Wazanzibar kuongoza Wizara/Taasisi zisizo za Muungano imekaaje kisheria?

Katiba ina mikanganyiko mingi. Nipo kwenye mashauriano na wanasheria tukianzia na hili la DC Iringa.

Wakiona kuna mashiko nitasonga mahakamani kuomba tafsiri sahihi.
Vilevile wapitie na teuzi nyingine za huko nyuma kuliwahi kuwepo mkuu wa wilaya, Ded, mkuu wa mkoa, Ras, Das kutoka zanzibar kama haijawahi tokea basi washauri wa Rais wanatest zari.
 
Katiba mkuu ndiyo inatoa huo uhalali wa mzanzibar kuwa Rais wa jmt, jiulize kwanini hatulalamikii wabunge kutoka Zanzibar kuwepo pale Dodoma? ?? Ni kwa sababu wako pale kwa mujibu wa katiba.
 
How comes CFD ambaye ni mmoja hawezi kucommand hivyo vikozi vya Zanzibar ambayo ni Tanzania?..Huu muungano wetu huu..una maswali mengi.

..cdf hawezi ku-command kmkm na jku kwasababu vyombo hivyo si sehemu ya jwtz.

..kmkm na jku wako chini ya serikali ya mapinduzi Zanzibar na hawafanyi kazi nje ya mipaka ya Znz.
 

..East African Community wanapendekeza confederation baina ya nchi wanachama.

..kuna kamati ya wataalamu wa sheria inafanyia kazi suala hilo kabla ya kuliwasilisha rasmi kwa nchi wanachama.

..Ikiwa Confederation ya EAC itakubaliwa itabidi Tanganyika na Zanzibar ziwe na uanachama tofauti badala ya kujiunga kama nchi moja, Tanzania.

..Nadhani hata Mwalimu Nyerere aliwahi kuzungumzia hatima ya muungano wetu ikiwa nchi za Afrika Mashariki zitaamua kuungana.
 
Maandamano mazuri ni kama lile Fuso limeandikwa katiba mpya.
Kila mabandiko yaandikwe Katiba mpya,haihitaji nguvu kubwa ni akili.
 
haya mambo huanza huko mitaani, watu wanasema mama anateuwa vibarakshea sana
 
Maandamano mazuri ni kama lile Fuso limeandikwa katiba mpya.
Kila mabandiko yaandikwe Katiba mpya,haihitaji nguvu kubwa ni akili.
Watawala huwa na kiburi sana ndugu. Hasa pale kinachofanywa hakitishii kiti chake hujifanya Wana ngozi ngumu mno.

Hivyo hiyo mbinu inayopendekeza wala haitawatisha.
 
Zanzibar imewekea vikwazo baadhi inchi kumi kuingia nchinin kwao kwa sababu ya Covid ikiwataka kufanyiwa vipimo vya haraka kabla ya kuingia , kwenye comment section nkaona baadhi ya wazanzibari wakisema wawawekee na watanganyika vikwazo pia.

Huu muungano hauleweki yanii
 
Watawala huwa na kiburi sana ndugu. Hasa pale kinachofanywa hakitishii kiti chake hujifanya Wana ngozi ngumu mno.

Hivyo hiyo mbinu inayopendekeza wala haitawatisha.
Kaka vilungu watanzania waoga Sana ,tunafanyaje Sasa mkuu
 
Tusubiri kidogo tu kile kizazi kilichoshuhudia Uhuru na Muungano kiishe, si hawataki kuweka wazi sababu na faida zake…. ni suala la muda tu.
 
Ndugu zanguni kuna jambo hamli juwi.
Kuna wapiga kura nama mbili Tanzania.
Watanzania na wazanzibari watanzania
Wanao mchaguwa Rais watanzania ni watanzania wote ukijumuisha na wazanzibari ( Kwa mujibu wa katiba Zanzibar ni sehemu ya Tanzania)
Kwa hivyo wana haki kuitumikia na kufanya kazi serikali ya JMT

Wazanzibari ni watanzania na wanahaki ya kufanya kazi popote katika Tanzania na katika JMT.

Walio na haki ya kufanya kazi katika serikali ya Zanzibar ni wale wanaopiga kura kuichaguwa serikali ya Zanzibar.
Si watanzania wote wanaweza kupiga kura Zanzibar, ila ni wazanzibari.

Katiba ya serikali JMT na ya CCM inatambua hilo.

Ndio maana wazanzibari hawautaki muungano huu uliokuwepo, hata tume ya Warioba umeliona hilo.
lakini nyinyi ma CCM na serkali yenu hamtaki kusikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…