Wazanzibari walikuwa sawa. Muungano wa mkataba ndio unaofaa.

iMind

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
3,039
Reaction score
4,889
Kwa muda sasa tangu Jaji warioba akabidhi rasimu ya pili ya katiba ya muungano kumekuwa na mijadala mingi kuhusu uwepo wa serikali mbili, tatu au moja.

Kila upande umekuwa ukivutia upande wake ili kuhalalidha kuwa wayasemayo ndo sahihi. Lakini bahati mbaya kama alivyofanya Jaji Warioba kutozungumza faida au hasara za maoni ya wazanzibari wengi kuhusu muungano wa mkataba na sisi hspa jamvini hatujatoa au kutafakati kwa kina kuhusu muungano wa namna hii yaani wa mkataba.

Baada ya kusikiliza pande zote mbili nafikiri muungano wa mkataba ni more appropriate kuliko serikali 3. Itakumbukwa kuwa hata huu muungano wa serikali mbili za sasa ni wa mkataba vile vile, ila mkataba ambao unaongelewa na wazanzibari ni ule wa uwepo wa serikali mbili ya Tanganyika na Zanzibar na zenye mamlaka kamili kila moja kama nchi. Ambazo zitaamua kushirikiana kwenye mambo kadhaa. Badala ya kuwa na serikali ya tatu kwa ajili ya hayo mambo tutakayokubaliana seriksli mbili zitakubaliana kuunda chombo kama ilivyo kwa jumuiya ya afrika mashariki.

Chombo hicho ambacho kitakuwa chini wa maraisi wote wawili kama wenyeviti wakipokezana ndo kitakuwa na kazi ya kuratibu shughuli zote chini ya mkataba. Sijui wenzangu mmaonaje maana ni dhahiri kuunda serikali ya 3 ambayo ndo unataka iwe kubwa wakati inashughulikia maeneo machache tena si yale yanayogusa maisha ya watu ya kila siku italeta mgongano tu.

Angalieni kwa sasa tu jinsi bunge na serikali zilivyo na mgongano sasa ndo tuongeze serikali na bunge lingine hali itakuwaje?
 
Umenena vyema.
Ubongo wako unafanya kazi unayotakiwa kufanya.
 
Muungano wa mkataba hata haina mantiki Tanganyika haitafuti koloni la kulitawala. Huo mkataba watasainiana na nchi gani? Mana ninachoelewa mkataba ni makubaliano ambayo yatafanya nchi fulani ije ikutawale ie uwe koloni lake, sasa kwanini wasiende kwa wazungu au waraabu wakatiliane mkataba.
 
Kama serikali mbili haikuwezekana hata Tatu hatutaziweza ,cha msingi kila mtu achukue chake,tuwe majirani wema tu.
 
Muungano wa mkataba hata haina mantiki Tanganyika haitafuti koloni la kulitawala. Huo mkataba watasainiana na nchi gani? Mana ninachoelewa mkataba ni makubaliano ambayo yatafanya nchi fulani ije ikutawale ie uwe koloni lake, sasa kwanini wasiende kwa wazungu au waraabu wakatiliane mkataba.

ww unaongea pombe hukijuwi ata unachokiadika wala kinachojadiliwa., wazungu na warab vip na wapi kwani European union waliwatafuta nchi za mbali kwenda kuunda mkataba wao wa muungano??
 
Kwani makubaliano kama ya africa mashariki au ulaya ni nchi gani imeitawala nyingine? Hapa kinachotakiwa ni ushirikiano utakao saidia nchi zote mbili kukua ki uchumi, na kijamii. Ukiangalia historia na Zanzibar ni Ndugu zetu wa damu. Tunaweza kushirikiana kama nchi mbili na kuleta muungano dhabiti kabisa kuliko huu wa sasa na ule ambao warioba anaupendekeza.

Cha msingi kujua hapa Zanzibar ilikuwa nchi inayojitegemea toka Zama hizo na walipigana kupata uhuru wao wenyewe. Hivyo kuweka serikali moja na kuifanya zanziba kama mkoa ni kitu kisichowezekana. Na kuunda serikali tatu, ambapo serkali ya 3 ya Tanganyika itahusika na mambo 7 tu yaliyopendekezwa na muungano italeta changamoto.

Imagine Raisi wa Tanganyika kutokuwa na mamlaka ya Jeshi wala Polisi. Ataongoza vipi nchi.

Kwa sasa Rais wa Muungano ni kama Rais wa Tanganyika tu. Mambo mengi ambayo ni ya muungano huko zanziba yamekuwa yakiendeshwa na Serikali ya Zanzibar chini wa Rais wa Zanzibar. Rais wa Muungano hana msdaraka yoyote juu ya mambo ya Zanzibar. Yaani kule Zanziba ni ceremonial president tu. Lakini kila kitu wanamalizana wenyewe.

So utakapo leta Rais wa muungano ambaye hana mamlaka Zanzibar wala Tanganyika isipokuwa mambo 7 tu will not work. Ukizingatia hayo mambo yote hayafanyiki in isolation. Yote yanategemeana. Ina maana Rais wa Tanganyika anaweza akakwama kutekeleza mambo flani kwa sababu anasubiri Rais wa Tanganyika and vice versa na Zanzibar hivyo hivyo. Tutashuhudia vurugu za ajabu na nchi haitatawalika. Trust me.
 
Siyo lazima nchi washirika kuwa na cheo cha Raisi mnaweza mkawa na mawaziri wakuu wenye nguvu na mamlaka ndani ya nchi zao, Au mkawa na Rais wa wa Muungano asiyekuwa na nguvu akawa kama ujerumani au Islaeri nk wanavyofanya. Tatizo huo mkataba unamlazimisha nani? kwani tulivyoungana mwaka 1964 hawakusaini mikataba?

Kwani makubaliano kama ya africa mashariki au ulaya ni nchi gani imeitawala nyingine? Hapa kinachotakiwa ni ushirikiano utakao saidia nchi zote mbili kukua ki uchumi, na kijamii. Ukiangalia historia na Zanzibar ni Ndugu zetu wa damu. Tunaweza kushirikiana kama nchi mbili na kuleta muungano dhabiti kabisa kuliko huu wa sasa na ule ambao warioba anaupendekeza.

Cha msingi kujua hapa Zanzibar ilikuwa nchi inayojitegemea toka Zama hizo na walipigana kupata uhuru wao wenyewe. Hivyo kuweka serikali moja na kuifanya zanziba kama mkoa ni kitu kisichowezekana. Na kuunda serikali tatu, ambapo serkali ya 3 ya Tanganyika itahusika na mambo 7 tu yaliyopendekezwa na muungano italeta changamoto.

Imagine Raisi wa Tanganyika kutokuwa na mamlaka ya Jeshi wala Polisi. Ataongoza vipi nchi.

Kwa sasa Rais wa Muungano ni kama Rais wa Tanganyika tu. Mambo mengi ambayo ni ya muungano huko zanziba yamekuwa yakiendeshwa na Serikali ya Zanzibar chini wa Rais wa Zanzibar. Rais wa Muungano hana msdaraka yoyote juu ya mambo ya Zanzibar. Yaani kule Zanziba ni ceremonial president tu. Lakini kila kitu wanamalizana wenyewe.

So utakapo leta Rais wa muungano ambaye hana mamlaka Zanzibar wala Tanganyika isipokuwa mambo 7 tu will not work. Ukizingatia hayo mambo yote hayafanyiki in isolation. Yote yanategemeana. Ina maana Rais wa Tanganyika anaweza akakwama kutekeleza mambo flani kwa sababu anasubiri Rais wa Tanganyika and vice versa na Zanzibar hivyo hivyo. Tutashuhudia vurugu za ajabu na nchi haitatawalika. Trust me.
 
Kwani tulivyoungana 1964 hatukutiliana mikataba? we ndiye unayetaka kulazimisha mnakomalia muungano wa mkataba kwanani? Mbona sisi Hatujawahoji au kushinikiza mambo yetu myakubali?

ww unaongea pombe hukijuwi ata unachokiadika wala kinachojadiliwa., wazungu na warab vip na wapi kwani European union waliwatafuta nchi za mbali kwenda kuunda mkataba wao wa muungano??
 
Kwani tulivyoungana 1964 hatukutiliana mikataba? we ndiye unayetaka kulazimisha mnakomalia muungano wa mkataba kwanani? Mbona sisi Hatujawahoji au kushinikiza mambo yetu myakubali?

1964 ule muungano karume hakujuwa athari yk baadae itakuwaje mzee nyerere alimzidi nguvu karume na kuweka mambo mengi pole pole na sasa ikawa Zanzibar kama imetawaliwa na Tanganyika., sasa mkataba unaoogelewa saivi ni kuchagua mambo ambayo pande zote 2 itaona zinafaa kuungana bila kuzid na kupungua pia kuwe na Option ya mmoja kujitoa juu ya jambo fulani au kujitoa kabisa kwenye huo mkataba wa muungano endapo hakutakuwa na manufaa., tunaongelea mkataba huo ndugu,
 
Ninyi ni kawaida yenu kulalamika hamridhiki, 2011 mlikuwa na vuguvugu la kuukataa muungano sijui mliishia wapi!, sasa mnataka wa mkataba. Hivi nasisi tukiweka masharti yetu mtaweza kuhimili ninyi! Usimwone kobe kainama............., Ningetegemea mngedai kura ya maoni kwanza ili tujue kama tunauhitaji Muungano halafu ndiyo tuzungumze.

Tatizo la mkataba wa sasa ulimtaka Rais wa Tanganyika ndo ashughulikie mambo ya muungano. Hivyo kufanya wa Zanzibari kujiona wanyonge kila siku. What if mambo ya muungano yakawa yanaongozwa kwa awamu. Miaka 5 Rais wa Tanganyika, miaka mitano Rais wa Zanzibar. What if kukaundwa chombo cha kuratibu mambo ya muungano. Marais wote wawili wakawa wakuu wa chombo hicho, wenye kura za veto. Options ziko nyingi ila Serikali 3 hata kama ukawa na mawaziri wakuu bado italeta mtafaruku.

Angalia tu sasa hivi, manaibu waziri na mawaziri hawaivi chungu kimoja. Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi hawaivi chungu kimoja. Mawaziri na makati wakuu hawaivi chungu kimoja. Je itakuwaje kwa Rais wa Muungano ba Rais wa Tanganyika na Zanzibar. Ukikuta ndo wa vyama tofauti sasa. Watakao umia ni wananchi. Mfumo wa serikali 3 utakuwa na changamoto nyingi sana.
 
Mfumo kristo hauwezi kukubali muungano wa mkataba na zanzibar kwa sababu kanisa halitopata nafasi ya kuitawala zanzibar.
 
Ninyi ni kawaida yenu kulalamika hamridhiki, 2011 mlikuwa na vuguvugu la kuukataa muungano sijui mliishia wapi!, sasa mnataka wa mkataba. Hivi nasisi tukiweka masharti yetu mtaweza kuhimili ninyi! Usimwone kobe kainama............., Ningetegemea mngedai kura ya maoni kwanza ili tujue kama tunauhitaji Muungano halafu ndiyo tuzungumze.

Siku zote ufahamu Zanzibar hawana shida ya Muungano na Tanganyika., na kama itapigwa kura wazanzibari zaidi ya 80% wataukataa muungano, lakini ilionekana kuwa makada wa CCM kutoka Tanganyika wazo hilo hawatalikubali kwasababu ya manufaa ya nchi yao ya Tanganyika wanayoyapata kuinyonya Zanzibar, ndio sasa Zanzibar basi ikasema kama ni Muungano uwe wa Mkataba pia mumekataa mumeleta JMT iwe nchi tena kwenye rasimu ili muwe na mamlaka pia kuendelea kuinyonya zanzibar,
 
Thubutu tena wananchi wanautaka sana tatizo ni hao wanasiasa wenu ambao wanapaspoti 2, na wanao ungwa mkono na Omani, Wananchi wanajua jinsi biashara ilivyowasidia kukidhi riziki zao, Wazanzibar wametepakaa mikoani huku Tanganyika wapo huru wanafanya biashara zao salama, wanjenga majumba hakuna taabu hafu leo uwaambie eti hamuutaki muungano wakukubalie.

Siku zote ufahamu Zanzibar hawana shida ya Muungano na Tanganyika., na kama itapigwa kura wazanzibari zaidi ya 80% wataukataa muungano, lakini ilionekana kuwa makada wa CCM kutoka Tanganyika wazo hilo hawatalikubali kwasababu ya manufaa ya nchi yao ya Tanganyika wanayoyapata kuinyonya Zanzibar, ndio sasa Zanzibar basi ikasema kama ni Muungano uwe wa Mkataba pia mumekataa mumeleta JMT iwe nchi tena kwenye rasimu ili muwe na mamlaka pia kuendelea kuinyonya zanzibar,
 
Mfumo kristo hauwezi kukubali muungano wa mkataba na zanzibar kwa sababu kanisa halitopata nafasi ya kuitawala zanzibar.

Sidhani kama ni mfumo kristo. Nchi nyingi duniani sasa zinatafuta kuungana na nyingine ili kujenga nguvu za kiuchumi kwa pamoja. Tatizo la wazanzibar ni kwamba kila mmoja alikuwa anasema tunataka muungano wa mkataba halafu mnaidhia hapo. Hamkwenda mbali kuiambia tume huo mkataba uweje na uhusishe mambo gani na kivipi. Na tume ilivyokuwa haikuchambua kwa kina mkataba mnaoutaka na hivyo kutupilia mbali. Lakini binafsi nafikiri kuna haja ya msingi kuwa na muungano wa mkataba. Baadae kidogo nitakuja na mambo ya msingi kuwa katika mkataba.
 
Thubutu tena wananchi wanautaka sana tatizo ni hao wanasiasa wenu ambao wanapaspoti 2, na wanao ungwa mkono na Omani, Wananchi wanajua jinsi biashara ilivyowasidia kukidhi riziki zao, Wazanzibar wametepakaa mikoani huku Tanganyika wapo huru wanafanya biashara zao salama, wanjenga majumba hakuna taabu hafu leo uwaambie eti hamuutaki muungano wakukubalie.

Ndio mana nikasema kabla kwamba akili yako ina acid: Ivi kwani kwa akili yako Wazanzibari wametapakaa kwenye Ardhi ya Tanganyika tu?? wazanzibar wapo Uk., wapo Canada, wapo Marekani wapo Dubai, wapo China, wapo Finland wapo Ujerumani wapo Australia wapo kila nchi duniani wanatafuta hizo hizo riziki zao kwaiyo unataka kuniambia tumeungana na hizo NCHI??? mm nipo Holand mwaka 7 sasa na ni mzanzibar na sidhan kama Holand imeungana na Zanzibar or Tz.,

Ni upeo wenu finyu wa mawazo na fikra mbovu, lakini pia kutokutemebea duniani mukaona hali halisi ya mambo inachangia akili yenu kuwa mgando.,
 
Andamaneni muukatae huo MUUNGANO,

Ndio mana nikasema kabla kwamba akili yako ina acid: Ivi kwani kwa akili yako Wazanzibari wametapakaa kwenye Ardhi ya Tanganyika tu?? wazanzibar wapo Uk., wapo Canada, wapo Marekani wapo Dubai, wapo China, wapo Finland wapo Ujerumani wapo Australia wapo kila nchi duniani wanatafuta hizo hizo riziki zao kwaiyo unataka kuniambia tumeungana na hizo NCHI??? mm nipo Holand mwaka 7 sasa na ni mzanzibar na sidhan kama Holand imeungana na Zanzibar or Tz.,

Ni upeo wenu finyu wa mawazo na fikra mbovu, lakini pia kutokutemebea duniani mukaona hali halisi ya mambo inachangia akili yenu kuwa mgando.,
 
Kwa muda sasa tangu Jaji warioba akabidhi rasimu ya pili ya katiba ya muungano kumekuwa na mijadala mingi kuhusu uwepo wa serikali mbili, tatu au moja.

Kila upande umekuwa ukivutia upande wake ili kuhalalidha kuwa wayasemayo ndo sahihi. Lakini bahati mbaya kama alivyofanya Jaji Warioba kutozungumza faida au hasara za maoni ya wazanzibari wengi kuhusu muungano wa mkataba na sisi hspa jamvini hatujatoa au kutafakati kwa kina kuhusu muungano wa namna hii yaani wa mkataba.

Baada ya kusikiliza pande zote mbili nafikiri muungano wa mkataba ni more appropriate kuliko serikali 3. Itakumbukwa kuwa hata huu muungano wa serikali mbili za sasa ni wa mkataba vile vile, ila mkataba ambao unaongelewa na wazanzibari ni ule wa uwepo wa serikali mbili ya Tanganyika na Zanzibar na zenye mamlaka kamili kila moja kama nchi. Ambazo zitaamua kushirikiana kwenye mambo kadhaa. Badala ya kuwa na serikali ya tatu kwa ajili ya hayo mambo tutakayokubaliana seriksli mbili zitakubaliana kuunda chombo kama ilivyo kwa jumuiya ya afrika mashariki.

Chombo hicho ambacho kitakuwa chini wa maraisi wote wawili kama wenyeviti wakipokezana ndo kitakuwa na kazi ya kuratibu shughuli zote chini ya mkataba. Sijui wenzangu mmaonaje maana ni dhahiri kuunda serikali ya 3 ambayo ndo unataka iwe kubwa wakati inashughulikia maeneo machache tena si yale yanayogusa maisha ya watu ya kila siku italeta mgongano tu.

Angalieni kwa sasa tu jinsi bunge na serikali zilivyo na mgongano sasa ndo tuongeze serikali na bunge lingine hali itakuwaje?

Sasa Wazanzibar huo mkataba watasaini na nani wakati serikali ya Tanganyika haipo? Huoni kuwa ni muhimu Tanganyika ianzishwe kwanza ndipo tujadili kuhusu huo mkataba hapo baadae?
 
Back
Top Bottom