Zanzibar 2020 Wazanzibar nguvu yenu Dua, amkeni usiku Tahajjud mumshitakie Mwenyezi Mungu

Haohao waajiitao WANAMAPINDUZI DAIMA NDIO WAMEIFIKISHA ZANZIBAR HAPO.
Ole wao wanaojiunga na waovu...
 
Maneno ya kwenye vijiwe vya kahawa bro.
Atakuwa amekuwa akishinda ndotoni sio kwenye box la kura. Msiongee kwa maneno kwamba kila mwaka anashinda bila ushahidi?? Anang'ang'ania uongozi sababu hataki kuwaachia vijana hyo nafasi yake. Wapiga kura tukiona sura ya mtu yuleyule muda wote obvious tunampuuza tunaona bora kuchagua sura mpya.

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
Ingia BARABARANI... kama huwez tuliza kende
 
Hahaha dua tena? Kwani Mungu hakuona uchaguzi unafanyika au alikuwa hayupo?

Dawa waseme sasa basi.
Dawa waache kumtumia mtu mmoja agombee toka sijazaliwa mpaka naanza kupata mvi. Kachoka na haaminiki
 
Yaani bado hamtosheki na mliyoyafanya mnawazuia wasiombe kwa HAKIMU MUADILIFU,sasa kama ALLAH hatoweza kijibu dua zao pindi wakiomba nyie inawababaisha nini?
 
Mungu hana muda na wajinga na wapumbavu
 
Siku zoote awaswali wala kumuomba Mungu alafu leo ndo unawaambia waswali na kuomba?
wakati wa mikutano yao yasiasa hawakumtanguliza wala kumuomba Mungu leo ndo wanajua kuna Mungu wa kumuomba?
 
Acha kuchanganya watu mkuu. watafute mbinu ya kuzuia wizi. Kama vyama vya upinzani wekeni wapelelezi serikalini ,muwalipe wawafanyie kazi ya kujua kuiba kura inafanyikaje, kisha mtafute mbinu ya kuzuia na siyo kumtumia huyo mungu wa muhamad. eti dua acha ujinga mkuu
 
Acheni utani na Dini kwa matamanio yenu yaliyofunikwa na Ujinga wa hali ya Juu

Tusomeni Dini yetu
Uislam,haukuacha kubwa wala dogo,isipokuwa umelisema na kulitolea maelezo

Tuweni makini mno


Hammaz Allah akuhifadhi na kila shari Bro
 
Acheni utani na Dini kwa matamanio yenu yaliyofunikwa na Ujinga wa hali ya Juu

Tusomeni Dini yetu
Uislam,haukuacha kubwa wala dogo,isipokuwa umelisema na kulitolea maelezo

Tuweni makini mno


Hammaz Allah akuhifadhi na kila shari Bro
Naomba unijibu, je ni halali au haramu kwa muislamu kupiga kura katika chaguzi za vyama vya kisiasa, na Je ni halali au haramu kwa muislamu kugombea nafasi yoyote ya kisiasa kupitia vyama vya siasa?

Ukijibu hayo maswali basi unaweza kujua kama unachokisema kina mashiko au la!
 

Ndugu yangu ulicho usia ni kizuri.lakini mtu hawezi kumshitakia Mola tu na kukaa kusubiri. Tumefunzwa na Mtume (S. A. W.) kuwa mwenye
mwenye kujitahidi hufuzu. Pia kuna kisa ambapo mtu alikwenda kwa Mtume (S. A. W.) na alipofika hakumfunga kamba myama wake alomtumia kwa safari yake, alipoulizwa kwa nini hakumfunga, akajibu kuwa Mola atamlindia, Mtume Muhammad (S.A.W) akamwambia umfunge kwanza halafu ndio utawakal kwa Allah kuwa atakulindia. Point yangu ni kuwa katika mafunz ya dini yetu tunaambiwa tuombe na tufanye jitihada ya kupata tulichokiomba. Huwezi kuwa unaumwa halafu ukakaa tu kwenye msala kuomba lakini hufanyi jitihada yeyote ile ya kuepukana na maradhi uliyonayo kuanzia usafi wa mazingira, kutumia dawa n.k. Tumeambiwa kabisa mola anamsaidia yule anaejisaidia.

Hatuwezi tu kukaa na kuomba dua bila ya kufanya jitihada za vitendo kuzuia dhuluma zinazoendelea visiwani. Tuombeni dua halafu tuinuke na kudai haki zetu kwa njia yeyote ile ambayo tunaamini tutaweza kufanikiwa. Dua ni lazima lakini ni lazima zifuatwe na vitendo.

Mtume Muhammad (S.A.W.) amesema mwenye kujitahidi na kujipinda (kujituma kikweli katika kutatua haja yake) hufanikiwa. Kwa hiyo kama kweli tunataka mabadiliko zanzibar basi dua pekee haitoshi kunahitajika vitendo. Vitendo gani? hapo nawaachia walioamua kuwa viongozi katika harakati za mabadiliko visiwani.
 
Swadakta vyote vifanyike.

Mpaka sasa Wazanzibar wamekuwa na subira sana, wamefuata mifumo yote tuliyokubaliana ya kinchi kupata haki zao lakini bado dhulma inazidi. Jitihada ziendane na Dua
 
Ni kweli dua ni silaha kubwa, lakini je dua ya mnafiki inakubaliwa? Maana ukweli ni kwamba ukimuondoa Maalim Seif na kikundi kidogo cha watu, walio baki wote ni wanafiki/wasaliti.
Kwa nini nasema hivyo? Kwa sababu tulimuaminisha Maalim Seif kwamba "alipo tupo" nae akatuahidi kwamba ikitokea dhulma kwenye kura yeye atakuwa mstari wa mbele kuongoza maandamano adi kieleweke. Na kweli ametekeleza ahadi yake kama alivyo ahidi. "kama wanataka kutu uwa watuuwe, kama wanataka kutukamata watufunge acha watufunge, tunakwenda kuandamana na mimi nitaongoza".

Je tuliitikia wito?
Je ni kweli alipo na sisi tupo?

Tulicho mfanyia Maalim na nchi ni usaliti na unafiki.
Unafiki ni dhambi mbaya sana. Je kwa unafiki huu dua zetu zitakubalika?
 
akili mseto

Yaani Allah na Mtume wake,hakuwafunzeni njia ya kufanya....mpaka leo unasema tutumie njia yoyote ile...?!!!

Unataka uondoshe munkar kwa kutumia Munkar

ni sawa na anaejisafisha haja kubwa kwa haja kubwa......
 
Labda niwaambie kitu kimoja ndg zangu Wazanzibar

Ikiwa mnataka Zanzibar ijitoe katika Serikali hii...na mpate Serikali nyengine itakayowapa Dunia yenu....bila ya kuchunga Mipaka ya Allah na maamrisho yake.....Basi ni sawa kutumia njia hizi mnazotumia kwasasa

Ila
Tahadhari sana
Msitumie kivuli cha Dini kwa lengo la kuipata Dunia

Wallah hamtofanikiwa hata siku moja

Dunia huletwa na Dunia yake
Mbele ya Dunia....Hakuna Halali wala Haramu...Vyote ni sawa

Lkn Dini
inahitaji ufuate kanuni zake...ikiwa mnakusudia Dini

Bila ya hivyo
mnampigia mbuzi gita
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…