Nahisi wewe utakuwa mgeni wa siasa za Tanzania.
Hapo ulipo ni Zanzibar siyo Tanganyika, Zanzibari ina Rais wake ambaye ni Dr. Hussein Mwinyi na ana mamlaka yote yanayotakiwa kwa rais nje ya muungano.
Ukiwa Tanganyika kuna Rais Mh. Samia S. Hassan ambaye kwa pande zote anabeba kofia ya muungano wa pande zote akiwa ndiye amiri jeshi, hii ni baada ya ile chapa ya wazee wetu, Julius na Abeid.
Kwenye ofisi za umma au ofisi binafsi ambayo inafaa kuwepo alama ya taifa kama picha ya kiongozi wa taifa inatakiwa iwekwe ya kiongozi aliye madarakani kama rais na siyo mstaafu, hivyo basi zanzibari tuna Rais Hussein mwenye mamlaka na visiwa hivi siyo Nyerere wala karume na mama Samia anawakilisha muungano na siyo zanzibari.