimbali kutoka India zinaweza kuwekeza kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo ya umeme, usambazaji wa gesi ya mitungi (LPG) na uagizaji wa mafuta kwa pamoja (Bulk procurement) kwani kunahitajika washindani wengi ambao watatoa uhakika wa uwepo wa mafuta wakati wote.“


Tanzania tumejikita katika kuhakikisha tunatumia kila rasilimali tuliyonayo ili kuwa na nishati ya kutosha ikiwemo umeme ili kukidhi mahitaji ya wananchi,” amesema Dkt. Biteko.

Aidha, ameeleza kuhusu umuhimu wa ushiriki wa sekta binafsi katika kuendeleza miradi mbalimbali akitolea mfano kuwa, ili Tanzania ijitosheleza kwa mahitaji ya nishati inahitaji Dola za Marekani Bilioni 12 ambazo kupatikana kwake lazima sekta binafsi ihusishwe hivyo kupitia kwa Waziri Singh, amekaribisha wawekezaji kutoka India kuwekeza kwenye Sekta ya Nishati nchini.


Kuhusu ushiriki wa Tanzania katika Wiki ya Nishati India amesema kuwa Tanzania imefaidika na ushiriki wake katika Wiki hiyo kwani India tayari imeshapiga hatua kwenye Sekta ya Nishati hivyo imekuwa ni sehemu maalum ya kujifunza zaidi kuhusu sekta, kubadilishana uzoefu na kunadi fursa za uwekezaji ikiwemo duru ya tano ya uendelezaji wa visima vya mafuta na gesi asilia Tanzania.

Kwa upande wake, Waziri wa Petroli na Gesi Asilia wa India, Mhe. Hardeep Singh amesema kuwa India ina uhusiano mzuri wa kibiashara na Tanzania ambapo biashara kati ya pande hizo mbili imezidi kuimarika na kueleza kuwa nchi hiyo imejipanga kuimarisha zaidi biashara yake kwa Tanzania.
1739549636345.jpeg


Ameeleza kuwa, nchi hiyo pia kupitia Sekta binafsi inataka kuwekeza kwenye usambazaji wa mitungi ya gesi nchini hasa katika kipindi hiki ambacho Serikali inatekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia huku akieleza kuwa nchi hiyo imepiga hatua kubwa kwa kusambaza mitungi ya gesi kwa asilimia 99.9 kwa wananchi wake.

Ameongeza kuwa India imeamua kuwekeza kwenye uendelezaji wa Mafuta na Gesi Asilia ambapo baadhi ya kampuni zake zimejitokeza kushiriki Duru la Tano la kunadi vitalu vya Mafuta na Gesi Asilia linalotarajiwa kufanyika mwaka huu mwezi Machi nchini.“ India pia tupo tayari kuwekeza kwenye gesi ya kusindika (LNG), bayofueli pamoja na kushirikiana na Tanzania katika masuala ya kitaalam yanayohusu Sekta ya Nishati kwa kuwajengea uwezo zaidi wataalam wa Tanzania na pia kuwa na programu ya kubadilishana wataalam kati ya Tanzania na India,” asema Mhe. Singh.

Pia, ameipongeza Tanzania kwa kupiga hatua kubwa kwenye usambazaji wa umeme hususan vijijini na kwa jinsi inavyotekeleza mkakati wa nishati safi ya kupikia kwa namna mbalimbali ikiwemo kuweka ruzuku kwenye mitungi ya gesi.Vilevile, Waziri Singh amempongeza pia Dkt. Biteko kwa hekima zake na ukomavu ambao anauonesha pale anapoieleza dunia kuhusu masuala ya uendelezaji wa rasilimali zinazoweza kuzalisha umeme ambazo Bara la Afrika imebarikiwa nazo lakini mpaka sasa hazijaendelezwa ipasavyo kutokana na misimamo ya kidunia ikiwemo makaa ya mawe ambayo yakiendelezwa yatazidi kutoa uhakika wa uwepo wa nishati ya kutosha.

Mazungumzo kati ya viongozi hao yamehudhuriwa pia na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambaye anamwakilisha Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Idd Kassim, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Mhandisi Innocent Luoga na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Dkt. James Andilile
 
Februari 13, 2025
New Delhi, India

Tanzania yawahakikishia wawekazaji wa kimataifa, inasukuma mchakato wa mradi wa gesi LNG ukamilike haraka gesi itoke

BITE-332x221.jpg

INDIA: NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amehakikisha kuwa serikali inajadiliana na wawekezaji kuhusu motisha ya kodi ili kujenga mtambo wa kuzalisha gesi asilia ya kimiminika (LNG) wenye thamani ya dola za Marekani bilioni 42 (takriban trilioni 109/-) nchini.


Dk Biteko ambaye alikuwa India kuhudhuria kongamano la tatu la kila mwaka la Wiki ya Nishati (IEW) alisema mazungumzo hayo yanaweza kukamilika ifikapo Juni 2025.


Kampuni ya Equinor na Shell ni waendeshaji wa pamoja wa mradi mkubwa wa gesi nchini, huku Exxon Mobil, Pavilion Energy, Medco Energi na kampuni ya kitaifa ya mafuta ya Tanzania TPDC ni washirika.

"Mradi haujasimama, tunajadiliana kuhusu jinsi tunavyoweza kufanya mradi huo kuwa wa manufaa kwa sisi sote," alisema Dk Biteko.

Aliongeza kuwa baadhi ya motisha za serikali zitapaswa kutolewa, na kwamba kiasi cha uzalishaji kinategemea mazungumzo.
Aliongeza "Siwezi kusema hadi tukamilishe mazungumzo, lakini nadhani mazungumzo yatakamilika ndani ya mwaka huu wa fedha, kati ya sasa yaani February 2025 na Juni 2025."

Mradi huo utazalisha futi za ujazo trilioni 47.13 za gesi asilia nchini. Dk Biteko aliongeza kuwa nchi inatarajia kuzindua duru ya leseni ya utafutaji wa vitalu 26 vya mafuta na gesi mwezi ujao Machi 2025.
 
Tunapoingia hii mikataba tuangalie sana na kufikiria sana Tanzania ya baadaye.
Kuna fikra tukiwa nazo basi tutajua ni nani wakusaini naye mikataba.

Tusiwaze sana kulipwa Kodi ili tulipane mishahara minoni serikalini na sisi akaunti zetu zikatuna na tukapata hela za kampeni pia maisha ya Leo yakaendelea lakini maisha ya Tanzania ya baadaye yasiwepo.

Wahindi/Waarabu/Wachina ni watu hatari sana kufunga nao mikataba na kuwategemeaa kwenye uwekezaji maana bado wanawaza kimasikini na wako kwenye stage yakuamini kutesa na kuumiza watu ili kupata mafanikio.
Mikataba mikubwa na hao jamaa ni kuwafanya watanzania masikini maana ni watu ambao hawajali ustawi wa binadamu mwingine nje yao, Wazungu ajira zao hujali utu na maendeleo ya mtu hivyo watalipa watu wetu vizuri, watalinda Afya za watu wetu na watawaendeleza watu wetu maana wao hawawazi kimasikini kama hao wengine.

Chukulia mfano makampuni ya ujenzi wa barabara ya kichina, kihindi na kiarabu halafu uje ufikirie makampuni ya ujenzi wa barabara kutoka Ulaya, fikiria ajira katika makampuni ya Ulaya na ajira katika jamii hizo nilizozitaja.

Wanasiasa muache kufikiria leo yenu na familia zenu, ni wakati wa kufikiria kesho ya watanzania.
 
Back
Top Bottom