Wazamani (wahenga) tukutane hapa

Wazamani (wahenga) tukutane hapa

Wakongwe mnakumbuka zile studio za kurekodi na kuuza kanda za muziki? Binafsi nakumbuka vichache
Kimoja kilikuwa pale Manzese Argentina,kingine Temeke mwisho, na kingine Mtoni kwa Azizi Ali.
Wakongwe wenzangu mtakuwa mnayakumbuka mengine.
 
FB_IMG_15839145902858219.jpg
nilichogundua huu uzi ni wa wahenga ila wahenga wa mzizima.. na hapa ndio tulikuwa tukipata ratiba ya cinema mjini uhuru/mzalendo
 
Naongeza na Mzinga Troupe wazee wa morogoro.,Morogoro Jazz, Kilombero Jazz,

Tafadhalini naomba mkongwe mmoja aniwekee ngoma iliyokwenda kwa jina 'Kinyonga' kutoka Mzinga Troupe.
Huu wimbo unaitwa 'mazoea yananikondesha', ukipigwa hata leo utadhani ni wimbo mpya, hauchuji. Muimbaji na mtunzi wake nasikia ameshafariki akiwa kapuku tu. Kama ingekuwa ni enzi hizi angalau angevuna mamilioni.

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maeneo ni yaleyale, ila Butiama hakujabadilika sana lakini kidogo Shibam kumebadilika

James Jason
James Jason pale Magomeni kulikuwa na Zambia Hotel, ilikuwa karibu na soko la Magomeni eneo ambalo barabara ya Kawawa inapita, barabara ya Kawawa ilipojengwa nyumba zote za eneo lile zilibomolewa kupisha barabara.

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnakumbuka story ya mtu aliyegeuka chatu pale Buguruni wahenga wenzangu?
Yap naikumbuka sana,kwamba alioga,kopo la kwanza,la pili akageuka chatu,
Na kuna kawimbo staili ya singeli kaliimbwa mtu kugeuka chatu!!
Nilikuwa bado chalii wa miaka 7 kipindi hicho,
Nakumbuka uvumi wa ugonjwa wa seven days,Story ya maumba,mdudu kaingiaje kwenye kokwa la embe
 
Sijuj kama unafahamu hii maana ya neno Daladala.

Dala ilikuwa ni shs 5. Sasa Nauli ya maeneo mengi ilikuwa ni shs 5, kama ilivyo shs 400 siku hizi.

Wapiga debe walikuwa wanasema nauli dala dala. Ndio jina lilipopata umaarufu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ngoja niwape hii. Miaka hiyo nasoma Mtendeni kwa Ally Futo, tunaishi posta mtaa wa Libia dada yangu anaishi Ubungo zile kota ndogo jirani na RUBADA. Akawa amekuja kututembelea jumapili. Ilipofika jioni tukamsindikiza na mdogo wangu ili akapande basi Mnazi mmoja. Wakati huo kuna njia katikati ya bustani. Kabla hajapanda Ikarus akatupa dala ili tugawane kila mtu shilingi mbili na senti hamsini. Wakati tunarudi tukiwa kwenye zile njia za bustani nikamwambia mdogo wangu hela imeanguka. Nikajifanya naitafuta wakati hela iko mfukoni. Na yeye akainama, mara akatokea mtu akauliza mnatafuta nini mwenzangu akamjibu tumeangusha shilingi tano. Yule mtu akaanza kutafuta wakaanza kuongezeka watu wengi. Sasa jinsi ya kusema kwamba nilikuwa natania nikawa naogopa kwa sababu kulikuwa na watu wazima.
Jinsi ya kumwambia mwenzangu tuondoke nashindwa. Nikasogea pembeni nikatoa hela mfukoni huku nikiwa natetemeka, nimeinama nikasema hii hapa. Wakati huo watu kibao na wamechafuka mikono kwa vumbi.
 
R.T.D kipindi cha Bujaga izengo kadago,kilikua kinaitwa Ngoma zetu asilia,

Tangazo la IPP "Ah! mama Mariam vipi?...Hizi nguo dadaangu,nimetumia kila aina ya sabuni lakini bado tu hazitakati!!" "Si utumie Komesha"
Nazitamani zile ngoma nizisikie tena. Nakumbuka vituko vya Michael Katembo.

Sent from my LM-Q710(FGN) using JamiiForums mobile app
 
Ngoja niwape hii. Miaka hiyo nasoma Mtendeni kwa Ally Futo, tunaishi posta mtaa wa Libia dada yangu anaishi Ubungo zile kota ndogo jirani na RUBADA. Akawa amekuja kututembelea jumapili. Ilipofika jioni tukamsindikiza na mdogo wangu ili akapande basi Mnazi mmoja. Wakati huo kuna njia katikati ya bustani. Kabla hajapanda Ikarus akatupa dala ili tugawane kila mtu shilingi mbili na senti hamsini. Wakati tunarudi tukiwa kwenye zile njia za bustani nikamwambia mdogo wangu hela imeanguka. Nikajifanya naitafuta wakati hela iko mfukoni. Na yeye akainama, mara akatokea mtu akauliza mnatafuta nini mwenzangu akamjibu tumeangusha shilingi tano. Yule mtu akaanza kutafuta wakaanza kuongezeka watu wengi. Sasa jinsi ya kusema kwamba nilikuwa natania nikawa naogopa kwa sababu kulikuwa na watu wazima.
Jinsi ya kumwambia mwenzangu tuondoke nashindwa. Nikasogea pembeni nikatoa hela mfukoni huku nikiwa natetemeka, nimeinama nikasema hii hapa. Wakati huo watu kibao na wamechafuka mikono kwa vumbi.
Ni kwamba watu walikuwa wema sana au kila mtu alitamani aiokote halafu aminyie?

Sent from my LM-Q710(FGN) using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom