Kwa muda sasa tangu Jaji warioba akabidhi rasimu ya pili ya katiba ya muungano kumekuwa na mijadala mingi kuhusu uwepo wa serikali mbili, tatu au moja.
Kila upande umekuwa ukivutia upande wake ili kuhalalidha kuwa wayasemayo ndo sahihi. Lakini bahati mbaya kama alivyofanya Jaji Warioba kutozungumza faida au hasara za maoni ya wazanzibari wengi kuhusu muungano wa mkataba na sisi hspa jamvini hatujatoa au kutafakati kwa kina kuhusu muungano wa namna hii yaani wa mkataba.
Baada ya kusikiliza pande zote mbili nafikiri muungano wa mkataba ni more appropriate kuliko serikali 3. Itakumbukwa kuwa hata huu muungano wa serikali mbili za sasa ni wa mkataba vile vile, ila mkataba ambao unaongelewa na wazanzibari ni ule wa uwepo wa serikali mbili ya Tanganyika na Zanzibar na zenye mamlaka kamili kila moja kama nchi. Ambazo zitaamua kushirikiana kwenye mambo kadhaa. Badala ya kuwa na serikali ya tatu kwa ajili ya hayo mambo tutakayokubaliana seriksli mbili zitakubaliana kuunda chombo kama ilivyo kwa jumuiya ya afrika mashariki.
Chombo hicho ambacho kitakuwa chini wa maraisi wote wawili kama wenyeviti wakipokezana ndo kitakuwa na kazi ya kuratibu shughuli zote chini ya mkataba. Sijui wenzangu mmaonaje maana ni dhahiri kuunda serikali ya 3 ambayo ndo unataka iwe kubwa wakati inashughulikia maeneo machache tena si yale yanayogusa maisha ya watu ya kila siku italeta mgongano tu.
Angalieni kwa sasa tu jinsi bunge na serikali zilivyo na mgongano sasa ndo tuongeze serikali na bunge lingine hali itakuwaje?