mr yamoto
JF-Expert Member
- Oct 2, 2016
- 923
- 1,395
Kama mataga wameshindwa kujibu hata swali moja sidhani Magufuli hataweza kujibuRais Magufuli nilikusema kuhusu miradi inayoeendelea chato kupitia uzi huu Miradi inayoendelea chato inahitaji mjadala wa kitaifa ila sikujibiwa kilichofuata ni mimi kutukanwa na wafuasi wako kwamba ni siasa.
Mh Rais tuachane na hayo je miradi yako mikubwa inayotekelezwa kwa nini haina transparent?
1: Ununuzi wa ndege: Serikali yako imeshindwa kabisa kujibu tuhuma za kwamba unanua ndege cash ili upate 10% kama aya ni ya kweli inamaana kama umetumia 1.8 trion mpaka sasa kununua ndege 6.
Mpaka sasa kama unatupiga 10% inamaana tumeshapoteza 180bilion je ni ya kweli haya kama sio ya kweli kwa nini ofisi yako ipo kimya haijibu chochote? Kama sio ya kweli kwa nini CAG haruhusiwi kukagua ununuzi wa ndege na shirika letu la ATCL? kuna nini uko Mh Rais? ningepata majibu na Watanzania wangepata majibu ingekuwa vizuri.
2: Mh Rais Sector ya madini imekuwa pia haikaguliwi kwa nini? nini kinafichwa uko mbona waziri wako wa madini hasemi kwa nini sector hii haikaguliwi? Mh Rais watanzania sio vilaza kiivyo kama ulivyowaita watoto wetu kule UDOM wana uelewa mpana wa kuchanganua mambo hata kama hawaoni kama mimi ninavyoona ivi Mh Rais kwanini madini yanatoroshwa sana kule melelani Arusha?
Na yanasindikizwa na maafisa wa idala ya usalama wa taifa? wewe utabisha sana lakini maafisa wa Migiration umewaweka kwenye wakati mgumu sana kwa kupambana mizigo isivushwe maana inasindikizwa na watu wazito kweli naongea hivi nikiwa na ushahidi 100%.Mh Rais kumbe ndio maana wale polisi waliokamatwa na mzigo wa madini walisamehewa kwanini walisamehewa? kuna tuhuma kwamba kuna madini yanafichwa Rwanda je izi tuhuma ni uongo kama ni uongo kwa nini IKULU haikanushi ili swala? Mh Rais naomba uelewe watanzania sio wajinga hata kidogo naomba serikali yako ilete majibu.
3: Mh Rais Ujenzi wa SGR Je Unajua kwamba kampuni ya uturuki inayojenga SGR moja ya watu wenye hisa kwenye kampuni iyo ni Fisadi Rostam Aziz? alituma mtu baada ya kuona umekata milija ya wachina kujenga reli iyo akaenda kununua hisa kwenye iyo kampuni kwa kutumia mtu mingine je unayajua ayo ? Sizani kama uyajui na sizani kama Rostam alikuja kwa bahati mbaya IKULU sizani na sizani kama kukubali kwake kurudisha CHANEL TEN na MAGIC FM ni kwa bahati mbaya ni fadhira ya kazi yako uliyoifanya kwa either kwa kujua au kutojua.
Mh Rais je ni kweli kwamba wachina walishindwa kukupa 10% na waturuki unachukua 10% je aya niyakweli? kama hayana ukweli kwanini umekataa kuendelea kwa ujenzi wa bandari ya bagamoyo ambayo ndio ingekuwa bandari kubwa East,Central and south of Africa continent na ingeweza kuudumia nchi si chini ya 10 kusini mwa jangwa la sahara.?
Mh Rais ivi wakitoa 10% awa wachina kweli utabaki namsimamo wako? tuyaache turudi kwenye SGR je kama hakuna ufisadi kwenye ujenzi wa SGR kwanini CAG harehusiwi kufanya ukaguzi uko? kuna nini cha ziada ? Nini kinafichwa uko?
Mh Rais ingekuwa vema kama serikali yako ingejitokeza na kutoa ufafanuzi wa kutosha kuhusu miradi ya ununuzi na ujenzi kugubikwa na ufisadi wa kutisha hasa ule 10% watetezi wako tunapata wakati mugumu sana kwa sababu mambo mengine tunayaona wenyewe kila kona ufisadi.
Ulichofanikiwa ni kuziba midimo ya media na wapinzani wako ili wasiseme ukweli kwa taarifa tu ni kwamba kampuni inayopewa tenda za ujenzi wa barabara ya Nyanza road sasa imefirisi nchi kwa kulipwa pesa na kushindwa kujenga barabara nchini, Mh Rais je unafikiri hatujui ufisadi unaendelea kwenye ujenzi wa MELI ndani ya ziwa victoria? Je ujenzi wa daraja la Busisi utakaoanza karibuni ufisadi wake wewe ufahamu?
Mh rais haya yote unayataka mwenyewe kwa kutoruhusu CAG Kukagua miradi yako ya ujenzi na madini, Mh Rais mimi nakupenda wewe na naipenda Tanzania na mimi ni mzalendo wa kweli nakwambia ukweli kuliko wanaokupaka mafuta kwa mgongo wachupa!
Nitasema ukweli daima funua ufisadi uliopo ndani ya serikali ruhusu mijadala iliyo huru, viache vyombo vya habari viwe huru ili watu wajue kunachendelea ndani ya serikali yako mimi nakuhakikisha usiporuhusu ukaguzi ulio huru Mh Rais Serikali yako itaweka rekodi ya kuwa serikali ya kifisadi kuliko serikali zote zilizokutangulia.
Mimi nakupenda nakwambia ukweli niliyoyaona ndani ya utawala wako toka mwaka 2015 mpka sasa sio mambo ya kunyamazia hata kidogo.
Mh Rais Watanzania sio wajinga hata kidogo.
Kama ameshindwa kukaa na Prof Assad katika mapambano ya rushwa katika ofisi za serikali hakika hakuna mwema katika CCM
Jaribu kutafakari majibu ya huyu mtu [emoji116][emoji116] ni [emoji706][emoji706] tupu
Mlianza kumhujumu Magufuli nyuma ya pazia
Mlipiaibishwa mmejitokeza hadharani sasa
Mtaendelea kuaibika hamtafanikiwa