mpita-njia
JF-Expert Member
- Dec 3, 2010
- 1,734
- 1,616
Aisee!
Wachache sana hata leo wana uelewa huo.Nilikuja kugundua baadae baabda ya kwenda nje ya nchi kama zile Range milango 6 ni gari za msafara wa kwenye misiba. Zinabeba wafiwa.
Sasa wakati sisi wadogo tukimuona Sheikh Yahya anapita nalo mtaani tulikuwa tunamkimbia.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaha naikumbuka,na ile gari ya akina IDD janguo nayo milango sita ,nimesahau
Hahahaha, mie Mtoto ana baiskeli lkn haendeshi yy ni game tuTulikiwa tunatoka Sinza hadi Mikocheni kwa baiskeli, tunazungumka Beach yote. Wazazi walikuwa wanachukulia poa.
Ila cha kushangaza siku hizi mwanangu haruhusiwi hata kwenda mtaa wa pili kucheza.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaha, ukiacha hy ratiba nimeona hapo Peugeot 504, inauzwa tena inatembeaView attachment 1418394nilichogundua huu uzi ni wa wahenga ila wahenga wa mzizima.. na hapa ndio tulikuwa tukipata ratiba ya cinema mjini uhuru/mzalendo
Huu wimbo unaitwa 'mazoea yananikondesha', ukipigwa hata leo utadhani ni wimbo mpya, hauchuji. Muimbaji na mtunzi wake nasikia ameshafariki akiwa kapuku tu. Kama ingekuwa ni enzi hizi angalau angevuna mamilioni.Naongeza na Mzinga Troupe wazee wa morogoro.,Morogoro Jazz, Kilombero Jazz,
Tafadhalini naomba mkongwe mmoja aniwekee ngoma iliyokwenda kwa jina 'Kinyonga' kutoka Mzinga Troupe.
Umechanganya madesa, umeenda 'up-side-down'. Mzee James yuko sahihi. Batavuz niliendesha nilipoanza kazi pale Dom mwaka 2000, ilikuwa moja tu na spea zake zilipatikana KJ Motors pekee.View attachment 1417643
JBourne59 hii tulikuwa tunaiita "Skuta" au kwa jina lake halisi ni "Scooter".
Hii hapa chini ndiyo Batavuzi!!
View attachment 1417641
Sie wahenga wa Kishumundu tunacomment wapi?[emoji848]View attachment 1418394nilichogundua huu uzi ni wa wahenga ila wahenga wa mzizima.. na hapa ndio tulikuwa tukipata ratiba ya cinema mjini uhuru/mzalendo
James Jason pale Magomeni kulikuwa na Zambia Hotel, ilikuwa karibu na soko la Magomeni eneo ambalo barabara ya Kawawa inapita, barabara ya Kawawa ilipojengwa nyumba zote za eneo lile zilibomolewa kupisha barabara.Maeneo ni yaleyale, ila Butiama hakujabadilika sana lakini kidogo Shibam kumebadilika
James Jason
Kwa mama njerii
Yap naikumbuka sana,kwamba alioga,kopo la kwanza,la pili akageuka chatu,Mnakumbuka story ya mtu aliyegeuka chatu pale Buguruni wahenga wenzangu?
Ngoja niwape hii. Miaka hiyo nasoma Mtendeni kwa Ally Futo, tunaishi posta mtaa wa Libia dada yangu anaishi Ubungo zile kota ndogo jirani na RUBADA. Akawa amekuja kututembelea jumapili. Ilipofika jioni tukamsindikiza na mdogo wangu ili akapande basi Mnazi mmoja. Wakati huo kuna njia katikati ya bustani. Kabla hajapanda Ikarus akatupa dala ili tugawane kila mtu shilingi mbili na senti hamsini. Wakati tunarudi tukiwa kwenye zile njia za bustani nikamwambia mdogo wangu hela imeanguka. Nikajifanya naitafuta wakati hela iko mfukoni. Na yeye akainama, mara akatokea mtu akauliza mnatafuta nini mwenzangu akamjibu tumeangusha shilingi tano. Yule mtu akaanza kutafuta wakaanza kuongezeka watu wengi. Sasa jinsi ya kusema kwamba nilikuwa natania nikawa naogopa kwa sababu kulikuwa na watu wazima.Sijuj kama unafahamu hii maana ya neno Daladala.
Dala ilikuwa ni shs 5. Sasa Nauli ya maeneo mengi ilikuwa ni shs 5, kama ilivyo shs 400 siku hizi.
Wapiga debe walikuwa wanasema nauli dala dala. Ndio jina lilipopata umaarufu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Siku hizi unamfahamu leo unampa hela ya vocha unakula leo.Siku hizi wasichana wamejirahisisha sana. Zamani unafukuzia demu mwaka, unaambulia kumshika mkono tu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sio Vespa?View attachment 1417643
JBourne59 hii tulikuwa tunaiita "Skuta" au kwa jina lake halisi ni "Scooter".
Hii hapa chini ndiyo Batavuzi!!
View attachment 1417641
Nazitamani zile ngoma nizisikie tena. Nakumbuka vituko vya Michael Katembo.R.T.D kipindi cha Bujaga izengo kadago,kilikua kinaitwa Ngoma zetu asilia,
Tangazo la IPP "Ah! mama Mariam vipi?...Hizi nguo dadaangu,nimetumia kila aina ya sabuni lakini bado tu hazitakati!!" "Si utumie Komesha"
Ni kwamba watu walikuwa wema sana au kila mtu alitamani aiokote halafu aminyie?Ngoja niwape hii. Miaka hiyo nasoma Mtendeni kwa Ally Futo, tunaishi posta mtaa wa Libia dada yangu anaishi Ubungo zile kota ndogo jirani na RUBADA. Akawa amekuja kututembelea jumapili. Ilipofika jioni tukamsindikiza na mdogo wangu ili akapande basi Mnazi mmoja. Wakati huo kuna njia katikati ya bustani. Kabla hajapanda Ikarus akatupa dala ili tugawane kila mtu shilingi mbili na senti hamsini. Wakati tunarudi tukiwa kwenye zile njia za bustani nikamwambia mdogo wangu hela imeanguka. Nikajifanya naitafuta wakati hela iko mfukoni. Na yeye akainama, mara akatokea mtu akauliza mnatafuta nini mwenzangu akamjibu tumeangusha shilingi tano. Yule mtu akaanza kutafuta wakaanza kuongezeka watu wengi. Sasa jinsi ya kusema kwamba nilikuwa natania nikawa naogopa kwa sababu kulikuwa na watu wazima.
Jinsi ya kumwambia mwenzangu tuondoke nashindwa. Nikasogea pembeni nikatoa hela mfukoni huku nikiwa natetemeka, nimeinama nikasema hii hapa. Wakati huo watu kibao na wamechafuka mikono kwa vumbi.
Kwa macheni je?Unakumbuka Magoti...? Je unamkumbuka Maumba...? Fodi je...?