Wazaliwa wa mkoa wa Tanga tukutane hapa

Wazaliwa wa mkoa wa Tanga tukutane hapa

washambaa mzaivaa na mzaona?
f2c52f7d985bef21d00f35e2f03db976.jpg
[emoji1][emoji1][emoji1] weshu tiivie
 
Hii hatari, wanaosema tanga uchumi haupo wamefika tanga gani ? Njooni muone mahanjumati hayoooooooo. Kama huna hela utanunulia nini ? Badala ya kuja tanga eti mwenda dodoma. Mayoooooo kweli zimtini.
Kweli akili yako iko kwenye kisosi, uchumi wa maandazi na bagia
 
Sasa tuzungumze la maana hapa.

Tanga ni mkoa unaoweza kujijenga vizuri sana kiviwanda. Ipo katika uwezo wetu wana Tanga na Watanzania wengineo kuzitumia fursa zilizopo mkoani hapa kujikwamua kiuchumi. Aghalab sio uvivu bali ni kukosa muongozo wa kibiashara tufanye nini.

Nitatoa mifano ya fursa za kibiashara na viwanda zilizopo Tanga. Nikitambo kidogo tangu niwe nyumbani kwa hiyo mifano mingine inaweza kuwa tayari inafanyiwa kazi. Kama ni hivyo nijuze. Pia unakaribishwa kuongeza mifano mingine unayodhani inaweza kutusaidia kibiashara au kiviwanda.

Mifano:
1. Kusindika samaki karibu na bahari.
2. Kusindika nazi (tui la makopo) pamoja na bidhaa nyingine za minazi, kama vile pombe ya mnazi ndani ya kopo.
3. Kusindika matunda (maembe, machungwa, matufaa, n.k.), kutengeneza pombe ya matunda kama hard-cider kutokana na matufaa.
4. Kusindika mboga (kukausha-wanafanya hii sasa, kutia kwenye makopo, n.k).
5. Kutengeneza bidhaa za maziwa kama cheese, shikirimu, n.k.
6. Kutengeneza pombe kali (spirits) kutokana na mkonge (Taquila), kutokana na mnazi (distillery ya pombe ya mnazi), kutokana na pombe ya muwa (boha), kutokana na pombe ya mapumba ya mahindi (kangara).

Nimejaribu kutoa mifano ya kibiashara tunayoweza kiijengea viwanda nayo. Tunashindwa na nini ndugu zangu? Ama kweli penye miti hapana wajenzi. Tuibadilishe hii dhana jamani.

Pengine baadae tunaweza kuweka vichwa chini na kutengeneza Business Plans za baadhi ya hizi fursa.

WAKAYA TEVANA?
Ndio mkuu, tizaivana
 
Back
Top Bottom