Wazanzibari walikuwa sawa. Muungano wa mkataba ndio unaofaa.

Wazanzibari walikuwa sawa. Muungano wa mkataba ndio unaofaa.

Thubutu tena wananchi wanautaka sana tatizo ni hao wanasiasa wenu ambao wanapaspoti 2, na wanao ungwa mkono na Omani, Wananchi wanajua jinsi biashara ilivyowasidia kukidhi riziki zao, Wazanzibar wametepakaa mikoani huku Tanganyika wapo huru wanafanya biashara zao salama, wanjenga majumba hakuna taabu hafu leo uwaambie eti hamuutaki muungano wakukubalie.

Ww shida yako ni nn hasa? Unajua km ukishuka tu bandarin znz ndugu zako wamejaa wanauza vinyago? Tena hao wa upande wa pili wakija tanganyika shida iko wapi? Watu munacomment as if wazanzibar hawawezinkuishi bila ya mkono wa tanganyika!...st****
 
Sasa Wazanzibar huo mkataba watasaini na nani wakati serikali ya Tanganyika haipo? Huoni kuwa ni muhimu Tanganyika ianzishwe kwanza ndipo tujadili kuhusu huo mkataba hapo baadae?

Kwani kunahitaji mchakato mkubwa kiasi gani kurudisha Tanganyika mkawa na katiba yenu na kule Zanzibar mda huohuo masharti ya mkataba wa kuungana yanakuwepo? nyinyi Tanganyika mambo munayafanya makubwa ata kufungua mlango wa gari munasema inahitahi muda
 
Katiba haisjisimamii yenyewe lazima pawepo viongozi watakaosimamia katiba hiyo, mfano Rais au Waziri Mkuu wa Tanganyika na taasisi zake kama ilivyo kwa Zanzibar hao ndio watasimamia utiaji saini wa mkataba.
 
Nashukuru mtoa mada kwa kuelewa kuwa swala la muungano wa mkataba kwa sasa limekosa mashiko kwa kuwa serikali ya Tanganyika haipo. hivyo ninawashauri Wazanzibar wote waunge mkono kuanzishwa kwa serikari ya Tanganyika ili baadae serkali ya Zanzibar ijadiliane na serikali ya Tanganyika kuhusu muungano wa mkataba, tofauti na hapo ni ubishi na malalamiko yasiyo na hoja.
 
Katiba haisjisimamii yenyewe lazima pawepo viongozi watakaosimamia katiba hiyo, mfano Rais au Waziri Mkuu wa Tanganyika na taasisi zake kama ilivyo kwa Zanzibar hao ndio watasimamia utiaji saini wa mkataba.

Kwani tatizo liko wapi ingefanyika hivyo ili tukawa na huwo mkataba wa pande 2., ni woga na hofu ya CCM tu., muda si issue kuliko kutekeleza matakwa ya wananchi kupata katiba bora inayokidhi maisha ya watu kwa sasa.,
 
Jiondoeni kwani mmelazimishwa? Mmeanza kuapizana na mnataka wanaotaka serikali 3 wajieleze wanufaa yao ni yapi

Ww shida yako ni nn hasa? Unajua km ukishuka tu bandarin znz ndugu zako wamejaa wanauza vinyago? Tena hao wa upande wa pili wakija tanganyika shida iko wapi? Watu munacomment as if wazanzibar hawawezinkuishi bila ya mkono wa tanganyika!...st****
 
Tanganyika haina tabia hizo bali viongozi wenu ndo wanaotaka, naona baada ya CUF kuingia madarakani ile kasi ya kuupinga muungano imeisha kabisa

Tukiandamana kuukataa Muungano Tanganyika itatupiga mabomu.,
 
Tanganyika haina tabia hizo bali viongozi wenu ndo wanaotaka, naona baada ya CUF kuingia madarakani ile kasi ya kuupinga muungano imeisha kabisa

narudia tena msimamo wa kuuvunja muungano sio wa CUF tu bali ni kwa wazanzibar wote hadi kesho, ila kwa vile ndugu zetu wa Tanganyika wamekalia vibaya ata kuuwa watu ndio tukapendekeza muungano wa mkataba angalau na hata huo mkataba wamekataa wameleta serikali 3 kwenye rasim
 
Kama ni Wazanzibar wote hamuutaki muungano iweje mpendekeze serikali muutake uendelee kuwepo? Unadhani hatuwaoni?

narudia tena msimamo wa kuuvunja muungano sio wa CUF tu bali ni kwa wazanzibar wote hadi kesho, ila kwa vile ndugu zetu wa Tanganyika wamekalia vibaya ata kuuwa watu ndio tukapendekeza muungano wa mkataba angalau na hata huo mkataba wamekataa wameleta serikali 3 kwenye rasim
 
Mkuu ukiacha mawazo na mitazamo ya wanasiasa, wewe pale Kijijini kwako au mtaani kwako mnapokuwa na mijadala au mikutano ya kero za maendeleo, ni mara ngapi au kwa asilimia ngapi umeshawahi kusikia wananchi wa kawaida wakielezea jinsi muungano unavyoathiri maisha yao ya kila siku?? Nakuhakikishia kama una uwezo wa kutembelea vijiji 100 vya nchi hii (Tanganyika) na ukauliza kero zao kuu hutasikia kabisa walitaja kero ya muungano, achilia mbali aina ya muungano au hata neno muungano!!! Ukisikia wanaosema muungano wa serikali moja, mbili, tatu nne, shirikisho etc ni siasa tuuu!! ndiyo maana sitegemei hata mara moja kuwepo na kura ya maoni kuamua SIYO TU KUWAULIZA WATZ WANATAKA AINA GANI YA MUUNGANO BALI JE WANAUTAKA MUUNGANO WENYEWE? Wanasiasa sasa hivi wanasumbuliwa na mambo kama niwe Rais wa Muungano? wa Zanzibar, wa Tanganyika? etc. Wengine wanadai wanawaenzi waasisi wa muungano!! kwani mambo ya kuwaenzi waasisi hawa ni muungano na muundo wake tuu? vp kuhusu ufisadi? rushwa? uzalendo na mengine??
 
Ww shida yako ni nn hasa? Unajua km ukishuka tu bandarin znz ndugu zako wamejaa wanauza vinyago? Tena hao wa upande wa pili wakija tanganyika shida iko wapi? Watu munacomment as if wazanzibar hawawezinkuishi bila ya mkono wa tanganyika!...st****

Dada acha dharau kuwa na kauli nzuri watanganyika wote waliopo znz wanauza vinyago??? Acheni mambo ya kibaguzi tatizo huwa hamjifunzi kutokana na makosa waliyofanya nchi za wenzetu. Kuweni na mtazamo sahih na si kutanguliza maneno ya kashfa na kibaguzi. muungano unahitajika sana kulinda maisha ya watanganyika na wazanzibar coz kuvunjika kwa muungano ni kuvunjika kwa Unnguja na Pemba coz baada ya kuvunjika kitakachofuata watu kuishi kwa sheria za nchi husika ndio hapo maisha yatakapokuwa magumu kwa wapemba waliojisahau kwa kujenga na kuwekeza kila kitu chao Tanganyika na hapo sasa ndo watakaporudi kuja kudai nchi yao coz Pemba ilisahaulika ndo wakakimbilia Tanganyika na mpaka sasa bado Pemba imetelekezwa sijui mtawaimbia nyimbo gani...
 
Kijana jibu hoja matusi hayakusaidii, Mkiongeo kwenye tv mnajifanya muungano hatuuataki, mkiwa nyuma ya kamera hoo! Tunataka muungano uendelee sisi tupo kimya tunawaoneni.

1. Nimekujibu mara elf1 zanzibar muungano na tanganyika hautakiwi kwa asilimia kubwa., reason Tanganyika inainyonya Zanzibar.

2. Kwa sababu wahafidhina na kanisa Tanganyika wanafaidika na muungano hawako tayri kwa vyovyote iwavyo kuvunja muungano ndio mana wazanzibari basi wakasema kama haiwezekani kuvunja muungano basi tuwe na muungano wa mkataba angalau kupunguza makali ya muungano kuendelea kuiangamiza zanzibar ili wakubaliane kwa baadhi ya mambo tu.

3. Sasa unaposema kwenye Tv unaona tunasema tunautaka ndio hawo wahafidhina na vibaraka ambao hutumiliwa na kufaidika akina shamsi na wenzake.

4. Usiwe mbabaifu hakuna mtanganyika hata 1 asiyejuwa kuhus zanzibar kwamba muungano hawautaki.,
 
Serikali ya CCM inapenda sana kupeleka mambo kimzaha mzaha, kabla ya kuanza
kusanya maoni ya katiba mpya walipaswa kukusanya maoni ya muungano (usiwepo au uwepo kwa muundo upi) hayo tuliwashauri lakn wakayapuuza leo sasa wengine wanautaka, wengine hawautaki kabisa, wengine wanataka uwe na seriali 3, wengine wanataka uwe wa mkataba.......
Haya yote ndo yalipaswa kujulikana kabla ya katiba mpya tena kwa pande zote mbili.
Mwanzo wakati uamsho wanajadili muungano walioneka wahalifu na magaidi coz Wanaccm na watanganyika walidhani zile hoja hazitawagusa wakaangalia action zao na wakasahau kuangalia hoja zao. Kwa kukumbusha tu migomo na maandamo kipindi cha Trade Unionism in UK kuna kiongozi alisema "tutawashinda kudhibiti action zao lakin tutashindwa na hoja zao sasa ni muda wa kujadili hoja zao". Hivyo ingawa Uamsho matendo yao ya kibaguzi waliyoyafanya siyakubali wala hayakubaliki ulimwenguni kote na hata katk dini yetu tukufu ya uislam lakn hoja zao zilitakiwa kutafakariwa.
 
chukueni hatua msibaki na manung'uniko yakaja kutuumiza nasisi.

1. Nimekujibu mara elf1 zanzibar muungano na tanganyika hautakiwi kwa asilimia kubwa., reason Tanganyika inainyonya Zanzibar.

2. Kwa sababu wahafidhina na kanisa Tanganyika wanafaidika na muungano hawako tayri kwa vyovyote iwavyo kuvunja muungano ndio mana wazanzibari basi wakasema kama haiwezekani kuvunja muungano basi tuwe na muungano wa mkataba angalau kupunguza makali ya muungano kuendelea kuiangamiza zanzibar ili wakubaliane kwa baadhi ya mambo tu.

3. Sasa unaposema kwenye Tv unaona tunasema tunautaka ndio hawo wahafidhina na vibaraka ambao hutumiliwa na kufaidika akina shamsi na wenzake.

4. Usiwe mbabaifu hakuna mtanganyika hata 1 asiyejuwa kuhus zanzibar kwamba muungano hawautaki.,
 
Kuamua kwenu siyo lazima mkiwa na serikali3, Muungano ni mali ya wananchi wakiamua kuukataa viongozi hawawezi kuulinda hata kwa nguvu ya jeshi.

Hatua ni pole pole ukila na kipofu usimshike mkono., serikali 3 zikiwepo ni rahisi kuukwamisha muunga na kuutokomeza kuliko ilivyo sasa.,
 
Back
Top Bottom